Uganda yasalimisha umiliki uwanja wa ndege Entebbe kwa Wachina

Uganda yasalimisha umiliki uwanja wa ndege Entebbe kwa Wachina

Tanzania inatakiwa kulipa compasation ya hela itakayotumiwa na China kuchimba bandari ya bagamoyo.

We hujiulizi kwa nini China wanaitaka sana hiyo bandari kuliko sisi tunavyoitaka? Wachina wako tayari kuuwa kiongozi yoyote anayepinga bandari hiyo.
C wajenge kwao na kwao bahari si hipo tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Viongozi wa Afrika wanapokuwa wanafanya haya huwa hawakumbuki wananchi wao masikini. Hizo hela watakuwa walizitumbua sasa unadhani yeye Museveni inamuhusu nini? Akiondoka madarakani kizazi chake chote kinao utajiri wa kutisha.
 
Wachina sio watu, mabeberu hawana haya wanatudai tangu miaka ya 60 na still wanatukopesha na mengine wanayasamehe.Hatujawahi sikia beberu kakamata mali ya nchi yeyeto na aachi kopesha.
Anaewadanganya wakakope China ni nani?
 
bilioni 450tsh zimewatoa kamasi waganda,sisi ni trillion 21,wengine tulipokuwa tunalia kifo cha magufuli tulionekana kana kwamba tunalilia ulaji kukatika,sijui ulaji gani ulikuwepo awamu ya 5[emoji17][emoji17]
Bandari ya Bagamoyo sio mkopo ni tri Gvt financing kuna Oman TZ na China.

Bado majadiliano yatafanyika .
Hii Bandari ni 4th generation port na megaships zitakuwa zinatumia bandari ya Dar itakuwa inatumiwa na meli za kawaida.

Lamu na Beira ni bandari za kisasa tukibaki na Dar port tutaachwa nyuma sana.

Ujenzi wa Bagamoyo port uharakishwe baada ya kuweka win win situation.

Bagamoyo port project ni part ya mega project za kuiweka TZ juu kiuchumi kuna BSEZ Bagamoyo Special Economic Zones hundreds of Industries will built na kuna South Korea Institute of Science and Technology itakuwepo pia.
 
Wakikubaliana kule bwagamoyo watuambie na sisi wanaweka nini bondi, maana hawa zungoren hawashindi kuchukua hata watu!
Hata figo zetu watachukua,hawa zingzong wametumwa pesa aisee wamemaliza miti yetu yote mikubwa wamepeleka kwao kidogo wamalize punda zote nchini.
Zingihoo noma Sana hawa
 
bilioni 450tsh zimewatoa kamasi waganda,sisi ni trillion 21,wengine tulipokuwa tunalia kifo cha magufuli tulionekana kana kwamba tunalilia ulaji kukatika,sijui ulaji gani ulikuwepo awamu ya 5[emoji17][emoji17]

Endelea kulia
 
M7 Ni muongo maisha yake yote,hilo bomba halitajengwa Wala nini.Kule Tanga si tulimpa bandari miaka mingi ilishapita,hajawahi kuifanyia chochote kile.

Yule jamaa Ni muongo EA hakuna wa kumfikia.
Hivi washaanza hata kuchimba mtaro kweli,story za bomba kitambo Sana nazisikia
 
Wakuu, wahenga walisema " mwenzio akinyolewa, zako tia maji' hawakukosea!!

Kumekuwa na malalamiko mengi mno kutoka kwa wadau wenye mapenzi mema na nchi yetu pendwa Tanzania( Nikiwemo Mimi mshale21 ), juu ya mikopo na kupanda kwa Kasi kwa deni la Taifa, huku kukiwa na viuluzo vingi namna ambavyo fedha hizo zinatumiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali, matokeo yake, waziri Mwigulu simple tu antoka hadharan anadai tuangalie miradi inayoendelea nchini!!

Tunaporaise doughts juu ya ukuaji wa deni la Taifa hatukurupuk, tunapoonesha kutia mashaka kwenye mikopo tunayoipata kimataifa hatukurupuk, pamoja na kwamba mikopo inakuja na mashart yake na kwamba ni masharti magum au laah, ikumbukwe deni la Taifa linapanda daily, na ni muhim kuonyesha umakini mkubwa katika suala hili!

Bila shaka Rais Samia na Rais wa muda wote wa uganda , Rais Museveni ni marafiki sana, na wanashirikiana sana, na wanapongezana sana , sasa Uganda uwanja wa ndege mchina kapita nao kwa kushindwa kulipa deni, huku kwetu deni linakua kwa Kasi sana!

Kwa kuwa tumeona exactly madhara ya kushindwa kulipa deni kwa kujifunza kwa majirani zetu, ni muhimu Rais Samia aongeze umakini sana kwenye maswala ya mikopo!

Deni la Taifa ni kubwa , Bado mnang'ang'ana mikopo na miradi inayozidi uwezo wa uchumi tulio nao, hii ni hatari sana, na kwa mfumo huu ipo siku tutasikia mbuga Fulani au ziwa au mgodi fulan sio Mali ya Tanzania!!

Punguzen matumiz yasiyo ya lazima
 
Kwa tamaa zetu kuna watu wanaweza kuweka bond Serengeti na Mikumi
Kuna watu wana roho za kishetani
Hivi huyo waziri wa ug anaesema tusingesaini kwa baadhi ya vipengele tena anaongea Bungeni

Hivi walishindwa kumkatakata hata kwa meno

Sasa mchina atapitisha kila kitu maana ni airport yake na uhuru nao hao walinzi kama kawaida yetu watapewa hela ya kubrashi na maisha yanaenda

Nilimpa mmisri $100 kwa safari fupi tu ya Taxi akaniambia chukua Cairo yote

Wacha wabebe kila kitu au wahamishe deni kwa wasomali tuone kama patakalika hapo [emoji23][emoji23]
 
Wanafahamu kila kitu, ila tamaa zao binafsi na ulafi unawatia kiburi na upofu.
 
Taarifa za ndani sanaaaa, eti tumeiweka zanzibar [emoji1787][emoji1787][emoji1787].koloni letuu

33296E4F-5F02-4551-A8AA-E6C0756ABAA5.jpeg
 
Wakuu, wahenga walisema " mwenzio akinyolewa, zako tia maji' hawakukosea!!

Kumekuwa na malalamiko mengi mno kutoka kwa wadau wenye mapenzi mema na nchi yetu pendwa Tanzania( Nikiwemo Mimi mshale21 ), juu ya mikopo na kupanda kwa Kasi kwa deni la Taifa, huku kukiwa na viuluzo vingi namna ambavyo fedha hizo zinatumiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali, matokeo yake, waziri Mwigulu simple tu antoka hadharan anadai tuangalie miradi inayoendelea nchini!!

Tunaporaise doughts juu ya ukuaji wa deni la Taifa hatukurupuk, tunapoonesha kutia mashaka kwenye mikopo tunayoipata kimataifa hatukurupuk, pamoja na kwamba mikopo inakuja na mashart yake na kwamba ni masharti magum au laah, ikumbukwe deni la Taifa linapanda daily, na ni muhim kuonyesha umakini mkubwa katika suala hili!

Bila shaka Rais Samia na Rais wa muda wote wa uganda , Rais Museveni ni marafiki sana, na wanashirikiana sana, na wanapongezana sana , sasa Uganda uwanja wa ndege mchina kapita nao kwa kushindwa kulipa deni, huku kwetu deni linakua kwa Kasi sana!

Kwa kuwa tumeona exactly madhara ya kushindwa kulipa deni kwa kujifunza kwa majirani zetu, ni muhimu Rais Samia aongeze umakini sana kwenye maswala ya mikopo!

Deni la Taifa ni kubwa , Bado mnang'ang'ana mikopo na miradi inayozidi uwezo wa uchumi tulio nao, hii ni hatari sana, na kwa mfumo huu ipo siku tutasikia mbuga Fulani au ziwa au mgodi fulan sio Mali ya Tanzania!!

Punguzen matumiz yasiyo ya lazima
Kwani tumekopa tena?
 
Wacha wakope tu hakuna namna ila viongozi wetu ni matahira sana
SGN_11_26_2021_1637934876563.jpg
 
Back
Top Bottom