Naamini hapa kuna kitu kilikuwa kinaendelea. Maana jana Biden amefanya presa conference na alisema kwamba Marekani ilitoa mafunzo yote ya kijeshi kwa wanajeshi wa jeshi la Afghanistan ikiwepo hadi jeshi la anga. Tafsiri yake ni kuwa serikiali na jeshi walikuwa wana silaha nzito na za kisasa ukilinganisha na Taliban.
Akasema Marekani haiwezi kuendelea kupigana vita ya kufa na kupona ilhali wanajeshi wa nchi husika hawako tayari kupigania nchi yao.
Ila pia inasemekanika kuwa pamekuwa na rushwa sana ndani ya serikali na kupelekea polisi na wanajeshi kutolipwa stahiki zao kwa muda mrefu. Hii imepelekea hawa watu kuona hamna faida ya kundelea kujiweka rehani maisha yao ilhali hamna wanachopata.