Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Daaaah maisha ni magumu kama ni hivyo, ukichukua demu utaambiwa ukimwi, ukivuta sigara utaambiwa cancer, ukinywa konyagi utaambiwa livercirhosis, ukila kiti moto utaambiwa kisukali , shenzi kabisa sasa nimeamua sifuati tena maushauri yenu
Vijijini ndo vyakula vyao na wamevitumia enzi na enzi kama ni kweli wengi wangekuwa wameshakufa
Tatizo ni hiyo sumu iitwayo Aflatoxin itolewayo na hao fungus huwepo kwenye mahindi hata hao fungi akifaa.Tufwile nyambala Kyala nnunu gwe! Hatufi kirahisi rahisi hivyo wewe njoo na style nyingine boss
Kumbe hata fungus akitokoshwa Kwenye uji hafi anazidi kuwa strong ahahahahahhaha Asante Kwa hii elimu ya fungus hafi Kwenye uji
Du aiseeeee....ndio mbinu mpya ya ccm hiyo
Ni kweli mkuu,maana kijijini mihogo huvundikwa hadi ivunde na kuota fungus juu(ule utando wa juu) ndipo huwa tayari kupondwa-pondwa kwaajiri ya kutayarisha Unga!Kwani kijijini kwenu hajawahi kufa watu kwa saratani ya ini!?
Ni tetesi kwa sababu hakuna takwimu zenye kuhusisha ulaji wa ugali wa dona na kansa.
Bado ukweli ni kwamba kiini cha mahindi hutunza "fungus" na ndiyo mama wa "aflatoxin".
Kwa maeneo ya joto na unyevunyevu (kama huku TZ) kansa ni ugonjwa mkubwa kwa kula aina hiyo ya vyakula vinavyozalisha "fungus" km dona, unga wa mhogo unaovundikwa hadi kuwa mweusi nk.
...
Ukifuata kila linalosemwa utashindwa kuishi. Eat what you like, badilisha badilisha, fanya mazoezi, usinenepeane, kunywa pombe kwa wastani na usivute sigara. Maisha yatakwenda tu na siku yako ikifika unakwenda.
Dona mbaya miaka na miaka Wasukuma kule tunakula dona na hakukuwa na kansa wala huu upuuzi mwingine. Yamekuja haya mavyakula ya viwandani ndiyo kansa imeripuka kila kona barani Afrika kisa tunaiga wazungu. Aaaaargh!
Ukifuata kila linalosemwa utashindwa kuishi. Eat what you like, badilisha badilisha, fanya mazoezi, usinenepeane, kunywa pombe kwa wastani na usivute sigara. Maisha yatakwenda tu na siku yako ikifika unakwenda.
Dona mbaya miaka na miaka Wasukuma kule tunakula dona na hakukuwa na kansa wala huu upuuzi mwingine. Yamekuja haya mavyakula ya viwandani ndiyo kansa imeripuka kila kona barani Afrika kisa tunaiga wazungu. Aaaaargh!
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mambo haya na nina kabrasha zima limejaa research papers kuhusu ishu hii. Tatizo langu na wanasayansi hawa (wengi wao kutoka Ulaya) ni kutoa tafiti zinazokinzana halafu hawasemi watu wafanyeje. Leo utasoma kuhusu uzuri wa kunywa kahawa na kesho unasoma utafiti mwingine unasema kahawa ina madhara kibao. Juzi juzi hapa kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu utafiti mmoja uliosema kuwa "kuzamia chumvini" kunasaidia kupunguza baadhi ya kansa hasa za koo. Hapo hapo utafiti mwingine ukasema kuzamia chumvini ni chanzo kikubwa cha kansa za kinywa. Sasa hapo wanataka watu wafanyeje?Sasa hivi mnaona Kuna milipuko ya kansa kwasababu mnaenda hospitali.... Zamani mlikuwa hamuendi hospitali mnaishia kusema wagonjwa wamelogwa.
Na pia hospitali zenyewe zilikuwa chache, vifaa vya uchunguzi vilikuwa hamna nk.
Mimi ni mfuatiliaji mzuri sana wa mambo haya na nina kabrasha zima limejaa research papers kuhusu ishu hii. Tatizo langu na wanasayansi hawa (wengi wao kutoka Ulaya) ni kutoa tafiti zinazokinzana halafu hawasemi watu wafanyeje. Leo utasoma kuhusu uzuri wa kunywa kahawa na kesho unasoma utafiti mwingine unasema kahawa ina madhara kibao. Juzi juzi hapa kulikuwa na mjadala mkubwa kuhusu utafiti mmoja uliosema kuwa "kuzamia chumvini" kunasaidia kupunguza baadhi ya kansa hasa za koo. Hapo hapo utafiti mwingine ukasema kuzamia chumvini ni chanzo kikubwa cha kansa za kinywa. Sasa hapo wanataka watu wafanyeje?
Mwaka juzi shirika la afya duniani (WHO) lilitoa ripoti ya kutisha kuhusu ueneaji wa kansa barani Afrika katika miaka ya karibuni. Sababu kubwa iliyotajwa ni kubadilika kwa mifumo ya maisha ikiwemo hasa utumiaji wa vyakula vilivyosindikwa viwandani na uhamiaji mijini ambako watu hudeka na hatimaye kunenepeana bila kufanya mazoezi wala shughuli za kuutaabisha mwili. Mengine ni unywaji wa pombe kali (viroba?) kuongezeka na uvutaji wa sigara.
Kama mdau mmoja alivyosema hapo juu mimi nadhani tatizo linaweza kuwa kwenye madawa yanayotumiwa kutunzia nafaka hizi ili zisiharibike. Hakuna anayejua viwango sahihi vinavyopaswa kutumiwa na unakuta mahindi yanachukuliwa kutoka ghalani yanapepetwa tu halafu yanakwenda kusagwa. Zamani watu walikuwa wanatumia majivu tu basi lakini sasa mambo yamebadilika.
Ushauri wangu ni ule ule. Kula ukipendacho lakini in moderation, badilisha badilisha, fanya mazoezi, epuka ulevi na sigara; na tumia common sense tu and you will be OK. Leo utakula hichi na kesho wataibuka tena na kusema nacho kinasababisha kansa.
Otherwise nakubaliana na point yako.
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.
Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA
Kuna vituvingine vinahitaji akili iliyo lala ili uvielewee,tunaotoka kanda ya kati tunathamini dona kwea unyenyekevu usiohojika.naanzaje kuiletea madharau dona[emoji15]Wazee wetu zamani kulikuwa hakuna unga wa sembe walikuwa wanatwanga katika kinu au kusaga kwa mawe kisha wanapiga msosi. Tena walikuwa na afya nzuri kulinganisha na sisi wa kizazi cha digitali.
Walikuwa hawana maradhi kama ilivyo sasa tunaokula unga wa sembe.
Hivyo bado nina imani kubwa na unga wa dona katika afya ya binadamu.
You proved my point sir. That's what I was trying to say. Ni ku-adapt kulingana na mazingira mahali ulipo na siyo kufuata kila wanalosema hawa watafiti ambao mara nyingine tafiti zao zinakuwa contradictory!Sayansi, Research na ugunduzi ni dynamic haipo static.... Hivyo usitegemee ukipata jibu la jambo mara moja basi ndiyo hivyo hivyo
hiyo *aflatoxin* inaingia kwenye kiini cha hindi muda gani... wa kupandaaaaa, kunyunyuziaaaa ama muda wa kuhifadhi mahindi....Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.
Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).
Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.
TAFAKARI CHUKUA HATUA