Uganda yasalimisha umiliki uwanja wa ndege Entebbe kwa Wachina

Wanafahamu kila kitu, ila tamaa zao binafsi na ulafi unawatia kiburi na upofu.

Na watasaini mkataba na kuuza bagamoyo
Tatizo ni hela kuna binadamu wanatamaa sana
Hapo wakiwekewa hela kwenye acc wanasaini tu wala hawajali na wanajua hatuwafanyi kitu
 
Na watasaini mkataba na kuuza bagamoyo
Tatizo ni hela kuna binadamu wanatamaa sana
Hapo wakiwekewa hela kwenye acc wanasaini tu wala hawajali na wanajua hatuwafanyi kitu
Ndyo haya tunayopigia kelele kila siku, mwisho wa siku deni ni la Taifa Wala sio la CCM
 
Hivi deni la bomba la gesi limefika kisi gani pamoja na riba yake? Kwa sababu nalo tumepewa na EXIM hao hao wanaokomaa kuchukua Uwanja wa ndege wa Entebbe na wamekomaa kuendesha SGR ya Kenya hadi watakaporejesha hela yao.
 
Ndyo haya tunayopigia kelele kila siku, mwisho wa siku deni ni la Taifa Wala sio la CCM

Uoga mwingi na wanajua
Mtu akiwa na cheo kikubwa anafanya anavyotaka
Watu wanapiga kelele Katiba ila hawajui kuwa kuna mengi yanasiginwa kwenye katiba yetu sasa hiyo mpya itakuwa ni Msahafu ama biblia?

Dhambi zipo tu na dhulma wataendelea kufanya
 
Tukijiingiza kwenye mikopo mibaya itakuwa tumejitakia kwa sababu we have a lot to learn. Tuna scripts za kutosha za kusoma. Tena ni hapo mlangoni tu. Kunakuwa na faida gani Taifa kuja kuwa na facilities za kiuchumi katika Taifa letu kisa tu atazalisha ajira?
Na ajira zenyewe za makampuni ya watu wa Asia mara nyingi zinakuwq Under Employment?
Ajira za wachina na waarabu zitamsaidia nani?
 

Waulize sri lanka kwanini wamepoteza bandari yao. je kwenye hiyo investiment wachina wanapata faida gani? Kwenye hizo dola bilioni 10 tukishindwa inamana china wameweka pesa zao bure kama vile wanatupenda sana na kutupatia trilion 21 for free
 
But bagamoyo port siyo loan,, ni investment

Right. Ni kama tunawakabidhi Wachina hiyo bandari kwa short-term. Halafu baadaye waturudishie tuendelee wenyewe ikiwa imeimarika na miundombinu ya uhakika. Lakini bado wasiwasi mkubwa sana uko kwa aina ya viongozi tulio nao wenye uroho wa pesa za chap chap wasiojali kuuza nchi kwa peanuts.

Ujue Wachina wakiingia mahali huwa hawana mpango wa kutoka. Sijui kwa nini Waafrika hatujui hiyo sera ya Wachina ya kueneza himaya yao (lebensraum) kinamna. Wakishaingia tu wanaanza kupanga na kuingizia mikakati kibao ya kurefusha muda, kuongeza dau lao na idadi ya watu wao kushikilia business lines nyingi inavyowezekana - permanently. Lengo ni kuwa dominant zaidi na zaidi hadi washikilie [emoji817]. Na wanajua vizuri sana jinsi viongozi wetu wasivyokuwa na long-term strategic interests za taifa bali ulaji binafsi. Na sisi waafrika huwa hatuna kumbukumbu ya kitaifa ya muda mrefu - hata within one generation!

Sasa katika hiyo safari ndefu ya uwekezaji, Wachina hakika watatuingizia gia kibao za mikopo na misaada ya kila aina na katika kila sekta ikiambatana na hongo kwa waroho wetu. Tutashtukia mikataba kibao imeshasainiwa kuambatanisha rasilimali zetu muhimu na kutoa advantage kwa Wachina katika maeneo mengi ndani na nje ya bandari. Kama kawaida mengi ya hayo yatawasilishwa bungeni na viongozi wetu kwa propaganda za nguvu na kupitishwa kwa kelele za ndiyoooo! Mwisho wa siku spika, akiwa hai, atauliza “hivi nilikuwa wapi uozo kama huu ukipitishwa?” Wana na wajukuu watabaki kutoa macho: “what the heck is this dude talking about?”. That’s Tanzania.

Hatukupelekwa utumwani na kugeuzwa makoloni hivi hivi. Tumekwama sana kwenye kuwa na leadership with long term strategic vision on national interests - tangu zamani. Halafu tuna ugonjwa wa kupenda kukimbilia kuwa watumwa (subservient) kwa watu wenye nguvu kwa kuamini kuwa huo ndio ujanja kimaslahi. Hakuna umoja hapo; ni kuzungukana tu. Anyway, let’s hope for the best - for sane leadership - this time.
 
Kwa mawazo yako uganda haina tsh bilioni 500?,, Huo si sawa na utajiri wa Rostam aziz tu?, Kwa mawazo yako unataka kusema nchi kama uganda haina hiyo hela?

mimi sijui,ila sijui pia kwanini wameachia asset nyeti kama uwanja wao wa ndege.
 

kwani kilichoshindikana kuiongezea uwezo dar port,mtwara au tanga ni kipi!!!

tuna bandari tatu duni,anakuja mwekezaji ajenge ya 4,,mnafanya udalali kwenye rasilimali za taifa kwa utetezi dhaifu sana.

win win situation usimletee mtu aliyeweka 21 trilllion,hawezi kukuelewa mpaka hela yake irudi.
 
Tanzania inatakiwa kulipa compasation ya hela itakayotumiwa na China kuchimba bandari ya bagamoyo.

We hujiulizi kwa nini China wanaitaka sana hiyo bandari kuliko sisi tunavyoitaka? Wachina wako tayari kuuwa kiongozi yoyote anayepinga bandari hiyo.
Wachina wanajenga infrastructure ya silk road duniani ile kurahisisha uuzaji wa bidhaa zao lengo ni pure business,, wala hawana haja ya kuwawekea masharti ya kisiasa kama nchi za magharibi wafanyavyo
Lengo lao ni pure business that is why huoni kelele za kupinga ujenzi wa bandari kama hiyo kwenye nchi ambazo raia wao wako educated kama kenya,,
Nchi za magharibi wanajua china wakimaliza kuweka miundo mbinu yao,, US as a super power ndo itakua bye bye. That is why kuna propaganda chafu sana kuhusu miundombinu ya china,
US wako tayari kufund watu ili waendeshe kampeni za kupinga uwekezaji wa china ama Russia duniani, na wanatumia hadi uongo mwingi sana,
Jaribu kuresearch suala la ile bandari ya sri lanka ili ujue uongo tuliodanganywa kabla haijasanuka,,
Hata bandari ya bagamoyo inapigwa vita sana, na kuna watu wakamfanya JPM aamini eti serikali itakopa dola bilioni 10 kujenga bandari ya bagamoyo kitu ambacho ulikua ni propaganda chafu
 
Waulize sri lanka kwanini wamepoteza bandari yao. je kwenye hiyo investiment wachina wanapata faida gani? Kwenye hizo dola bilioni 10 tukishindwa inamana china wameweka pesa zao bure kama vile wanatupenda sana na kutupatia trilion 21 for free
Sio kweli,, ilikua bonge la propaganda yaani,, ilivyoelezwa sivyo ilivyotokea
 
Kwa sri lanka mradi ulikataliwa kwa mara ya kwanza hadi mchina alipo badili mkataba.
Au nakosea..
 
Halafu hiyo bank ya exim si ndo walasaini mkataba wa kujenga sgr kipindi cha kikweta halafu magu akaja kuupiga chini
 
But bagamoyo port siyo loan,, ni investment
Wasipopata faidi ndani ya kipindi husika mtalazimka kuwa fidia investment cost zao au kama vip muongezea tena miaka 40. yaani mtu huna control naye anafsnya anavyotaka bila kumwingilia hakuna hata siku moja atasema amepata faida
 
Waulize sri lanka kwanini wamepoteza bandari yao. je kwenye hiyo investiment wachina wanapata faida gani? Kwenye hizo dola bilioni 10 tukishindwa inamana china wameweka pesa zao bure kama vile wanatupenda sana na kutupatia trilion 21 for free
Uzuri Mama ni muelewa sana na anasikiliza ushauri wa wataalam hii bandari inahitajika haraka sana awamu ya 5 ilifanya makosa makubwa sana badala ya kurenegotiate masharti wakaleta siasa Mama yetu ataharakisha hii mega project itakayo tuweka TZ juu sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…