Uganda imekubali kuwapa raia wa Afghanistani hifadhi ya ukimbizi

Uganda imekubali kuwapa raia wa Afghanistani hifadhi ya ukimbizi

mimi nashindwa kuelewa kwann hawa waikimbie nchi yao wakati asilimia kubwa ya raia hawajaikimbia nchi yao
Hao wanatofautiana itikadi na wa Taleban yani kama ilivyo waislamu wa “Sunni” na “Shia” so moto lazma uwake na wa Taleban wabababe kichizi
 
Naamini hapa kuna kitu kilikuwa kinaendelea. Maana jana Biden amefanya presa conference na alisema kwamba Marekani ilitoa mafunzo yote ya kijeshi kwa wanajeshi wa jeshi la Afghanistan ikiwepo hadi jeshi la anga. Tafsiri yake ni kuwa serikiali na jeshi walikuwa wana silaha nzito na za kisasa ukilinganisha na Taliban.

Akasema Marekani haiwezi kuendelea kupigana vita ya kufa na kupona ilhali wanajeshi wa nchi husika hawako tayari kupigania nchi yao.

Ila pia inasemekanika kuwa pamekuwa na rushwa sana ndani ya serikali na kupelekea polisi na wanajeshi kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu. Hii imepelekea hawa watu kuona hamna faida ya kundelea kujiweka rehani maisha yao ilhali hamna wanachopata.
ina maana US imeshindwa kuwalipa wanajeshi wa Afghan?
 
Uganda wanapaoneaaa...

Ma Zionist(Wana israeli) mwaka 1903 walipokosa nchi ya kujihifadhi Walikabidhiwa Uganda(eneo la kenya ya leo) na Muingereza kabla ya kukataa kusema sisi tunatokea Palestina
Leo hii wa Afrighanistan Wamepelekwa huko huko....
Pia Idd Amin aliwahi teka ndege ya Israel
 
[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28]baada ya kusikia i habari nili jikuta tu nacheka kama mazuri
Mimi niliona picha ya trafiki mtalabani nikapata hamasa ya kwenda kutalii. Kumbe utalii umesogea hapa hapa kwetu?? Ile jamii ile....Shekhe Ponda aende haraka kuwasaidia wale jamaa wajitambue 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂 😂
 
Ni muhimu sana nyie pambaneni na Tozo sie wacha tukale kuku wa UNHCR hapo wakati tukisubiria pipa la kwenda USA

We huko utaonekana tuu umejiingiza muhimu nenda kigoma Kuna kambi huko za watu ambao huchukuliwa kila muda kwenda USA Kuna watu wawili waliendaga huko mpaka Sasa sijawaona bongo na Ni muda huenda Mambo yalitik
 
😂😂😂😂😂😂 kumbe kigoma kunaingilika
 
Yaani wamewabeba wale raia Afghanistan kwa mbwembwe utafkiri wanawapeleka Marekani au Canada mwisho wa siku kwa kuwakomoa wamewamwaga Entebbe na Museveni kakubali kuwapokea aise nahisi hao raia wanatamani hata wangepelekwa Jalalabad Pakistan au warudi Kandahar yaani wanajuta kudandia pipa.
Lile jibu alilowapa Biden kuhusu kupeleka wanajeshi ilitosha kabisa kujua hawa wamerekani ni waswahili,kwa nini waarab wa Taliban hawakujiongeza?😂
 
Yaani wamewabeba wale raia Afghanistan kwa mbwembwe utafkiri wanawapeleka Marekani au Canada mwisho wa siku kwa kuwakomoa wamewamwaga Entebbe na Museveni kakubali kuwapokea aise nahisi hao raia wanatamani hata wangepelekwa Jalalabad Pakistan au warudi Kandahar yaani wanajuta kudandia pipa.
Waletwe huku Mtwara madeiwaka yamejaa,watapalilia mikorosho na kuvuna pia
 
Hapa wilaya ya Hai kuna wasomali walimwaga miaka mingi hiyo Hadi Leo kunaitwa kwa wasomali wamechanganyika na wamaasi na ndio mji umekua balaa uwezi amini
Hai sehemu gani? Wako wengi? Unaposema ''mji umekua balaa'' una maana gani?
 
Kuna ndege ya Ufaransa/Israel ilitekwa magaidi wakaelekeza ikatue entebe

Bado sijui inshu ya hifadhi kwa Israel sijui wapalestina bado location n entebe

Leo marekani na wa Afghanistan n entebe.

Entebe Kuna nini kipo easy kuland na kuwa secured kihivyo ilihali Tanzania inaonekana na kujulikana haina Mambo mengi kuliko Uganda ebu wajuz wa Mambo njoon mnitoe tongotongo
 
ina maana US imeshindwa kuwalipa wanajeshi wa Afghan?
Haina maana kwamba USA ndio walikuwa responsible kwa ajili ya kulipa wanajeshi wa Afganstan. Wale walikuwa ni waajiriwa na serikali/nchi ndiyo yenye jukumu la kufanya hivyo.

Marekani walikuwa wanatoa mafunzo na kuwajengea uwezo. Ila sasa corruption ndani ya serikali naamini imeleta watu kutopata walichokuwa wanapaswa kupata.
 
Yaani wamewabeba wale raia Afghanistan kwa mbwembwe utafkiri wanawapeleka Marekani au Canada mwisho wa siku kwa kuwakomoa wamewamwaga Entebbe na Museveni kakubali kuwapokea aise nahisi hao raia wanatamani hata wangepelekwa Jalalabad Pakistan au warudi Kandahar yaani wanajuta kudandia pipa.
Hivi ninyi mnajua wanachokikimbia kule lakini? Hujasikia kwamba wanadandia ndege iwashushe popote pale nje ya ile nchi? Jamani iweni na utu. Mungu anawapenda. Yamewakuta hawakuomba. Kule hakuna uhai. Anga liko chini ya shetani. Hawatafuti utaliii wale.
 
Marekani wamemwomba raisi Museven awahifadhi kwa muda kabla hawajapelekwa Marekani.

Wapo 2000 na wote inabidi wapimwe COVID-19 wawe documented maana wengine waliingia tu kwenye ndege.

Hivyo wapo kwenye Transit Uganda itapiga mpunga wa kutosha hapo.

Ni shughuli ya miezi mitatu na nchi zingine zitaleta watu hao hapo Uganda.

Marekani itagharamia kila kitu.
Lazima wafanyiwe assessment unaweza Kuta Taliban ndio walidandia ndege Ili waje kufanya ugaidi Us ,vetting lazima
 
Hicho ndicho wanachokiamini kwa sasa. Wanasema wao sio ule utawala wa zamani wa kuwakumbatia magaidi
20210817_194657.jpg
 
Back
Top Bottom