Ufunguzi wa Mkutano maalumu wa baraza la Vyama vya Siasa 03 Januari 2024

Ufunguzi wa Mkutano maalumu wa baraza la Vyama vya Siasa 03 Januari 2024

Nchi ya Mungu huzungumza pamoja.
ff2436ab-98fc-4abb-88bb-c3d94fe414e7.jpg
 
Baraza la Vyama vya Siasa limeundwa ndani ya Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa. Wajumbe wa Baraza hili hujumuisha viongozi wa kitaifa wawili wa kila chama cha siasa chenye usajili wa kudumu. Ofisi ya Msajili wa Vyama vya siasa ndio yenye jukumu la kisheria ya kuratibu shughuli za Baraza la Vyama vya Siasa.

Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa na Makamu Mwenyekiti huchaguliwa kwa kupigiwa kura na wajumbe wa Baraza.

Majukumu ya Baraza la Vyama vya Siasa

1. Kumshauri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya mgogoro inayotokea kwenye vyama vya siasa;
2. Kumsahuri Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya masuala yenye maslahi kwa Taifa kuhusiana na vyama vya siasa au kuhusiana na hali ya kisiasa nchini;
3. Kuishauri Serikali kupitia kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya kupitishwa kwa marekebisho na utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa na sheria zingine zinazohusu masuala ya vyama vya siasa;
4. Kushauri juu ya kanuni zinazosimamia masuala yanayohusu vyama vya siasa;
5. Kutoa taarifa kwa Msajili wa Vyama vya Siasa juu ya uendeshaji wa chama chochote cha siasa.
6. Kugawana ulaji wa kodi za wananchi kwa njia ya posho!
 
Maisha ni kutafakari kwa pamoja. Nchi inayoongozwa vyema ni mazungumzo
ffd303aa-db06-4cb9-9929-d6f3d0436926.jpg
 
Watanzania wanatoa maoni yao. Acha kulalama
88d64388-f33f-4930-87b4-6cefd9403b38.jpg
 
Hekima, Umoja na Amani
Hizi ni ngao zetu.
Maneno haya ukiyatafakari kwa kina utajua sisi ni nchi ya kipekee sana hapa duniani.
Utapeli mtupu! Vipi kuhusu tume huru ya uchaguzi na katiba mpya? Kuna hata moja mmefanikiwa? Sasa nini kipya zaidi ya posho kwa Wajumbe?
 
Mada nzuri, maoni yangu ili demokrasia nchini itamalaki ni,kukifuta cheo cha msajili wa vyama, vyama vyote vya kisiasa vinavyotaka kushiriki kwenye chaguzi, vijisajili kwa tume huru ya uchaguzi,NEC, hawa NEC ndio wenye uchaguzi na LAZIMA wawe na watumishi wao kwa ngazi zote za kichaguzi na sio kutegemea watumishi wa serikali, pia NEC ndiye awe msimamizi wa katiba zote za political parties, na hii itaifanya NEC pia isimamie chaguzi za vyama vya siasa (uchaguzi wa viongozi ndani ya political party)
 
Utapeli mtupu! Vipi kuhusu tume huru ya uchaguzi na katiba mpya? Kuna hata moja mmefanikiwa? Sasa nini kipya zaidi ya posho kwa Wajumbe?
Tanzania inaamini katika
1. Hekima
2. Umoja
3. Amani

Sasa comment yako hii imeangukia kwenye kipi?
 
Upendo wa kweli ni kusikilizana na kuzungumza
c523ee34-f27f-41c9-9db4-9f7a46969f44.jpg
 
Historia ya kidemokrasia Tanzania
Kuanzia katikati ya miaka ya 1980, chini ya utawala wa Rais Ali Hassan Mwinyi, Tanzania ilifanya mageuzi kadhaa ya kisiasa na kiuchumi.
Mnamo Januari na Februari 1992, serikali iliamua kupitisha demokrasia ya vyama vingi.
Hapa 1992, Mabadiliko ya sheria na katiba yalipelekea kusajiliwa kwa vyama 11 vya siasa.
Kurejelea(referencing) historia ni muhimu sana katika Jamii, hii inasaidia Maridhiano, ustahimilivu, mabadiliko na Ujenzi kwa upya.

SHIRIKI KATIKA MKUTANO MAALUM WA BARAZA LA VYAMA VYA SIASA


Kwa Lengo la kujadili Miswaada ya Sheria za Uchaguzi na Sheria za Vyama vya Siasa iliyosomwa kwa mara ya kwanza Bungeni Novemba 10, 2023
🗓 Mkutano huu utafanyika Tarehe 3 na 4 Januari, 2024
📍Ukumbi wa Julius Nyerere International Convention Centre - Dar es salaam
 
Wazee wa wale ambao wako tayari kuanzisha chama kipya Cha upinzani,usajili wa mda mfupi ni 25,000 tsh na usajili wa kudumu ni 50000, baada ya kupata wafuasi 200 katika mikoa 10 ya Zanzibar na Tanzania bara,
Nipo mbioni kuanzisha chama changu Cha upinzani, mana Hivi vilivyopo sina Iman navyo,
 
Wazee wa wale ambao wako tayari kuanzisha chama kipya Cha upinzani,usajili wa mda mfupi ni 25,000 tsh na usajili wa kudumu ni 50000, baada ya kupata wafuasi 200 katika mikoa 10 ya Zanzibar na Tanzania bara,
Nipo mbioni kuanzisha chama changu Cha upinzani, mana Hivi vilivyopo sina Iman navyo,

..anzisha chama kipya kwasababu huna imani na chama tawala.

..ukianzisha chama kwasababu huna imani na vyama vya upinzani utaelekeza nguvu zako mahali pasipo sahihi.
 
Back
Top Bottom