Ugonjwa wa Gauti(Gout): Chanzo, Dalili na Tiba yake

Ugonjwa wa Gauti(Gout): Chanzo, Dalili na Tiba yake

555015_513769728661342_1661088236_n.jpg


Gout is a disease that is caused by uric acid build-up in the body. Uric acid is formed when the digestive system breaks down purines in our food. A diet low in purines helps by allowing excess uric acid to be flushed out in the urine.

Here are some foods that prevent gout.

1.Pineapple
Pineapple contains an enzyme called bromelain that is an anti-inflammatory. Research has found that supplementing with bromelain may relieve the pain associated with gout.

2.Ginger
Ginger is a powerful anti-inflammatory that has been found reapeatedly in clinical studies to reduce chronic inflammation. One study in mice found that a compound in ginger may help to reduce the inflammation associated with uric acid buildup.

3.Turmeric
Turmeric has long been recognized as an anti-inflammatory by many cultures and has been proven in several studies. Some experts recommend a daily dose of turmeric to reduce the inflammation associated with gout.

4.Cherry Juice
Cherry juice has been used to alleviate gout symptoms for decades. Small studies in Italy and the United States have reported success with cherry juice as a gout treatment, though scientists are not certain what mechanism is active in producing this result. Cherry juice does not appear to lower uric acid levels directly but research suggests that its anti inflammatory properties may play a role in reducing gout attack occurrence from 3-4 times per year to about once a year.

5.Hot Peppers
Hot peppers are rich in vitamin C which has been shown to reduce uric acid levels.

6.Watercress
Watercress contains moderate levels of vitamins and minerals and is reputed to be very beneficial to the kidneys. It may help to rid the body of excess uric acid.

7.Lemons
Studies have found that the higher a person's vitamin C intake, the lower the incidence of gout. Try adding lemon to your water every day to alleviate gout symptoms.

,
Mkuu Mzizimkavu popote ulipo Ahsante sana sana,wapi hapa Dar es salaam naweza kupata matibabu sahihi ya ugonjwa wa gauti?
Muhimu sana sana Mkuu,hii nina Bibi yangu anaumwa sana sana,hawezi hata kutembea,alienda KCMC-MOSHI Akaambiwa imekuwa critical,hivyo wakamrudisha nyumbani,huko huko Moshi,but sijakata tamaa,naomba kama una Daktari unamfahani au hospital unaifahamu ambayo anaweza kupata haya matibabu nijulishe Mkuu,nijue,ukiweza na gharama zake itakuwa vem pia,ili nimsafirishe toka Moshi aje DSM Kwa matibabu.
Ahsante sana sana MKUU
 
USICHOKIJUWA KUHUSU GAUTI (GOUT) NA MADHARA YAKE MWILINI

Ukitembea katika jamii hasa mijini utawasikia watu wengi hasa wanaume wanapokunywa bia na kula supu wakizungumzia ugonjwa huu wanaoutaja kama gauti. Unaweza kujiuliza, huu ni ugonjwa gani?

Huu ni ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili unaosababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa kuliko kawaida cha tindikali aina ya uriki (uric acid) katika damu.

Ongezeko hilo la uriki husababisha madhara katika viungo vya mifupa, viungo ni sehemu ya mwili inapokutana, inapoungana mifupa miwili. Kwa kawaida, gauti inaweza kutokea ghafla au ikawa sugu.

Kwa ile inayotokea ghafla huwa na maumivu makali na mara nyingi huathiri kiungo kimoja tu wakati gauti sugu inaweza kuathiri kiungo zaidi ya kimoja na huambatana na hali ya kujirudia ya maumivu na uvimbe kwenye viungo.

Visababishi vyake

Gauti husababishwa na kuwepo kwa kiwango kikubwa kuliko kawaida cha tindikali ya uriki katika damu. Hali hii hutokea iwapo mwili wa mgonjwa unatengeneza uriki nyingi kuliko kawaida au unashindwa kutoa tindikal ya uriki mwilini kama inavyotakiwa.

Ongezeko hili husababisha mrundikano wa tindikali ya uriki katika majimaji yanayozunguka viungo yanayoitwa synovial na hatimaye kutengeneza vijiwe vidogovidogo vya tindikali ya uriki ambavyo husababisha viungo kuvimba na hatimaye kuathirika.

Vihatarishi

Ingawa chanzo halisi hakieleweki vyema, ugonjwa hutokea kuwapata baadhi ya watu walio wa familia moja. Wanaume huathiriwa zaidi kuliko wanawake ingawa wanawake waliokoma kupata hedhi huathiriwa zaidi.

Aidha, unywaji pombe unachangia kwa kiasi kikubwa kuwepo kwa ugonjwa huu pamoja na matumizi ya baadhi ya dawa kama vile za kutoa maji mwilini ambazo kwa ujumla husababisha ongezeko la kiwango cha uriki katika damu.

Vihatarishi vingine ni pamoja na kuwa na ugonjwa wa kisukari, magonjwa ya figo, unene uliokithiri, upungufu wa damu unasababishwa na seli mundu (sickle cell) au aina nyingine za upungufu wa damu, pamoja na saratani ya damu (leukemia).Pia, gauti inaweza kusababishwa na matumizi ya dawa ambazo utendaji wake kazi huingiliana na utoaji wa tindikali ya uriki mwilini.

Dalili za ugonjwa huo

- Dalili kwa kawaida huhusisha kiungo kimoja au vichache. Viungo vinavyoathiriwa zaidi ni pamoja na kidole kikubwa cha mguuni, magoti, au kiwiko cha mguu.

-Wagonjwa huwa na maumivu yanayoanza kwa ghafla, hususan nyakati za usiku. Mara nyingi mgonjwa hudai anasikia maumivu makali kama kitu kinachokata, kupwita au mifupa inayosagana.

-Viunganio katika mwili hubadilika na kuwa na joto, kuvimba na kuwa na nyekundu (hujionyesha zaidi kwa watu wenye ngozi nyeupe). Kwa kawaida mgonjwa hulalamika maumivu makali ikiwa ataguswa kwenye kiungo chenye matatizo.

-Shambulio linaweza kudumu kwa siku kadhaa kabla mgonjwa hajapata nafuu, pia laweza kujirudia mara kwa mara.

-Pia mgonjwa anaweza kujihisi homa. Baadhi ya wagonjwa hupata gauti sugu ambayo huwaletea madhara sugu katika viungo (chronic arthritis) hali ambayo husababisha mgonjwa kujihisi maumivu na muda mwingi kushindwa vizuri kutumia viungo vyake.

Wagonjwa wa muda mrefu huwa pia na vinundu chini ya ngozi inayozunguka viungo vilivyoathirika. Vinundu hivi ni ishara ya muhimu kwa madaktari.

Vipimo

-Kiwango cha tindikali ya uriki katika damu. Hata hivyo, si kila aliye na kiwango kikubwa cha tindikali ya uriki katika damu huwa na gauti.

-Kiwango cha tindikali ya uriki katika mkojo

-Uchunguzi wa maji maji yanayozunguka viungo (synovial fluid) kuchunguza vijiwe katika viungo.

-X ray ya kiungo kilichoathirika.
-Uchunguzi wa utando unaozunguka jointi (synovial biopsy)

Matibabu

Matibabu hujumuisha matumizi ya dawa, lishe pamoja na mabadiliko katika tabia na mienendo ya kimaisha ya mgonjwa.

Dawa hutumika mara tu mgonjwa anapopata shambulio la ghafla. Dawa hizo ni pamoja na:

-Dawa za kutuliza maumivu kama vile codeine, paracetamol

-Dawa za kutuliza mcharuko mwili kama vile ibuprofen (brufen), indomethacin (indocid), diclofenac.

Pia, ni muhimu mgonjwa kumfahamisha daktari wake iwapo ana matatizo yasiyoendana na matumizi ya dawa hizi kama vile vidonda vya tumbo au mzio.

Dawa hizo husaidia kupunguza maumivu, uvimbe, na mcharuko mwili. Baadhi ya madaktari huchoma sindano dawa ya corticosteroids kwenye viungio vilivyoathirika ili kupunguza maumivu na uvimbe.

Kwa kawaida, maumivu huondoka saa 12 baada ya kuanza matibabu, na mgonjwa hupata nafuu kamili baada ya saa 48.

Ili kupunguza kiwango cha tindikali ya uriki katika damu, mgonjwa hupewa dawa za allopurinol au probenecid kila siku.
Wagonjwa wanaotumia dawa hizi ni wale ambao hupata mashambulizi ya mara kwa mara ndani ya mwaka au wale ambao hupata mashambulio makali, wagonjwa waliopata madhara mkubwa kwenye jointi, wagonjwa walio na vinundu au wagonjwa wenye vijiwe vya uriki katika figo.

Lishe na mabadiliko katika mfumo wa maisha husaidia pia kuthibiti na kumwepusha mgonjwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya gauti.

Ushauri:

-Tuache pombe
-Tupunguze ulaji wa vyakula vyenye viasili vya purine (aina ya protini) kama vile nyama ya mbuzi, samaki jamii ya sardines na herring, maini au figo, mkate mtamu, maharage yaliyokaushwa, njegere, baadhi ya uyoga, spinachi. Dhibiti pia ulaji wa nyama kwa kila mlo.

Jiepushe na matumizi ya vyakula vya mafuta kama vile ice creams, mayonise au vyakula vya kuokwa. Kula kiasi kikubwa cha wanga. Iwapo utaamua kupunguza uzito, hakikisha unapunguza kidogo kidogo kwa sababu upunguzaji wa kasi unaweza kusababisha vijiwe vya uric kujitengeneza katika figo.
 
FULL MOTION

Je una tatizo la joints/ gaut kwenye viungio vya magoti na mikono? Pata FULL MOTION tiba Asili ya kuimarisha joints/ viungio vya magoti,mikono na kuimarisha mifupa kwa ujumla.

FULL MOTION inasaidia kurudisha ute ute uliopotea katika joints na kusababisha mifupa kujisugua hivyo kupata maumivu utembeapo.

Kwa maelezo zaidi tuwasiliane 0719 252523
 

Attachments

  • FULL MOTION.png
    FULL MOTION.png
    12.7 KB · Views: 159
Mtoa mada what is gout? (Sio gaut rekebisha juu)....kama unaijua gout tutaamini dawa yako.
 
Habari zenu wana jamvi,

Nina mgonjwa anayesumbuliwa na miguu, sehemu za magoti zinavimba na kupelekea miguu kuuma sana. Nadhani ni Gout. Kaenda hospital lakini wapi, katumia dawa lakini hazijasaidia.

Tangu aanze kuumwa ni muda mrefu kidogo, sasa imeanza kuwaka moto tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inauma tuu. Sasa inauma na kuwaka moto. Kukuja goti ni shida, kutembea nako kwa tabu hadi inabidi aburuze mguu mmojawapo.

Please ndugu zangu, mwenye kujua dawa please.

CC. MZIZI MKAVU msaada please.
 
Pole sana, mimi ni mtalaam wa haya magonjwa, si vema akaanza kunywa dawa kabla ya vipimo. Karibu wilolesi dispensary ipo mafinga tuna vipimo vya aina nyingi. Karibu tumshauri na kumtibu. Kwetu mteja ni dhahabu. Tupo mafinga mtaa wa met
 
Huko hospitali alipewa dawa inayoitwa Allopurinol? Allopurinol is used to treat gout and certain types of kidney stones.
 
MKUU HILO TATIZO MARA NYINGI LINAKUWA NA UHUSIANO NA FIGO. NJOO 4LIFE, TUPO MWENGE NAKIETE HOUSE GHOROFA YA PILI MTU WAKO ATAPATA TIBA NA WALA HATAHAINGAIKA HOSPITALI TENA. TUNAO WATU WALIOKUWA NA MATATIZO KAMA YAKO KWA ZAIDI YA MIAKA 15 LAKINI SASA WANATEMBEA VIZURI NA HAWANA SHIDA TEENA. wasiliana nasi kwa 0659-649891 na kwa kutaka kufahamu zaidi tembelea www. 4life.com
 
Habari zenu wana jamvi,

Nina mgonjwa anayesumbuliwa na miguu, sehemu za magoti zinavimba na kupelekea miguu kuuma sana. Nadhani ni Gout. Kaenda hospital lakini wapi, katumia dawa lakini hazijasaidia.

Tangu aanze kuumwa ni muda mrefu kidogo, sasa imeanza kuwaka moto tofauti na hapo awali ambapo ilikuwa inauma tuu. Sasa inauma na kuwaka moto. Kukuja goti ni shida, kutembea nako kwa tabu hadi inabidi aburuze mguu mmojawapo.

Please ndugu zangu, mwenye kujua dawa please.

CC. MZIZI MKAVU msaada please.
Mkuu nyantuzu ninakupa dawa hii kwa muda atumie lakini ukitaka dawa

kamili utanitafute kwa wakati wako. Juisi ya Bamia. Matayarisho yake Fanya hivi: tayarisha Mabamia yako

4 kwa siku , Na Uyakoshe Vizuri halafu Uyakate Slice ndogo ndogo. Na kisha uyatie kwenye

Jagi na Maji Safi ambayo Unaweza kupata Glasi kama tatu za Maji Funika kwa muda wa masaa

mawili. Baada ya hapo utapata Maji Mazito ya Urenda. Kisha kunywa Mara 3 hadi 4 kwa siku.

Fanya hivyo hivyo kwa muda wa siku 7 au siku 14. Ukitaka Dawa Kamili nitafute kwa wakati


okra+in+water.jpg
 
matunda.jpg





Juisi za mboga na matunda



Mboga zina nafasi kubwa sana katika kupambana na maradhi yanayomkabili mwanadamu na huwa ndiyo kinga ya mwili wakati wote zinapotumiwa. Katika kutibu tatizo la Gauti, juisi ya mchanganyiko wa karoti, tango na Kiazisukari (Carrot, Cucumber & Beet) huweza kusaidia sana.

Tengeneza juisi ya tango na kiazi sukari ya ujazo wa mili lita 100 kila moja, kisha tengeneza juisi ya karoti ya ujazo wa mililita 300, halafu changanya juisi zote tatu ili upate mililita 500 (lita moja) ya juisi yeye mchanganyiko wa mboga hizo tatu na unywe kiasi kila siku.

Kwa upande wa matunda yanayoweza kukupa ahueni na kinga dhidi ya ugonjwa huu ni pamoja na maepo (apple). Tunda hili linajulikana kwa ubora wake katika kutibu Gauti kutokana na kuwa ?malic acid? ambayo ina uwezo wa kuiyeyusha ?uric acid? inayoleta madhara mwilini. Ili kupata faida ya tunda hili, mgonjwa anashauriwa kula epo moja kila baada ya mlo wake wa kila siku.

Ukiacha Apple,(Tufaha) ndizi nayo imo katika orodha ya matunda yanayoleta ahueni kwa wagonjwa wa Gauti. Dayati ya kula ndizi pekee kwa muda wa siku tatu ama nne, itaweza kumpa ahueni mgonjwa. Ili kupata ahueni kwa kutumia ndizi mbivu, mgonjwa anashauriwa kula ndizi pekee kati ya nane na tisa kila siku kwa siku hizo zilizotajwa hapo juu, na asile tunda lingine.

Limau nalo lina faida kubwa kwa wagonjwa wa Gauti. Kwa mujibu wa utafiti wa kisayansi, Vitamin C, ambayo inapatikana kwa wingi kwenye limau, ina uwezo wa kukinga na kutibu maumivu ya viungo kwa kuimarisha tishu za mwili. ?Citric Acid? iliyomo kwenye limau, ina uwezo wa kuyeyusha ?Uric Acid? ambayo ndiyo chanzo cha tatizo. Ili kutumia limau kama dawa, kamua nusu limau kwenye glasi na kunywa mara mbili kwa siku.

DAYATI YA MGONJWA WA GAUTI

Ukishajijua kwamba una Gauti, unashauriwa kuzingatia sana vitu unavyopaswa kula na vile ambavyo hupaswi kula. Kwa wagonjwa wenye hali mbaya, wanashauriwa kufanya funga ya kunywa juisi ya machungwa na maji tu kwa siku tatu ama nne, hii ina maana kwamba katika siku hizo, kitu pekee utakachokula kutwa nzima ni juisi ama maji tu.

Baada ya funga hiyo, utaona nafuu kwenye tatizo lako na unashauriwa kufanya funga nyingine ya kula matunda pekee kwa siku tatu ama nne mfululizo. Baada ya hapo, mgonjwa anashauriwa kupendelea kula vyakula vya asili huku akitilia mkazo matunda na mboga mboga.

Epuka ulaji wa nyama, mayai, samaki, chai, kahawa, sukari, vyakula vitokanavyo na unga mweupe (ukiwemo mkate mweupe), vyakula vya kwenye makopo na vya kukaanga.

Mwisho, mgonjwa anashauriwa kukaa sehemu za wazi ili kupata hewa safi na afanye mazoezi ya viungo mara kwa mara na kuacha kuwaza ili kuepuka mfadhaiko wa akili ambao tumeona kuwa unachangia ugonjwa huu
 
Je huyo mgonjwa ameenda kupimwa kiwango cha uric acid kwenye damu? Kama ni kapimwa na kugundulika kuwa kiwango hicho cha uric acid kiko juu basi ale maparachichi kwa sana kwa sababu hata mimi yamenisaidia sana mpaka sasa napiga nyama kama kawa
 
Back
Top Bottom