Majenerali wote hao ni 'watanzania' kwa nasaba / makuzi kuanzia jenerali Yoweri Kaguta Museveni, Jenerali Muhoozi Kainerugaba, Jenerali Joseph Kabila, Jenerali Paul Kagame na maofisa wakuu pia maofisa wengine katika majeshi ya Ukanda wa Maziwa Makuu.
Tanzania kupitia Idara zake za Usalama, na Utambuzi Jeshini (MI), waliisoma historia ya wazungu kugawa mipaka kutengeneza vita za baadaye baina ya nchi jirani kwa kisingizio cha ukabila, taifa la Tanzania ikawezeza sana kutengeza mazingira kuzuia hali hiyo.
Historia ya majenerali wote hao wa DR Congo, Uganda, Rwanda hata Burundi utaona hawata waza kuigeuka nchi rafiki katika ukombozi na mapambano.
Tuwape maua vyombo makini vya ulinzi na Usalama Tanzania kuisoma hali hiyo tangu miaka ya 1960 hadi sasa 2025 bila kukosea sana.
TOKA MAKTABA:
Geopolitiki za Nchi za Maziwa Makuu, Ushawishi wa Tanzania
Simulizi za Mzee Ahmad Ibrahim Bakundukize : Vuguvugu la kisiasa 1950 - 1960 nchi za Maziwa Makuu za Tanganyika, Burundi, Ruanda na Congo Zaire
View: https://m.youtube.com/watch?v=55pVkWr0rvk
Waswahili wa nchi hizi 4 wamefanya makubwa bila kujali mipaka ya nchi zao, waliunganishwa na lugha ya kiSwahili na u-mjini wao kuwa popote ni kambi hivyo palipo na "waswahili" yaani panapoongewa lugha ya kiSwahili ni nyumbani na Panafaa kuongoza harakati na vuguvugu la movement .
Source : Mashariki