Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Great thinker? Unajibu kirahisi kabisa. Duuh Nchi yangu
viwanda ni mipango ya muda mrefu havioti kama uyoga ,hao kila Mo Dewji tunaowategemea kuanzisha viwanda vikubwa wamekuwa hawazalishi bidhaa badala yake wanafanya udalali tu.

Watu wana mambo mengi hatuwezi subiria hivyo viwanda,juzi waziri kaongea na wafanyabiashara wanakubali kwamba hawana uwezo hvyo defficit haiepukiki kwa sasa wacha tu tuagize maana hata usipoagiza watu wanaleta kimagendo .
 
Nani atapoteza muda kumkumbuka dikteta mshamba na muuwaji,,
Utamkumbuka wewe na bibi zako
 
Hivyo viwanda vya sukari hapa nchini vimeshindwa kutupatia unafuu, wanataka 'monopoly' tu na kutuongezea bei kila siku... wacha Uganda na nchi zingine watuletee, kiburi chako kipungue, na labda bei iwe nzuri kwa wananchi tumechoshwa na ubabaishaji.
 


Sukari ilikuwa haitoshi na tunaagiza sasa tulikuwa tunawanyima Uganda halafu tunatoa Brazil!!! lakini viwanda vikishajengwa tutapunguza
 
Katika vile viwanda 3000 na ushee hakuna vya sukari?
Kuna usanii ulikuwa unafanywa na mmoja wa mawaziri wa viwanda, akiita cherehani ni kiwanda, mtambo wa kufyatua tofali ni kiwanda.

Unless tungekuwa na serious people wenye vision na right strategy ya kuanzisha viwanda tungefika kwa haraka sana.
 
Kwenye kuchambua hizo siku 100 sasa,waandishi wetu wa habari. Karibia kila media itakuwa ni kusifia tu kwamba kafanya mazuri,kajitahidi. Kutakuwa hamna hata mmoja kuweka fact ubaoni
Njaa inawatesa wadau hawa remember kila mtu ana hofu na hatima ya maisha yake kwenye kupata mkate wa siku, hivyo hakuna jinsi.

Ndg mwandishi anajua akiponda kesho haitwi kwenye press so atakosa bahasha ya kaki 😁!.


Babati bado kidogo ni mpaka mwezi ujao (June) ndipo tufanye uchambuzi hapa hapa.
 
Ok, uhitaji wetu ni kiasi gani?, Tunapungukiwa na kiasi gani?, Waganda wataingiza kiasi gani?....umakini ukikisekana viwanda vyetu vyaweza kufungwa.
 
Sukari ni kama simenti wenye viwanda wanataka faida ndefu sana ili hela yao irudi kwa haraka nadhani utakumbuka Dangote alivyopigwa vita na mpaka sasa bei ya siment naona ni sawa na viwanda vingine.Kama sukari ya kutosha ipo ni nani ataangaika na sukari toka nje? Ila pamekuwepo na ujanjaujanja wa kurebag sukari, sukari inatengenezwa Brazil lkn mifuko imeandikwa kiwanda cha hapa nchini na wanaofanya hivyo ni wale waliopewa vibali vya kuingiza sukari nchini ili kukidhi mahitaji wakati mwingine unakuta ni haohao wenye viwanda nchini, ila mwenda zake alikuwa amekomesha ujinga huo.
 
Ok, uhitaji wetu ni kiasi gani?, Tunapungukiwa na kiasi gani?, Waganda wataingiza kiasi gani?....umakini ukikisekana viwanda vyetu vyaweza kufungwa.
Sukari ilikuwa inatoka Uganda kwa magendo inauzwa shilingi 2500/= lakini ya Kagera inauzwa 2800/= naamini uhitaji wetu ni mkubwa na uzalishaji ni mdogo sana...bora Waganda watuletee sukari na tupate unafuu wa maisha...pia watu wanapinga importation ya sukari kutoka Uganda lakin wanasahau Uganda pia ananunua vyakula kwa kiwango kikubwa kutoka kwetu...
 
Sukari itatoka Brazil, Asia, itapita Mombasa au Dar es salaam port itaenda Uganda itakunja kona kurudi kuuzwa TZ.
Wawaruhusu na wazanzibar watuuzie sukari maana kiwanda chao kinazalisha Tani elf 3 wanataka kutuuzia Tani elf 18.
Haya ndo yatakayo fanyika kwa sukari toka Uganda. Manji ataagiza sukari toka Brazil ata pack upya pale Uganda na kuleta nchini. Magufuli alikuwa sahihi kukataa kuagiza baadhi ya bidhaa Kama sukari.


Sent from my TECNO RA7 using JamiiForums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…