Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Habari!

Pole Sana, Jitahidi kufanya yafuatayo.

1. Pendelea kutumia Matunda, Hasa Tunda la PAPAI.. Na mengine yenye kamba kamba.

2.Kunywa Maji Mengi Safi na Ya Kutosha kiasi cha Lita 3.5-5 kulingana na aina ya shughuli zako za kila siku.

3.Tumia Dawa (Zipo ambazo inabd uandikiwe kwenye cheti/daftari la matibabu na zile ambazo unanunua dukani bila cheti)

4.Tumia maji ya uvuguvugu kwa kujiloweka/kukalia sehemu za haja kubwa.

5.Punguza Mazoezi hasa hayo ya kubeba vitu vizito.. Unaweza ukabadili pia aina hiyo ya mazoezi.

6.FIKA HOSPITALI/KITUO CHOCHOTE Cha Huduma za afya kwa Matibabu Zaidi.

Asante na Karibu.
 
Shukrani sana mkuu
 
Shukrani sana mkuu
 
Mkuu walioshauri matunda na kubadili mfumo wa maisha hasa ulaji naungana nao.

Pia mkuu mazoezi sitisha kidogo hasa kama unapiga skwashi na yafananayo na hayo

Pia pombe ipe likizo mkuu

Kingine usitumie nguvu sana kwenye kujisaidia, pia chuchumaa mkuu usikae.

Pressure kubwa wakati wa kujisaidia hupelekea ilo.

Kama upo Dar nakushauri nenda Kairuki hospital pale yupo mzee specialist iyo pande yupo vyema
 
Nashukuru sana kiongozi
 
Umeupaataje huu ugonjwaa au unashiriki michezo michafu???
 
Kula matunda ya kutosha, Mboga za maji na kunywa maji mengi litaisha
 
Haya mawazo yanafanya watu kuto kuweka matatizo yao wazi kwa sababu ya akili kama zako maradhi ya aina hii yana sababu tofauti tofauti, siku yakikukuta utaelewa.
Umeupaataje huu ugonjwaa au unashiriki michezo michafu???
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…