Uganda imekubali kuwapa raia wa Afghanistani hifadhi ya ukimbizi

Uganda imekubali kuwapa raia wa Afghanistani hifadhi ya ukimbizi

Basi uganda wako na bahati sana kanda yetu, maana hata israel ya leo kama wasingekataa ungekuta wako uganda kwa sasa.
Hata matukio mengi yamewahi kutokea uwanja wa ndege wa entebe, na hata la sasa litawainua mno!

Ajabu kwangu hao waasi hawaoni aibu kukombiwa na wananchi wao?

Lakini pia ni jinsi gani africa isivyo na thamani mbele ya wenzetu, tunafanywa kama jalala!
Mbona walioondoka ni wachache walobaki ni wengi?
 

Wakimbizi wa Afghanistan

AFPCopyright: AFP
Uganda imesema kuwa itawachukua wakimbizi 2000 wa Afghanistan wanaokimbia mzozo nchini mwao – kufuatia ombi la Marekani.
Hii inafuatia hatua ya wanamgambo wa Taliban kuchukua uongozi wa nchini hiyo wikendi iliyopita baada ya serikali iliyokuwa madarakani kuanguka.

Uganda imepongezwa kimataifa kutokana na sera yake ya kuwakaribisha wakimbizi.
Kundi la kwanza la karibu Waafghanistan 500 linatarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Entebbe saa chache zijazo.

Waziri wa Wakimbizi wa Esther Anyakun ameiambia BBC kwamba Rais Museveni amekubali kuwachukua jumla ya wakimbizi 2000 raia wa Afghanistan – kufuatia ombi la Marekani.

Aliongeza kuwa watakapofika watafanyiwa vipimo vya corona na kuwekwa karantini. Vifaa na gharama zote zitashughulikiwa na Serikali ya Marekani.

Uganda itakuwa nchi ya kwanza ya Afrika kuwapokea watu wanaotoroka ghasia nchini Afghanistan.

Uganda ambayo imekuwa na historia ya muda mrefu ya kuwakaribisha wakimbizi - kwa sasa ni nyumbani kwa zaidi ya watu milioni moja waliokimbia mzozo na majanga.
Wakimbizi nchi humo wanaoishi katika makazi au vijijini na wenyeji. Baadhi yao wamepewa kipande cha ardhi na kuruhusiwa kufnaya kazi
 
Wachangiaji wanadai Uganda ni hatua ya kwanza, then watapelekwa USA baada ya muda. Mimi swali langu, kwani USA hana kambi za kuwahost kama wakimbizi mpaka ije iwe Uganda?
 
Duniani Raha Sana
Sasa Hivi Wataanza Kula Ugali Na Matoke
Toka Afghanistan Mpaka Uganda 😂😃🤣
 
Yaani wamewabeba wale raia Afghanistan kwa mbwembwe utafkiri wanawapeleka Marekani au Canada mwisho wa siku kwa kuwakomoa wamewamwaga Entebbe na Museveni kakubali kuwapokea aise nahisi hao raia wanatamani hata wangepelekwa Jalalabad Pakistan au warudi Kandahar yaani wanajuta kudandia pipa.
bro Uganda ni kuzur mara kumi ya huko unakotaja
 
Well the America we as Great today was build by immigrants.., kwahio kama hao wakimbizi wakiwa assimilated wakatumia knowledge zao vizuri huenda wakasaidia kujenga haya makazi yao mapya

After all maybe its about time ukizingatia dhambi kubwa waliyofanya ya kuwakimbiza wahindi wote....
 
Lazima wafanyiwe assessment unaweza Kuta Taliban ndio walidandia ndege Ili waje kufanya ugaidi Us ,vetting lazima

Hili neno ugaidi sijalisikia kwa mayahudi/mabeberu dhidi ya mashambulizi ya kumng'oa saddam na yale ya Gadafi n.k kote duniani. Icpokuwa lina2mika kwa waisilamu tu. Why?
 
Hao jamaa wenyewe wana matumaini ya kwenda Canada na USA halafu wanajikuta Entebe kwa Mtaliban mweusi M7.

Tutarajie kuona makumi ya wahamiaji haramu waarabu wakipitishwa kwenye malori wakienda SA.
 
Sipati picha Mange anajisikiaje huko Instagram 😂😂😂😂😂😂 ,hata hivyo sio mbaya kikubwa bado wanaendelea kuishi
Wale waliodandia karibia wote wamekufa kijinga, nilikuwa naangalia clip moja wakati huu kuna maiti imebanwa na Landing gear inamevunjwa vunjwa na upepo wa huko 39000ft
 
Wale waliodandia karibia wote wamekufa kijinga, nilikuwa naangalia clip moja wakati huu kuna maiti imebanwa na Landing gear inamevunjwa vunjwa na upepo wa huko 39000ft
Itume hapa tuiangalie
 
Basi uganda wako na bahati sana kanda yetu, maana hata israel ya leo kama wasingekataa ungekuta wako uganda kwa sasa.
Hata matukio mengi yamewahi kutokea uwanja wa ndege wa entebe, na hata la sasa litawainua mno!

Ajabu kwangu hao waasi hawaoni aibu kukombiwa na wananchi wao?

Lakini pia ni jinsi gani africa isivyo na thamani mbele ya wenzetu, tunafanywa kama jalala!
if u have studied a lot about Refugees and Asylum seekers u couldn't say that...
 
Back
Top Bottom