Return2roots
JF-Expert Member
- Jun 12, 2015
- 874
- 438
Kamarade, na dadaangu ktk jamvi la JF...kuna ugaidi! Na unatusulubu...lkn ukweli mbaya, na usiofurahisha ni namna wanasiasa walivyoanza cheza siasa hata ktk hili... "mmoja, mwenye asili ya kutokea pembe ya afrika, anadai hata yeye, na wenziwe, kina msukuma, na malima, "walitekwa!"....hatukubali taarifa ya kunyanyaswa kwao, kama tusivyokubali kunyanyaswa mtu mwingine yoyote.....lkn, wakati, tunatafakari masuala ya kutekwa kwa kina Roma, na Ben saa8, ....kutuletea "maugomvi, na kupishana, na kuthibitiana kichama" na kutaka kupata sympathy ile ile wanayopatata kina Ben saa8, inakuwa ni kuleta uchuro ktk maana nzima na tafsiri ya "kweli" ya kutekwa....tusipotafakari, wanasiasa siku ingine watakapozidiwa na "mambo ya ndani, ktk vibanda hasara", watatujia na kutueleza kuwa ,vibanda hasara hivyo ni njama za mahasimu wao, na vilitumika kuwateka....Kinachoendelea sasa hivi Tanzania ni ugaidi (terrorism).
Lengo la ugaidi ni kuwatia watu hofu na kufikisha ujumbe kwa wengi kwa njia ya hofu.
Matukio yanayoongelewa sana kwenye vyombo vya habari na mitandao yote ya kijamii mpaka nchi za nje kwa sasa ni hayo, kuanzia watu kutekwa, kutolewa bastola hadharani, mauaji ya Kusini huko, watu kukutwa kwenye viroba, kupotea kwa watu na mengi mengineyo, yote yanaashiria ugaidi.
Magaidi hujitokeza na kusema sisi ndiyo tuliyoyafanya hayo ili waogopwe au matakwa yao yatimizwe au hukaa kimya na kuwachochea kivingine kwa lengo hilo hilo.
Matukio ya ugaidi yanapotokea pia hujitokeza wengine ambao hutumia fursa hiyo kufikisha ujumbe wao kwa njia tofauti.
Kwa yanayotokea Tanzania, ukweli ni kuwa, kuna wanaofanya huo ugaidi wa kutisha na kuna wanaotumia huo gaidi kama ni fursa kwao kufikisha ujumbe wao ama kwa kuongezea ugaidi mwingine au kwa kuendeleza hofu kwenye jamii na vyombo husika.
Watanzania tunachotakiwa kufanya ni kukaa kimya na kufunga hii mijadala yote na kuwacha kuripoti matukio yote ya kigaidi ili kushindana na ugaidi.
Gaidi kama matukio yake hayaongelewi kazi yake inakuwa haijafanikiwa.
Au leta mawazo yako ni njia gani zitumike kutatuwa hili tatizo "linalotukabili".
Kwa muono wangu, kila tunapoyaongea na kuyasambaza ndiyo furaha ya magaidi na ndiyo lengo lao, wengi wajawe na hofu.
Kwanini? Mie sijuwi.
...tuwe makini na wanasiasa wenye kufanya siasa kimchezomchezo, na wenye kutumia masahibu ya "mitaani", kama kifaa ktk makabiliano yao "mchezoni"...