Uganda Yatangaza Nia Ya Kuchukua Jimbo la Ituri la DRC

Uganda Yatangaza Nia Ya Kuchukua Jimbo la Ituri la DRC

Inshort, hii ni vita ya kugombania madini DRC inayoendeshwa na Rwanda na Uganda kwa ufadhili wa mabeberu.
 
Karne hii unavamia mipaka ya nchi nyingine na kuimega halafu majirani wako kimya. Hawa jamaa wameota mapembe wanahitaji kushushiwa kipigo. wakimalizana na hao ipo siku uganda idai kagera rwanda idai kigoma siku ikigundulika kidoma kuna madini au mafuta.
Wakidai KG ni yao, tunawaambia chukueni, baada ya hapo na sisi tunadai Rwanda na KG vyote ni mikoa yetu..
 
TOKA MAKTABA :

16 November 2023


UPDF, JESHI LA KONGO FARDC WAFUNGUA SEKTA MPYA DHIDI YA MAGAIDI WA ADF WALIO KATIKA MISITU YA MASHARIKI YA CONGO


View: https://m.youtube.com/watch?v=OcjVGmehbYY

Vikosi vya Ulinzi vya Jeshi la,Wananchi wa Uganda UPDF na jeshi la Kongo FARDC wamefungua kampeni ya nne kwa kuongeza mashambulizi dhidi ya Allied Democratic Forces ADF katika jimbo la Ituri.

Kikosi cha UPDF kiliongozwa na Meja Jenerali Dick Olum kamanda wa operesheni iliyopewa jina Operesheni Shujaa kiliashiria mwanzo wa ufyatuaji wa risasi katika maeneo yanayokaliwa waasi wa ADF nchini Congo
 
TOKA MAKTABA mwaka 2024

Fahamu utumishi uliotukuka wa wa ajabu ya Jenerali Dick Olum, ambaye Operesheni Shujaa nchini Congo



View: https://m.youtube.com/watch?v=zw3AekpyJFs
Jenerali Dick Olum mwanajeshi ambaye nyayo zake zimeacha alama zisizofutika katika historia ya mapigano ya Afrika.

Alipoocha ndoto za kuwa padri kwa kuondoka shule ya Seminari ya sekondari na kujiunga katika mapambano tangu 1986, mwaka alipojiunga vuguvugu la wanajeshi wa NRA kisha kuingia katika Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Uganda kwa kifupi UPDF ambaye ni kiongozi wa Operesheni Shujaa katika misitu ya Congo, kuwasaka na kuwamaliza waasi wa ADF wanaoleta taabu kwa nchi za Uganda na Congo.
 
Kagame kaingia direct na museveni... Yani wameota mapembe now hawajifichi hadi huyo muhoozi anatangaza hadharani kuchukua kipande cha nchi nyingine. Kwanza sijui hii jumuiya ya Afrika Mashariki ina maana gani kama inashindwa kutatua migogoro na kuwajibishana.
Juzi tu walikuwa kwenye mkutano na Mseveni na Kagame wakiwemo.

Sasa hili tamko ni kuonesha kwamba kilichoongelewa kwenye hiyo mikutano yao hakina maana kwao.

Ofcourse kama wanaweza kuchukua hayo maeneo na amani ikarudi ni sawa tu. Maana wengine wameshindwa kurejesha amani
 
Juzi tu walikuwa kwenye mkutano na Mseveni na Kagame wakiwemo.

Sasa hili tamko ni kuonesha kwamba kilichoongelewa kwenye hiyo mikutano yao hakina maana kwao.

Ofcourse kama wanaweza kuchukua hayo maeneo na amani ikarudi ni sawa tu. Maana wengine wameshindwa kurejesha amani
Ukianza kuchukua huwa hutosheki utaendelea kuchukua na kuchukua. Jana nimeona kwenye mkutano wa AU ethiopia imeweka ramani ikiwa inaonyesha inaoccupy maeneo ya somalia na djbout
 
Mimi sijaelewa malengo na faida za Jumuia ya Afrika Mashariki na malengo yake,hata hiyo SADC ndio hovyo kabisa,nimawaelewa wale viongozi waliojitoa ECOWAS waliona mbali sana,hata Morroco kujitoa AU (Zamani OAU) waliona mbali sana maana wana faida kuliko walioko kwenye AU
 
Mimi sijaelewa malengo na faida za Jumuia ya Afrika Mashariki na malengo yake,hata hiyo SADC ndio hovyo kabisa,nimawaelewa wale viongozi waliojitoa ECOWAS waliona mbali sana,hata Morroco kujitoa AU (Zamani OAU) waliona mbali sana maana wana faida kuliko walioko kwenye AU
Malengo ya hivu vyama ni maslahi ya watawala na viongozi tu. Ndio maana swala linalohusu wananchi hawana habari.

Wanaungana pale tu wanapoiba chaguzi kwenye nchi zao na kupongezana. Ikibidi kuazinana majeshi wakati wa tension za wizi wa kura
 

Mfahamu : General Muhoozi Kainerugaba CDF UPDF Uganda | FACT FILE


View: https://m.youtube.com/watch?v=_kecg3PzokE
Alizaliwa Aprili 1974 mjini Dar es Salaam nchini Tanzania .Elimu; Alipata elimu yake ya awali nchini Tanzania, Kenya, na elimu ya juu Sweden na Kampala Wazazi, (Shule ya Msingi)Kings Collage Budo (O-Level Sekondari)Chuo cha St Mary's Kisubi (O+A Level Secondary) Chuo Kikuu cha Nottingham, Uingereza (Shahada ya Kwanza ya Elimu ya Siasa).Kazi ya Jeshi; 1999 - Alijiunga na ...
 
Rais Felix Tshisekedi - "Mfadhili halisi wa upinzani M23 ambao ulichukua silaha kwa kushirikiana na Rwanda anayejificha: ni Joseph Kabila," alisema. "Ingawa Joseph Kabila hakubali na hachukui jukumu la kujitokeza kwa matendo yake ya kufadhili Movement ya M23"

Mfahamu Jenerali Joseph Kabange Kabila :

View: https://m.youtube.com/watch?v=lElMstEAAww
Joseph Kabange Kabila, mtoto wa kiongozi wa waasi wa Kongo Laurent Kabila , alilelewa kwa kiasi kikubwa na kusomeshwa nchini Tanzania . Alipigana kama sehemu ya vikosi vya waasi ambavyo vilimsaidia baba yake kumwondoa madarakani. Mobutu Sese Seko wa Zaire mwaka wa 1997. Kisha Laurent alichukua urais na kurejesha jina la zamani la nchi hiyo , Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, na Joseph alitumwa China kwa mafunzo ya ziada ya kijeshi . Aliporejea, akawa mkuu wa majeshi ya nchi, akiwa na cheo cha meja jenerali.
 

Mfahamu : General Muhoozi Kainerugaba CDF UPDF Uganda | FACT FILE


View: https://m.youtube.com/watch?v=_kecg3PzokE
Alizaliwa Aprili 1974 mjini Dar es Salaam nchini Tanzania .Elimu; Alipata elimu yake ya awali nchini Tanzania, Kenya, na elimu ya juu Sweden na Kampala Wazazi, (Shule ya Msingi)Kings Collage Budo (O-Level Sekondari)Chuo cha St Mary's Kisubi (O+A Level Secondary) Chuo Kikuu cha Nottingham, Uingereza (Shahada ya Kwanza ya Elimu ya Siasa).Kazi ya Jeshi; 1999 - Alijiunga na ...

Duuh
 
Uvumi kuwa rais Kabila siyo mkongomani, dhambi ya ukabila inavyoitafuna Kongo

7 Oktoba 2014
Mwanaharakati wa Kongo Bw. Jacques Miango apofunguka kwa maelezo ya dhahama aliyokumbana nayo ya wana usalama wa Rais Joseph Kabila alipokuwa akihudhuria Mkutano wa Marekani na Afrika huko Washington DC. Bw. Miango anazungumza na SaharaTV kueleza kilichopelekea tukio hilo. Anapendekeza katika mahojiano kuwa Joseph Kabila hata si Mkongo


View: https://m.youtube.com/watch?v=aFDViCHeZls
 
Leo DRC kesho ni sisi, kama hamuoni huu upuuzi unaoendelea na kuushabikia watoto wenu wataona.
Ni vizuri zaidi huo unaoita upuuzi ukifika pia na huku.

Unapenda eneo gani ligombaniwe ? Kyela na Mbeya yote igombaniwe na Malawi na Tanganyika ? Au CCM ivurumishwe mbali na waasi wa Tanganyika wanayoitaka nchi yao irudi ?

Ipi itakuwa nzuri ?
 
Mfahamu Jenerali Paul Kagame

Paul Foyart

Picha maktaba : Rais Paul Kagame
Paul Kagame, Rais wa sasa wa Rwanda , alizaliwa Gitarama, katikati mwa Rwanda, Oktoba 23, 1957, katika familia ya Watutsi. Mnamo 1959, mauaji ya Watutsi yaliyofanywa na Wahutu yalipoanza, familia ya Paul Kagame ilikimbilia Uganda pamoja na maelfu ya Watutsi ili kuokoa maisha yao. Alikulia Gahunge, Uganda kabla ya kwenda kusoma kati ya 1972 na 1976 huko Kampala.
nunua fluoxetine mtandaoni fluoxetine hakuna dawa
.
Mwaka 1979, akiwa na umri wa miaka ishirini na miwili, Kagame alijiunga na National Resistance Army (NRA), inayoongozwa na Yoweri Museveni, ambayo ilikuwa ni wanamgambo wanaoungwa mkono na Marekani na kupigana na dikteta wa Uganda Idi Amin Dada . Mnamo 1986, NRA ilimpindua Amin na Museveni akawa Rais. Alimteua Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Uganda UPDF pia kuwa naibu mkurugenzi wa Idara ya Utambuzi / Ujasusi ya Jeshi Ulinzi ya Uganda.


Mnamo 1990, baada ya kuhudhuria kambi ya mafunzo ya kijeshi ya Merika huko Fort Leavenworth, Kansas , Kagame alianza kutawala katika nchi yake ya asili ya Rwanda. Mnamo Oktoba 1, 1990, Front Patriotique Rwandais (RPF), iliyojumuisha Watutsi wengi waliohamishwa, na kuundwa katika miaka ya 1980, walianza kushambulia miji ya mpakani mwa Rwanda. Mnamo Oktoba 2, kiongozi wa PRF Fred Rwigema alikufa vitani na Rais Museveni akamteua Kagame kama kiongozi mpya wa FPR.


Kati ya 1991 na 1993, Kagame aliongoza RPF katika mazungumzo huko Arusha, Tanzania kusitisha vita vya wenyewe kwa wenyewe vya Rwanda. Mnamo 1994, hata hivyo, baada ya kifo cha Rais wa Rwanda Juvénal Habyarimana katika ajali ya ndege, mauaji ya halaiki yalianza nchini Rwanda yaliyoelekezwa dhidi ya Watutsi na kuongozwa na serikali ya Rwanda yenye Wahutu. Takriban watu milioni moja waliuawa wakati wa mauaji ya kimbari. FRP ya Kagame, hata hivyo kwa msaada wa Uganda na Waafrika wengine
nunua avodart mtandaoni kwa duka la dawa kwa bei nzuri zaidi leo nchini Marekani mataifa, waliweza kushinda Jeshi la Rwanda ingawa FRP walikuwa wachache kwa moja.


RPF ilipata udhibiti wa serikali ya Rwanda, na kukomesha mauaji ya kimbari katikati ya Julai, 1994, miezi minne baada ya kuanza. Serikali mpya ya Umoja wa Kitaifa kudhibiti nchi ambapo Pasteur Bizimungu akiwa Rais, Faustin Twagiramunga akiwa Waziri Mkuu, na Kagame mwenye umri wa miaka 37 akiwa Makamu wa Rais na Mkuu wa Usalama wa Taifa.

Kagame aliongoza ujenzi wa nchi mwishoni mwa miaka ya 1990, kwa kuwaondoa serikalini viongozi wote wa mauaji ya kimbari na kukuza usawa wa kijinsia katika siasa. Pia aliongoza juhudi za Rwanda kusaidia vikosi vya upinzani vya Kongo katika mapambano yao dhidi ya dikteta wa Zaire Mobutu Sese Seko , hatimaye kumfukuza ofisini.

Mnamo Aprili 17, 2000, Kagame alichaguliwa kuwa Rais wa Rwanda na Bunge na kuchaguliwa tena na Direct Universal Suffrage mnamo 2003 kwa 95% ya kura. Aliendelea kutekeleza sera yake ya ujenzi upya baada ya mauaji ya kimbari kwa kupiga marufuku marejeleo ya kikabila katika katiba na sheria rasmi za taifa.

Alipochaguliwa tena mwaka 2010 kwa asilimia 93 ya kura, muongo wa Kagame madarakani mara nyingi ulitolewa kama mfano wa kuigwa na nchi nyingine za Afrika. Utawala wake ulipata matokeo ya kiuchumi ya kuvutia na kuleta utulivu katika nchi ambayo ilikuwa imejua miongo kadhaa ya vita vya wenyewe kwa wenyewe na hofu ya mauaji ya kimbari miaka michache tu kabla.

Kipindi hiki mara nyingi kimeelezewa kama "Muujiza wa Rwanda" na mnamo 2010, Kagame alipokea "Tuzo la Raia Ulimwenguni" kutoka kwa Wakfu wa Bill na Hillary Clinton kwa kazi yake nchini Rwanda.
Hata hivyo, katika miaka ya hivi karibuni wakosoaji wamebainisha kuwa Kagame anazidi kuwa kiongozi wa kiimla na kandamizi. Wanataja ukandamizaji wake wa vyombo vya habari na mauaji mengi yasiyoelezeka ya wapinzani wa kisiasa.

Mnamo 2015, Kagame alibadilisha katiba ili aweze kugombea muhula wa tatu. Alichaguliwa mnamo 2017 kwa 98.8% ya kura.
 
Back
Top Bottom