Uganda Yatangaza Nia Ya Kuchukua Jimbo la Ituri la DRC

Uganda Yatangaza Nia Ya Kuchukua Jimbo la Ituri la DRC

Hawa wasipothibitiwa watazidi kusonga kila mara. Sijui huu ujinga kwanini nchi za Afrika Mashariki zinawalea hawa wapuuzi.
Hakuna upuuzi hapo ukiwa mjinga na dhaifu lazima utandikwe na wababe bado zamu ya nchi moja iliyo milikiwa na chama kimoja cha kimabavu huku wananchi wake wakiishi kwenye dhiki.
 
Karne hii unavamia mipaka ya nchi nyingine na kuimega halafu majirani wako kimya. Hawa jamaa wameota mapembe wanahitaji kushushiwa kipigo. wakimalizana na hao ipo siku uganda idai kagera rwanda idai kigoma siku ikigundulika kidoma kuna madini au mafuta.
Urusi kaivamia Ukraine,Israel imevamia Palestine,Syria

Uturuki imeivamia Syria

Hapa hakuna cha zama ukiwa mpuuzi na mjinga utavamiwa tu Tanganyika ndipo inapoelekea.
 
Kagame kaingia direct na museveni... Yani wameota mapembe now hawajifichi hadi huyo muhoozi anatangaza hadharani kuchukua kipande cha nchi nyingine. Kwanza sijui hii jumuiya ya Afrika Mashariki ina maana gani kama inashindwa kutatua migogoro na kuwajibishana.
Jumuiya ya wehu
 
Majenerali wote hao ni 'watanzania' kwa nasaba / makuzi kuanzia jenerali Yoweri Kaguta Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jenerali Joseph Kabila, Jenerali Paul Kagame na maofisa wakuu pia maofisa wengine katika majeshi ya Ukanda wa Maziwa Makuu.

Tanzania kupitia Idara zake za Usalama, na Utambuzi Jeshini (MI), waliisoma historia ya wazungu kugawa mipaka kutengeneza vita za baadaye baina ya nchi jirani kwa kisingizio cha ukabila, taifa la Tanzania ikawezeza sana kutengeza mazingira kuzuia hali hiyo.

Historia ya majenerali wote hao wa DR Congo, Uganda, Rwanda hata Burundi utaona hawata waza kuigeuka nchi rafiki katika ukombozi na mapambano.

Tuwape maua vyombo makini vya ulinzi na Usalama Tanzania kuisoma hali hiyo tangu miaka ya 1960 hadi sasa 2025 bila kukosea sana.


TOKA MAKTABA:
Geopolitiki za Nchi za Maziwa Makuu, Ushawishi wa Tanzania

Simulizi za Mzee Ahmad Ibrahim Bakundukize : Vuguvugu la kisiasa 1950 - 1960 nchi za Maziwa Makuu za Tanganyika, Burundi, Ruanda na Congo Zaire


View: https://m.youtube.com/watch?v=55pVkWr0rvk

Waswahili wa nchi hizi 4 wamefanya makubwa bila kujali mipaka ya nchi zao, waliunganishwa na lugha ya kiSwahili na u-mjini wao kuwa popote ni kambi hivyo palipo na "waswahili" yaani panapoongewa lugha ya kiSwahili ni nyumbani na Panafaa kuongoza harakati na vuguvugu la movement .

Source : Mashariki
 
Tutaona na kushuhudia mengi, kwenye huu mgogoro wanufaika ni wengi, Uganda ni mnufaika pia kajiweka wazi.
 
Hawa wasipothibitiwa watazidi kusonga kila mara. Sijui huu ujinga kwanini nchi za Afrika Mashariki zinawalea hawa wapuuzi.
Nchi za Afrika Mashariki zinahusika vipi na upuuzi unaoendelea, hao wakata viuno na wacheza mayenu wapiganie nchi yao wenyewe. Hakuna mpumbavu atakayekubali ku-risk maisha kwa ajili yao huku wenyewe wakiwa busy kujichubua na kucheza masebene kwenye vilabu vya pombe.
Vita si lelemama.
 
Familia yako au wewe mwenyewe ungekuwa unaishi kwenye hizi nchi unazotaka zipigane ungeandika huu utopolo?
Wewe familia yako inaishi huko, pilipili usiyokula inakuwashaje? Kila mtu abebe mzigo wake mwenyewe.
 
TOKA MAKTABA

16 June 2024

URITHI WA UPDF: OPERATION SHUJAA : DOCUMENTARY YA MAPAMBANO DHIDI YA ADF


View: https://m.youtube.com/watch?v=-DWDivbqU1g
Tangu 2021 Novemba vikosi vya ulinzi vya watu wa Uganda UPDF vimekuwa vikipambana na waasi wa Allied Democratic Forces ADF ndani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Mashariki ya Kongo.

Watengenezaji wa dokumentari ya Operation shujaa documentary ,walifika mstari wa mbele , na kuongea na maafisa wakuu wa UPDF chini ya uongozi mahiri wa Jenerali Dick Olum wanaoongoza vita Dhidi ya ADF kama ilivyoripotiwa na mashuhuda,na ripota wetu kuona hali halisi mstari wa mbele wa mapambano hayo kumngoa adui ADF ...
 
Back
Top Bottom