Unajua sikuwa namtazama Jane Shirima? Jana kwenye kipindi cha TUAMBIE alikuwa anawaburuza watazamani waliokuwa wakipiga simu, alikuwa anawakatisha akidai kwamba kuna simu nyingi! WAPI! Huyu anatafuta maslahi CCM, anajua kwamba akiishabikia CCM atakuja kuula baadaye, anajipendekeza. Tatizo ni kwamba, upo uwezekano wa CCM kutokurejea madarakani. Kampeni ya CHADEMA ni KALI, ni mwiba kwa CCM.
Tundu Lissu ameuonesha Mkataba wa Bulyankhulu kwenye umma wa Watanzania, na kumwuliza Jakaya aseme ni lini atawaomba radhi Watanzania kwa kusaini mkataba uliosababisha Watanzania wafe kule Bulyankhulu, na lini atamwomba yeye (Tundu Lissu) radhi kwa kusababisha akamatwe kwa jambo lile lile ambalo Jakaya alisema ni uchochezi, huku leo anasema atawalipa fidia wakazi wa Bulyankhulu?!
Hatudanganyiki na hivyo vipindi vyenu vya muziki, na upuuzi mwingine! CHADEMA wamewasha moto, ambao hautazimika mpaka Oktoba 31, 2010!
-> Mwana wa Haki
Amandla! Awetu! Amandla! Maatla! People's Power! Power to All the People!