Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Ugali unaopikwa kwa Unga wa mahindi (dona) hatari kwa afya ya binadamu

Daah!...kama na dona sumu basi hakuna chakula tena

Ila hata kama kuna huyo "aflatoxin" kwenye dona bado virutubisho vya dona vinaweza kua ni vingi kuliko hiyo sumu

Na kabla ya kusonga ugali ule uji hua unachemka kwa centigrade nyingi sana hiyo sumu bado inabaki salama?
Mkuu Sumu Ikipikwa Haiondoi Sumu Iliyopo, Sema Kwa Dunia Ya Leo Mi Naona Kila Kitu Sumu Sa Sijui Tufanyeje, Coz Mpaka Mboga Za Majani Huwa Zinamwagiwa Dawa Sasa Hapa Tunaenda Wapi Ndugu.

Aaah Ebu Tule Bana Maana Hakuna Namna.
 
Najua wewe si mwehu,wala Juha,Huenda labda ulichanganyiwa kiroba udanganye watu hapa,Hivi kwa sisi hapa namanyere tunaolima mahindi wenyewe hiyo sumu inatokea wapi,na je vipi kwa wanaoosha mahindi kabla ya kukoboa?Na utafiti wako hmefanyia wapi?
Mtoa Uzi Amesema Sumu Hukaa Ndani Ya Kiini Cha Mahindi So Ukiosha Inatoka Vipi Hapo Mkuu?.

Hata Huko Namanyele Wakilima Wanauza Mahindi Kwa Wafanyabiashara Na Baada Ya Hapo Wafanyabiashara Huyahifadhi Ghalani Kwa Dawa.

Ndugu Tumuelewe Mtoa Uzi Japo Pengine Nia Yake Ni Kuuza Ile Sembe Ya Shop Kwake Hahahahahahha
 
Huyu atakuwa ni free mason.......maana hawa free mason......kila uchao wanatafuta namna ya kutumaliza ili tuishe kwa kutushawishi kufanya mambo ya kipuuzi kama haya........sasa wewe unaona ni bora tule unge mweupe ili tupate madhara ya kizembe au tukomae na dona......kwani wewe unadhani ini linafanya kazi gani tumboni...........si kupambana na sumu?!
 
Dona nimeanza kula tangu nikiwa mdogo, sasa hivi naelekea uzeeni sijasikia hata tumbo likiunguruma,sana sana likiunguruma nataka kujamba,kwa hiyo km umetumwa kudanganya watu ili wewe uuze sembe shindwa kwa jina la bwana wa majeshi
 
Tusitishane ili mfanye biashara zenu. Dona kwenda mbele.
 
Tusitishane ili mfanye biashara zenu. Dona kwenda mbele.
Pamoja na ushauri unaotolewa humu kuhusu kuandaa mahindi yako ili upate dona iliyo salama kwa matumizi ya binadamu bado hujaelewa, du!
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA
Dona ya kazi gani wakati siku hizi kuna virutubisho vinaongezwa kwenye sembe?? DONA ni hatari kwani mahindi yanapigwa dawa sana kukomesha vijidudu.
 
Watu wengi kwa sasa wamependelea kula ugali uliopikwa kwa unga wa mahindi usiokobilewa, maarufu 'dona'. Pamoja na kwamba mahindi uhifadhiwa kwa madawa ili yasiharibike (athari kwa fedha) kuna tatizo lingine kwa afya zetu yasemekana.

Tahadhali na unga wa dona, ni hatari kwa afya kwa sababu ya sumu inayoitwa 'aflatoxin" ambayo huwa ndani ya kiini cha mbegu ya mhindi. Ukikobolewa kiini uondolewa na kubaki unga mweupe (sembe).

Wengi sasa hawependi kula ugali wa sembe kwa sababu ya kukosa protini (iliyomo kwenye kiini). Lakini hasara ya kukosa hiyo protein ni ndogo sana kulinganisha na madhara ya "aflatoxin" itakayosababisha "cancer" mwilini mwa binadamu.

TAFAKARI CHUKUA HATUA

Naona hamna ha kuandika sasa yaani full kuchanganyikiwa. Sijui mmesomea wapi ama kweli google inatuaharibia wataalamu wetu. haya dona sumu tunasubiri tuambiwe mate nayo sumu makubwa haya....
 
Ndg nakuomba tusiseme juu ya chakula mana kuna vitu vingi n sum ktk mwil mfano, Chlorine /fluoride inasababisha kansa mwilin kulingana na kinga ya mtumiaji, lkn swali n hili Nan? Ambaye hatumii hivi vitu?
 
kama nilijua vile dona inatatizo maana nikila zile pumba hunisumbua sana tumbo sijui kwanini lakini nikila sembe najisikia vizuri salama salimini nina miaka zaidi ya 20 siujui ugali wa dona
 
kama nilijua vile dona inatatizo maana nikila zile pumba hunisumbua sana tumbo sijui kwanini lakini nikila sembe najisikia vizuri salama salimini nina miaka zaidi ya 20 siujui ugali wa dona
Dona haina tatizo ww ndo unatatizo, panya hawal mahindi yaliyokobolewa iweje sisi tulioambiwa kuwatawala tule yaliyokobolewa? Sasa nakwambia fanya mpango uaze kula dona kwan wanaokula sembe wanajiua wenyewe taratibu lkn kwa uhakika!
 
Back
Top Bottom