Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Kuna wengine huko wanatamani hata wapate pumba waipike lkn hawapati wamebaki kula viwavijeshi! acha watu wale dona wapate nguvu haijalishi biashara yako ya sembe inadorora tunataka vyakula vyenye nguvu.
 

kila kitu sumu dona inamfanya babu asimamie vizuri mechi
 

sasa tule nini kila kitu sumu too much is harmful soda sumu mbona zinatengenezwa ukiishi ivo kila kitu utaacha kula TUSIKIMBIE KULA TOENI SULUHISHO
kwani kansa haidhuiriki ipo kwenye dona tu
kuzitoa radicals au sumu zozote mwilini unazimaliza kwa vyakula ivo ivo you are for what you eat
matunda hayawezi kuweni makini na data zenu
 
Mkuu tungejaribu kupanua mawazo kidogo. Sidhani kama wanasema kula dona au unga wa mihogo utapata hayo madhara! Ni kula dona ambayo inatokana na mahindi ambayo hayajahifadhiwa vizuri. Na ule kwa kipindi kirefu. Na mihogo ni hivyo hivyo. Sasa nenda mbali zaidi uone hao wanaotumia unga wa mihogo huwa wanahifadhi namna gani? Mimi najua kuna njia za jadi za kukausha vitu kama mihogo ambazo ni nzuri sana kiasi ambacho fungus hawawezi kusogea. Halafu angalia upande wa pili wa shilingi: Je imeshafanyika research kujua kama kuna madhara au ongezeko la kansa kwa hilo eneo? Je diagnosis za hospital zetu ni nzuri kiasi ambacho tunajua kila ugonjwa unaosababisha kifo? Je ni wote wanakwenda hospital wanapougua? Mkuu hivi vitu bila research nadhani sio rahisi kujua! Unajua kuna mtu anaweza kuzaliwa mpaka akafikisha miaka 70 bila kuwa na mtu wa karibu ambaye amepata kansa kwa sababu ya sigara? Je inaondoa ukweli kuwa tunaweza kuwa na ndugu wengi wanavuta sigara na sigara zinachochea aina fulani za kansa?
 


Wewe utakuwa afisa habari wa Azam
 
Dunia ya leo kila kitu sumu hasa vile vitamu tukianzia na mke wa mtu na kuendelea dawa ni kula hakuna ambae ataishi milele aaaghhhrr sijakuja kulinda dunia mimi.
 
Hakika hawajakaza kula dona wala mihogo! Wametoa tu tahadhari ya kuhifadhi vizuri! Hata soda watu bado wanakunywa! Ila kuna tahadhari ya kutozidisha, Kama ilivyo pombe!
 
Daaah!!
Natafakari wale wazazi wa hapo nyuma waliokula na wanaendelea Kula Dona mpaka leo sijaona wakipata hayo madhara, ukizingatia wao ndio walikuwa Na wanatumia hayo madawa kuhifadhia mahindi.

Mtoa mada biashara yenu itakuwa inadoda yawezekana eeh?
 
Hakika hawajakaza kula dona wala mihogo! Wametoa tu tahadhari ya kuhifadhi vizuri! Hata soda watu bado wanakunywa! Ila kuna tahadhari ya kutozidisha, Kama ilivyo pombe!

ndo maneno hayo maana sumu almost vyakula vingi ipo uhifadhi vizuri kivipi akati huo ni unga na shida ipo kwenye kiini kilichosagwa
 
k




kwani kama kwenye dona huyo fungus akiingia kwenye sembe atashindwa kwanza unazijua tabia za fungus na reproduction yake wacha bwana fungus anareproduce asexualy kwa maana hata wakiingia punje



kuhusu dona mii naquote alichoandika mtoa mada sababu amecompare dona na sembe ,mimi nistick nachojua kansa nyingi tumeanza kuzisikia kutoka katika chi zilizoendelea huku kwetu zimekuja juzijuzi tu na nyingi ninavyojua zinatokaana na mabadiliko katika hali ya maisha kutoka ukale kuja katika usasa ni kama cases za presha na stroke.
 
Kusoma sana kunadhoofisha ufikiri!...miaka yote tunakula dona leo kuibuka kwa mashi e za kukoboa na kusaga dona imekuwa sumu!


Endeleeni kula makapi yenu, mie dona siachi ng'o!
 
Sio kweli

Aflatoxin ni sumu inayotengenezwa na aina ya fangasi wanaitwa Aspergiluss.Sumu hii inakutwa kwenye mahindi ambayo hayajahifadhiwa vizuri.Ukihifadhi vizuri mahindi yako wala hautapata matatizo
 
Mimi nadhani sio kweli kuwa ''kansa nyingi huku kwetu zimekuja juzi juzi tu''. Zilikuwepo ila kwa sababu ya uhaba wa hospital na utibabu wenye utaalam mdogo basi watu wengi walifariki bila watu kujua ni nini kimewaua. Mawazo yako ni kama ya waafrika wengi wanaosema eti wazungu wengi wana macho mabovu kwa sababu ya kuvaa miwani. Kumbe ukweli ni kuwa huku kwetu hakuna madaktari wa macho wengi na watu wengi wanazeeka bila kupata huduma ya macho.
 
Tumia dona ambayo mahindi yake hayakutiwa dawa. Unaweza kuagiza mahindi hata kijijini kwenu ukasaga mwenyewe kuliko kununua katka masoko.
Kama ni mbolea hata vijijini wanatumia sana kiongozi.Bado nasisitiza tunaomba ushauri tule nini?
 
Dona limeanza kuliwa kitambo saaana na mimi bado nalishindilia.
 

Mkuu mwenye so hiyo sumu iko ndani ya kiini cha punje. Imefikaje ndani ya kiini na isiwepo kwenye punje yote? Sababu umesema inatokana na dawa za kuhifadhia!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…