Wakuu, wahenga walisema " mwenzio akinyolewa, zako tia maji' hawakukosea!!
Kumekuwa na malalamiko mengi mno kutoka kwa wadau wenye mapenzi mema na nchi yetu pendwa Tanzania( Nikiwemo Mimi
mshale21 ), juu ya mikopo na kupanda kwa Kasi kwa deni la Taifa, huku kukiwa na viuluzo vingi namna ambavyo fedha hizo zinatumiwa katika kutekeleza miradi mbalimbali, matokeo yake, waziri Mwigulu simple tu antoka hadharan anadai tuangalie miradi inayoendelea nchini!!
Tunaporaise doughts juu ya ukuaji wa deni la Taifa hatukurupuk, tunapoonesha kutia mashaka kwenye mikopo tunayoipata kimataifa hatukurupuk, pamoja na kwamba mikopo inakuja na mashart yake na kwamba ni masharti magum au laah, ikumbukwe deni la Taifa linapanda daily, na ni muhim kuonyesha umakini mkubwa katika suala hili!
Bila shaka Rais Samia na Rais wa muda wote wa uganda , Rais Museveni ni marafiki sana, na wanashirikiana sana, na wanapongezana sana , sasa Uganda uwanja wa ndege mchina kapita nao kwa kushindwa kulipa deni, huku kwetu deni linakua kwa Kasi sana!
Kwa kuwa tumeona exactly madhara ya kushindwa kulipa deni kwa kujifunza kwa majirani zetu, ni muhimu Rais Samia aongeze umakini sana kwenye maswala ya mikopo!
Deni la Taifa ni kubwa , Bado mnang'ang'ana mikopo na miradi inayozidi uwezo wa uchumi tulio nao, hii ni hatari sana, na kwa mfumo huu ipo siku tutasikia mbuga Fulani au ziwa au mgodi fulan sio Mali ya Tanzania!!
Punguzen matumiz yasiyo ya lazima