Uganda Yatangaza Nia Ya Kuchukua Jimbo la Ituri la DRC

Hili kubwa jinga yani.
 
Madaraka yamemlevya. Kubwa jinga.
 
Hili kubwa jinga yani.

Hili ni lengo endelevu la kiusalama la Uganda siyo la CDF wa sasa wa UPDF CDF Muhoozi Kainerugaba ... usalama na uchumi vinakwenda pamoja hivyo ni suala nyeti lenye mguso mpana hasa likihusu tishio linalovuka mpaka toka nje ya mipaka ya Uganda



Meja Jenerali Olum Akabidhi kamandi ya Divisheni ya Milima (Mountain Division) ya UPDF kwa Meja Jenerali Otto​

22 Mei 2022
MakabidhianoOperesheni Shujaa
Mkuu wa Jeshi la Nchi Kavu Luteni Jenerali Kayanja Muhanga amempongeza Meja Jenerali Dick Olum kwa kazi yake iliyotukuka katika Operesheni Shujaa ambayo imewawezesha ‘wanainchi’ kuendelea na shughuli zao za kiuchumi na kijamii katika maeneo ambayo vikosi hivyo vinafanya kazi.

“Namshukuru Jenerali Olum kwa kazi nzuri. Ziara ya wajibu ni lazima katika jeshi. Tunamtakia Meja Jenerali Dick mafanikio katika kituo chake kipya cha kazi,” alisema Lt Jenerali Muhanga akishukuru huduma ya Jenerali Olum katika Kitengo cha Milimani na Operesheni Shujaa.

Luteni Jenerali Muhanga ameyasema hayo leo katika hafla ya makabidhiano ya Kamanda wa Divisheni ya Mlimani (Mountain Division) kutoka kwa Meja Jenerali Dick Olum kwa Meja Jenerali Richard Otto, iliyofanyika Fort Portal. Aliuomba uongozi wa eneo la Rwenzori kumkumbatia kiongozi huyo mpya na kufanya kazi naye kudumisha amani.

Katika maelezo yake, Meja Jenerali Olum alimshukuru Amiri Jeshi Mkuu , Jenerali Mstaafu Yoweri Kaguta Museveni, kwa kumkabidhi uongozi na kamandi ya divisheni ya Milimani (Mountain Division) na Operesheni Shujaa.

Kamanda anayekuja, Meja Jenerali Richard Otto alisema atajenga msingi uliowekwa na Luteni Jenerali Muhanga kama Kamanda wa kwanza wa Operesheni Shujaa na mafanikio ya mtangulizi wake, Maj Gen Olum.

Meja Jenerali Dick Olum, ambaye amekuwa Kamanda wa divisheni ya Milimani tangu 2022 alipochukua nafasi ya Luteni Jenerali Kayanja Muhanga - Kamanda wa Kikosi cha Ardhi wa sasa - alikabidhi kamandi kwa Meja Jenerali Richard Otto.

Maj Jenerali Olum na Meja Jenerali Otto, juu ya utumishi wao wa kijeshi, wamehudumu kama Makamanda nchini Somalia, Jamhuri ya Afrika ya Kati CAR, Divisheni ya 3 ya Wanajeshi wa miguu nchini Uganda, na teuzi zingine.

Hafla hiyo ilihudhuriwa na Kamanda wa pili wa divisheni ya (Mountain Division)Milimani Brig Jenerali Stephen Mugerwa, Kamanda wa kitengo cha anga Entebbe Brig Jenerali Kasaijja, Kamanda wa Brigedi Brigedia Jenerali Asaph Mweteise, mwakilishi wa Majeshi ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Lt Kanali Jacob Apunia FARDC na viongozi kutoka wilaya ya Kabarole
 
Tanzania Inasubiri Nini kuchukua Jimbo moja huko DRC
 
CDF wetu alinusa kitu aliposema kwa sasa kuna tatizo la watu kutoka nje kupenya kwenye mfumo wetu. Hili limeachwa tu lakini bila kushughulikiwa vizuri lina long term impact. Tuchukue hatua
 
Tanzania Inasubiri Nini kuchukua Jimbo moja huko DRC

Majimbo ya Kivu Kaskazini Goms , Kivu Kusini Bukavu na lile la Katanga ni majimbo yanayomezewa mate na wadau wengi kimataifa, ngumi mkononi ya kivita nje nje.

Ni hatari Tanzania kuingia, sisi tumalize SGR reli mpya ili kushiriki kiuchumi kusafirisha madini adimu na kuingiza mizigo ya kwenda Mashariki ya Congo, Rwanda, Burundi inatosha.

Unyakuzi wa jimbo ndani ya Congo tuwaachie wengine, tujikite kuweka vivutio watumie reli, bandari na viwanja vyetu vya ndege, soko la Kariakoo , Soko Jipya la Kimataifa la waChina Ubungo stendi ya mabasi ya mikoani jijini DSM.
 
Mtoto wa mama wa kambo huyo hakuna kudeka man
 
Rawanda na Kigoma ni mbali sana, hakuna mpaka baina ya Rwanda na mkoa wa Kigoma, labda Kagera.
 
UPDF DOCUMENTARY| 30th JANUARY 2020


View: https://m.youtube.com/watch?v=vURTlThkzIA
Toka jeshi la askari "keya" KAR la urithi kutoka kwa mkoloni la kuburuza kwa mabavu raia hadi jeshi la kisasa la Ulinzi la Wananchi wa Uganda UPDF chini ya uongozi imara wa Amiri jeshi mkuu Jenerali mstaafu Yoweri Kaguta Museveni pamoja na maafisa wakuu wa juu kulifanya UPDF kuwa jeshi la nidhamu ya hali ya juu na mfano wa kizalendo
 
Sisi wenyewe tujue Kinacho wakuta DRC kitatukuta!
DRC wana banyamlenge sisi tuna banyankalinzi!
 
DRC kama haina jeshi la kujilinda na kufurusha waasi na wavamizi bora itekwe yote tu ijulikane rwanda na uganda wameitwa congo. ni aibu kubwa nchi kuwa uwanja wa vita kwa mataifa ya nje kuja kupigana katika ardhi ya nchi yako. Hawa washenzi kina muhozi na mjomba wake wasijaribu hata kuwaza kuifanyia undava nchi fulani jirani yao isiyopenda hata kipande kidogo cha ardhi yake kuchezewa na wahuni wa ndani au nje
 
DRC kama haina jeshi la kujilinda na kufurusha waasi na wavamizi bora itekwe yote tu ijulikane rwanda na uganda wameitwa congo. ni aibu kubwa nchi kuwa uwanja wa vita kwa mataifa ya nje kuja kupigana katika ardhi ya nchi yako. Hawa washenzi kina muhozi na mjomba wake wasijaribu hata kuwaza kuifanyia undava nchi fulani jirani yao isiyopenda hata kipande kidogo cha ardhi yake kuchezewa na wahuni wa ndani au nje
 
Ulipita shule hata kidogo? Rwanda anavukaje Kagera mpaka Kigoma!!!???
Aliye karibu na Kigoma ni Burundi na Congo.Rwanda yupo close na wilaya za Biharamulo,Karagwe(Kyerwa),Muleba sehemu kidogo na Ngara.Uganda yupo close na wilaya ya Misenyi,Karagwe(Kyerwa).

Labda alichanganya mambo kidogo
 

Huyu analeta ujinga na baba yake. Kikinuka kila mtu afe kivyake
 
Hakuna Rais Mpumbavu kama Tshisekedi wa Congo DR hivyo ngoja anyooshwe na akina Uganda na Rwanda labda atakaa sawa. Huwezi kuwa Rais wa Taifa lisilo na Jeshi Imara na Taifa / Nchi halafu Usoni unajifanya kuwa Mpenda Amani na chini chini unawaunga mkono Magaidi / Wanamgambo ambao wanatumia Ardhi za Rwanda na Uganda kufanya Upumbavu wao.

Tena GENTAMYCINE nasema kama Rais wa Congo DR anaweza aanze kujiandaa Kukimbia nchi kwani ameshajaa 18 zao.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…