Mkuu usilaumu sana. Hao wote hawatakaa Uganda maishani mwao yote. Watakuwa chini ya UNHCR. Baada ya paper works kukamilika watatawanywa kila mmoja ama familia nchi tofauti tofauti zilizoendelea Australia, Marekani, Canada, Uingereza EU. Na sio wao wataamua ni nchi gani wanaenda.
Process itachukuwa muda kwaanzia miezi 12 hadi miaka 5. Wa Afghanistan wanaofanya kazi UNHCR watakuwwpo hapo kufacilirate kila kitu wakisaidiana na wafanyakazi wengine.
Halafu kwa Museveni ni hela ndefu atapata sana kwa kipindi hicho. Hao Waafghanistan watapokea msaada wa fedha na malazi kwa kipindi chote wakisubiri kuwaresettled hawajapoteza chochote kabisa.
Kumbuka pia majeshi ya Ethiopia jamii ya Tigray walioenda kulinda amani Darfur na kwengineko wote kwa mamia wako Uganda kama wakimbizi wakisubiri ni nchi gani watapelekwa.