Deogratius n
JF-Expert Member
- Jan 10, 2015
- 1,193
- 254
Nimekula Dona Toka 1936 Mpaka Leo Nina Miaka 80 Na Bado Naonekana Kijana
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Unauhakika kwamba hawajakujuza humu ndaniunless uniambie kuna mahindi ya GMO labda unayoyajua wewe yenye viatilifu vya aina hiyo
kitu ambacho sijasikia Labda ndugu zetu wa TFDA NA Kilimo mtujuze.
sipendagi kweli habari ambazo hazina ukweli ama zinazofikisha ujumbe ndivyo sivyo......Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.
Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Nashukuru mkuu umeleta huu uzi..Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.
Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Huo ndio ukweli kabisa. Bakresa kaona soko linazidi kudidimia na sasa hiyo ndiyo mbinu. Serikali lazima izime mbinu hizi chafu. Watoto wetu kula sembe ni kuendeleza kwashakor tu.Umetumwa na Bakhresa wewe.
Tumia dona ambayo mahindi yake hayakutiwa dawa. Unaweza kuagiza mahindi hata kijijini kwenu ukasaga mwenyewe kuliko kununua katka masoko.Toa ushauri sasa tule nini,mawe au miti?
Hii tetesi ina ukweli fulani
Hii sumu hutokezwa na aina ya fungus aitwaye Aspergillus flavus. Huyu fungus hushambulia nafaka kama karanga na wakati mwingine mahindi na nafaka zingine. Aflatoxin ni sumu, hata ukichemsha hii sumu haipungui makali na matokeo yake ni mabaya sana kama alivyogusia mleta mada. Kiukweli hili ni janga la karibuni sana kufahamika na huenda ikawa ndo "ukimwi" tuliohubiriwa kwa muda mrefu.
So far, hakuna antidot ya aflatoxin. Utafiti unaendelea kujua ni mlundikano wa sumu kiasi gani ya aflatoxin inaweza kusababisha madhara.
Wanaobeza hoja nadhani hawako sahihi.. wafuatilie na wachukuwe hatua za kujilinda dhidi ya hili janga
Mkuu laiti watu wengi wangekuwa na busara kama zako. Mimi bado nasisitiza kuwa elimu yetu ni majanga. Hii sumu iko dhahiri lakini kuna watu wanauliza mbona fulani kala dona mpaka kazeeka! Really? Mtu anayewaza namna hii elimu ilimsaidia? Wao wanataka kuona yale madhara ya tit for tat! Hawajui mambo ya probability...Nashukuru mkuu umeleta huu uzi..
Nimesoma baadhi ya comments na nimesikitika watu wengi hawajui kuhusu mycotoxins
1. Aflatoxin ni moja kati ya sumu nyingi sana zinazotokewa na fungus ambazo kwa ujumla huitwa mycotoxins.
2. Mojawapo ya nafaka ambapo aflatoxin huwepo sana ni mahindi hasa yanayolimwa maeneo ya kitropiki kama Tz
3. Tafiti kama 5 zimefanyika kwenye mahindi na kugundulika asilimia 30-50 ya mahindi yasiyokobolewa yameathirika na uwepo wa aflatoxin zaidi ya kiwango cha chini kinachoruhusiwa kitaifa na kimataifa
4. Kwa Tz kiwango cha chini kinachoruhusiwa ni 5 ppb (0.005 ppm) ingawa kwa mataifa mengi ni 10 ppb
5. Madhara yatokanayo na ulaji wa vyakula vyenye aflatoxin na kansa ya ini, ugonjwa wa figo, upungufu wa nguvu za kinga mwilini, matatizo kwq vichanga, kudumaa nk. (Kwa nchi nyingi ambazo chakula kina aflatoxin sana ikiwemo Tanzania watoto wengi wamedumaa)
6. Zaidi ya aflatoxin pia sumu nyingine za fungus kama fuminisins zipo sana kwenye mahindi
7. Hata uchemshe mahindi namna gani, aflatoxin haiwi deactivated.
8. Watu wanadhani mahindi yaliyooza au fungus zinaonekana kwa macho ndio yenye aflatoxin lakini ukweli ni kuwa hata mahindi masafi kabisa yanaweza kuwa na hiyo sumu
9. Aflatoxin na sumu nyingine za fungus hazina harufu, ladha wala rangi, hivyo sio rahisi kitambua chakula kilichaathirika
10. Mazao mengine ambayo yana aflatoxin kwa wingi ni karanga (zaidi hata ya mahindi), na mihogo ya kukausha.
11. Pamoja na kwamba madhara yanaweza kumpata yeyote lakini huwa na athari zaidi kwa watoto. Hivyo inashauriwa hata kama wewe unashindwa kuepuka basi walinde watoto wako. Usiwape vyakula vyenyr mahindi hayajakobolewa wala karanga