Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania (Tanganyika) Kenya+Uganda+Rwanda+Burundi bado kupa ardhi inabakia.

Ni habari njema kwa Uganda kuuza sukari Tanzania...
PRIVATE sector ya Tanzania inapenda zaidi uchuuzi kuliko Uzalishaji wa viwandani

Tatizo letu private sector yetu imejaa illiterates darasa la saba na wasiosoma kabisa ndio wanaoendesha private sector

Hata ukute mamilionea ni wachuuzi tu sio producers!!! au wazalishaji wa viwanda!!! Jirani zetu Kenya Private sector wasomi ndio wamejazana kuna viwanda balaa
 
Hao akina Bagamoyo Sugar Ltd kama walianzisha viwanda kisa tu wamehakikishiwa soko lipo kisa sukari ya nje imezuiwa basi wajiandae kisaikolojia.

Juni hii kiwanda kinatarajia kuanza uzalishaji halafu bimkubwa kapiga fungulia mbwa!

BTW:Bakhresa ana uzoefu na ushindani wa kibiashara naamini haitakuwa issue sana kupenya sokoni.
 
Huyu mama ni mkurupukaji sana, sijui hana washauri au hao washauri ndo wanamuingiza chaka, mweeeeeh

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
Tatizo letu ujuaji uliyopitiliza. Ukiambiwa amekurupuka kivipi labda utang’aa macho. Unajua ameruhusu kwa utaratibu upi, nini mahitaji yetu kwa sasa against uzalishaji wetu wa ndani?

Je, tunajitosheleza? Hapo nina uhakika hata underwear umegonga ya nje kama mimi. Tuzuie na hizo tuvae za hapa kwetu kama hatujatembea na kaubaridi maeneo.
 
Lazima tuwe makini sana tusije tukaua kabisa viwanda vyote vya sukari maana sukari ilikuwa inaingizwa kwa kuzingatia mahitaji ya soko...
Ukiruhusu uingizwaji bila kucheki mara mbili ni lazima tuchague kuuwa viwanda vyote!

Wa viwanda vya maziwa wajiandae kuvifunga maana ile ongozeko la ushuru kwenye bidhaa ya maziwa toka nje lazima liondolewe ili maziwa ya kenya yauzwe kwa wingi nchini
 
Acha kabisa wakifungua huo mpaka kwenye kahawa narudi kwenye game maana tulikua tunanunua Burundi 1500 kwa kilo moja Uganda unaenda kupiga 4000 chapchap cash na bila maelezo sasa roadblocks upande wa Bongo ikawa mchawi, tukaanza kupita majini nako wakaingia Bongo ukichek gap ya kilo moja 2500 ni pesa nyingi mno
Wahusika na hizo road block na serikali za mikoa hilo walifanyie kazi haraka.Wakuu wa mikoa la kwao hilo.Biashara za mipakani wakuu wa mikoa inawahusu

Yule mkuu wa mkoa wa Kilmanjaro Mama Mgwira yuko very active akiona wana KIlimanjaro wanaonewa ku export bidhaa kwenda Kenya
 
Kutoka Tanganyika, JMT hadi MIKURUPUKO state.

Tusubirie zile sukari kutoka Brazil zilizoisha muda(expire) wake zikafanyiwa PACKAGE zikiwa na made in UGANDA zikiwa SOKONI. Tanzania kweli failed state, kweli tunashindwa kujenga hata kiwanda cha SUKARI?

Alisema tutamkumbuka kwa kweli tutamkumbuka
 
Ukila lazima uliwe, huwezi kuuza nje tu wewe usinunue hasa bidhaa yenyewe inapokuwa haba kama sukari.
 
Huyu mama ni mkurupukaji sana, sijui hana washauri au hao washauri ndo wanamuingiza chaka, mweeeeeh

Sent from my Infinix X652C using JamiiForums mobile app
We ndio mkurupukaji! Unajua urasimu uliopo Tanzania kwenye viwanda vya sukari vinavyomilikiwa na wanasiasa akiwemo hayati mkapa na genge lake?

Unajua bei ya sukari kutoka Uganda ni 1500?

Unajua pia sukari kutoka Malawi ni 1500?

Unajua maana ya free market economy?

Unajua sisi tunauza sana Uganda kuliko wao wanavyouza huku?

Msijikite kulaumu tu wakati sukari ikipanda vile vile mnalaumu.

Pumbavu kweli ufahamu chochote kuhusu uchumi acha kulaumu Rais kwenye swala la uwekezaji yupo sawa kabisa mwenyewe namuunga mkono.

Tusifanye chuki zetu zitutoe ufahamu Tanzania bado hatujitoshelezi kwa Sukari, cement Na mafuta tuache siasa tufanye biashara.
 
PRIVATE sector ya Tanzania inapenda zaidi uchuuzi kuliko Uzalishaji wa viwandani

Tatizo letu private sector yetu imejaa illiterates darasa la saba na wasiosoma kabisa ndio wanaoendesha private sector

Hata ukute mamilionea ni wachuuzi tu sio producers!!! au wazalishaji wa viwanda!!! Jirani zetu Kenya Private sector wasomi ndio wamejazana kuna viwanda balaa
Mkuu kuongea facts ambazo ni undeniable. Ila pia kuna namna public inaweka mazingira ili private ikue kwa elites kama wewe kuingia.

2012-2013 serikali iliruhusu/ilitoa vibali kwa (wachuuzi) sukari na mchele toka nje kwa wingi kuliko sukari na mchele wa ndani.

Kilichofuatia sukari ya ndani ikadoda na mchele wa ndani ukadoda.

Ili kuwa na stable private sector lazima refa asiwe na interest kwa waachuuzi ambao wanatoa "cut" kwa refa baada ya zoezi lao kufanikiwa.

Ona Kenya wakijua wana interest kutuweka mezani, wamezusha mahindi yetu yana "sumu kuvu". Baada ya madam kukaa nao mezani egenda ya sumu kuvu imeisha. Ukipima kuna namna public sekta imecheza karata muhimu sana ili private sector yao iuze pia hata kama ni kwa ulaghai kama wa kisingizio cha sumu kuvu. Japo simaanishi nasi tucheze mchezo mchafu kama huo
 
Ndo kwaaanza safari imeanza!!!

Tafadhari midomo isiwe wazi!!
 
Hayahaya tuliyakataa, nchi haiwezi kuendelea kwa kuimport tu. Sasa pesa yetu ya madafu inaenda kuzorota zaidi.
Tatizo hamjui kanuni za uchumi. Marehemu alichokuwa anafanya ilikuwa ni primitive economy, na kamwe asingefanikiwa.

Kinachohitajika ni kuuchangamanisha uchumi wetu na uchumi wa Dunia. Watatuuzia sukari, lakini nasi tutawauzia bidhaa nyingine.

Ukifungia bidhaa za wengine, na wewe za kwako zitafungiwa. Wewe unajua hasara waliyoipata wafanyabiashara wa mahindi, mbao, korosho na matunda, kutokana na maamuzi ya hovyo ya marehemu ya kuanzisha chokochoko ambazo hazikuwa na msingi wowote dhidi ya Kenya?
 
Ila huku jforum kunavilaza sana. Sasa mbona miaka yote baadhi ya sukari inaagizwa nje mbona hamkulalamika au ni bora tununue mbali itakuwa na maana kuliko kununua kwa jiran yetu. Tujiulize kwann hatuzalishi sukari ya kutosha hapo ndipo penye kujishangaa
 
Tatizo hamjui kanuni za uchumi. Marehemu alichokuwa anafanya ilikuwa ni primitive economy, na kamwe asingefanikiwa.

Kinachohitajika ni kuuchangamanisha uchumi wetu na uchumi wa Dunia. Watatuuzia sukari, lakini nasi tutawauzia bidhaa nyingine.

Ukifungia bidhaa za wengine, na wewe za kwako zitafungiwa. Wewe unajua hasara waliyoipata wafanyabiashara wa mahindi, mbao, korosho na matunda, kutokana na maamuzi ya hovyo ya marehemu ya kuanzisha chokochoko ambazo hazikuwa na msingi wowote dhidi ya Kenya?
Wewe unaexport bidhaa gani Uganda?
 
Hili Taifa linageuzwa soko badala la kiwanda.

Kila anakoenda Mama badala ya kuwela wawekezaji yeye analeta wachuuzi.
Nitajie viwanda vikubwa vilivyoletwa na Mwendazake,
Licha ya mwendazake kuimba mapambio ya uchumi wa viwanda,badala yake kaua viwanda vingi sana,mfano kiwanda Cha Tumbaku na kiwanda Cha kutengeneza nguo/Cha Mazava vyote vipo mkoa wa morogoro,
Akageuka kuwa mzinduaji wa mashine za kusaga na kukoboa,
 
Back
Top Bottom