Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Uganda: Rais Museveni amshukuru Rais Samia kwa kumruhusu kuuza sukari Tanzania

Sometimes tukubali tu kwamba East Africa ni moja na watu wa East Africa ni watu wale wale tu. Sidhani kama ni vibaya waganda wakiuza sukari yao hapa, kama vile sisi tunavyotaka kuuza bidhaa zetu kwa majirani. Ni kosa kimkakati kuruhusu vimipaka vilivyowekwa na wakoloni vituzuie tusione udugu wa kihistoria baina ya watu wa nchi zetu.

La muhimu ni kuzingatia maslahi ya nchi kwa msingi wa nipe nikupe. Hata JPM ashawahi kuruhusu sukari kutoka Uganda, pengine hakuna kipya hapa.
 
Kwa ukubwa wa ardhi ya Tanzania (Tanganyika) Kenya+Uganda+Rwanda+Burundi bado kupa ardhi inabakia....
Hata JPM alikua na uzalendo na maono kama yako, ila baada ta miaka 6 aliharibu kila kitu Biashara ilawa ngumu sukali ikapanda bei mafuta ya kula seruji nk. Hizo analysis za geographical coverage ya Tanzania sio zinapotosha.
 
Habari wadau!

Sasa kilio cha upungufu wa sukari kitapungua maana mama amefungua milango na kuumuru sukari iingie nchini...

E0NhMwdXIAAW0HL.jpeg
 
Wao walikuwa hawapingi ni sisi wenyewe tu tulikuwa tukifanyiana roho mbaya kuzuiana. Sijawahi sikia tamko la Uganda kuzuia kahawa kuuzwa Uganda. Labda nimesahau.
Ni kweli huku kwetu kuna zengwe
Kwenye kuwapa bei,bei wanayowapa
Huku wanawalalia wakati ug kuna bei nzuri
Basi kwann wasivukishe kimagendo

Ova
 
Hata JPM alikua na uzalendo na maono kama yako, ila baada ta miaka 6 aliharibu kila kitu Biashara ilawa ngumu sukali ikapanda bei mafuta ya kula seruji nk. Hizo analysis za geographical coverage ya Tz sio zinapotosha.
Hakuna kiwanda cha chai kilichojengwa tukawa tuna expert chai

Hakuna kiwanda cha korosho kilijengwa tukawa tuna-export consumable cashews

Hapakujengwa kiwanda cha ku-export consumable products za kahawa, the list goes on;

Aliakuwa na maono, hapakuwa na financial instruments za kufanya mambo yatokee na hatukiwa na exports earnings.

Tunampoza kwa kuona sahihi ila it was unfortunate watu tulitaka Rais aone, yeye huyohuyo atekeleze, no it doesn't work that way.

Na kama hatuoni thamani ya ukubwa wa aridhi na kuwa na comparative analysis kwa kujiuliza wenzetu wanapatia wapi na sisi tunakosea wapi; ni hasara kwa Watanzania kutupeleka shule na tukashindwa kujiuliza maswali magumu ili kuijenga nchi yetu kwa kizazi cha sasa na kijacho.
 
Acha kabisa wakifungua huo mpaka kwenye kahawa narudi kwenye game maana tulikua tunanunua Burundi 1500 kwa kilo moja Uganda unaenda kupiga 4000 chapchap cash na bila maelezo sasa roadblocks upande wa Bongo ikawa mchawi, tukaanza kupita majini nako wakaingia Bongo ukichek gap ya kilo moja 2500 ni pesa nyingi mno
Nchi wanabana wanajua watu wengi watakuwa mabilionea.

Nchi hii kuna watu wanataka pekee yao.

Ndiyo wawe na mabilion,pekee yao ndiyo.

Wafanye biashara export,import

Ova
 
Mama endelea tu kuchanja Mbuga,kutoka kwako kunatuletea faida kwetu wananchi wa chini kabsa..Itakuwa faraja kubwa kama sukari ya Uganda itaingia nchini na kuleta ahueni ya bei kwetu. Mwendazake ametuachia matatizo makubwa mno.Bora tu Mungu alivyompumzisha salama.
 
Labda mama ana kampuni ya kuagiza sukari, lakini pia ni aibu kwa nchi kama Tanzania kuwa na upungufu wa sukari
 
Pesa za wastaafu yule shujaa alizochukua kwenye mifuko ya wastaafu na kwenda kujengea kiwanda cha sukari/mashamba ya miwa kinazalisha tani ngapi kwa mwaka?
Na sasa hela hiyo ya wastaafu ndivyo hivyo tena...isha yoyoma na kiwanda wala miwa haitaonekana!
 
Sidhani kama Mama anawashauri wazuri wa masuala ya Uchumi. Mambo mengi Rais anafanya kama anakurupuka
 
Sasa mnalalamika mama asikubali sukari isiuzwe hapa kivipi wakati viwanda havitoshelezi mahitaji,kuna upungufu wa Tani 300,000 kwa mwaka. Ingekuwa viwanda vinazalisha halaf sukari inakosa soko hapo sawa.

Tatizo watu wengi kichwani hamna kitu..ni kulaumu tuu. Kwahiyo mnaona bora sukari iagizwe Brazil iingie kuliko ya majirani zetu Uganda?
 
Wewe unataka ipigie kona wapi, kabla ya kufika Tanzania? Hiyo ambayo inaagizwa Brazil na kuja Tanzania, mbona hupigii kelele?
Wasiwasi ni kwamba wafanyabiashara janja janja nyingi, naweza agiza sukari brazil, nikaja kuchanganya na kidogo ninayozalisha Uganda, nitakuuzia kwa jina la sukari ya uganda, hichi tu wala sio kingine mkuu wangu, anaenufaika zaidi ni mfanyabiashara wa uganda, sina wasiwasi mwingine.
 
Wawaruhusu na nyie muuze kahawa huko Uganda

Ova
Mbona walikwa wanaruhusu lakini mamlaka za kwetu zikawa zinakamata hiyo kahawa kwa kisingizio kuwa zinauzwa kimagendo? au umesahau kuwa wanaoruhusiwa kununua mazao ni AMCOS pekee
 
Huyu mzee ni adui wa demokraisia - ni wa kukaa naye mbali saana!!
 
Back
Top Bottom