BICHWA KOMWE -
JF-Expert Member
- Jul 21, 2022
- 6,373
- 16,073
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Watu wanatafuta mitaji kwa nguvu. Banks ziko barabarani eti. Au pengine ni kuchanganyikiwa na maisha.Leo tu nimeshuhudia ugomvi usiolazima zaidi ya mara tano. Hapa Jamaa ni wakali, hawataki suluhu nq hawaelewi.
Bajaji, bodaboda, daladala na wenye magari madogomadogo ya kijapani wanaongoza.
Hapa jamaa kaguswa kidogo tu kifaa chenye thamani ya sh 3000, anapewa 4,000 hataki anataka ngumi tu.
Bodaboda wawili wamepisha kidogo tu lakini hawajaumizana, wamepigana vibaya sana.
Kwa utafiti wangu nimegundua watu wengi kama sio mapepo yanawasumbua basi kuna level ya stress kubwa sana hapa jijini hasa ukiangalia wengi tunaishi kwa kulazimisha (kufosi) maisha.
Tuwe watu wa sala, tuwakumbuke sana ndugu zetu wa jiji la dar es salaam hasa wanaomiliki vyombo vya moto. Ni wakali sana na kila mtu amekaa tayari kwa mapambano.
Unaishi Dar mkuuStory tu hizo, hivi kuna sehemu ina walalahoi wengi kama Dar?
Nilikiwa najua wenye komwe mnaubongo wa nyongeza hivyo busara zimepitiliza ugomvi wa nini tena hahahahaaha
Anataka umpige vitano vya nguvu,, hekaheka za dar zinamaliza nguvu za kiume wake zenu wawahurumie tu,Hizo tisa kumi ni pale unafika home bi kidawa naye alianzisha! 😀😀
Story tu hizo, hivi kuna sehemu ina walalahoi wengi kama Dar?
Aisee, hapo ni wapi?... Mbona kama ni Bangladesh, sema TZ ni nchi maskini sana, sura tu hapo zinaonyesha na Kwa Hali hiyo kutoana roho ni mara moja.View attachment 3125871
Kwa hali hii stress lazima