Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

BAWASIRI ni ugonjwa unaojitokeza katika njia ya haja kubwa, hujitokeza kama uvimbe au kijinyama ambacho huweza kuonekana hadi nje. Kwa Kiingereza ugonjwa huu huitwa Haemorrhoids au piles.

Bawasiri inaweza kusababisha upungufu wa damu mwilini lakini unaweza kutibiwa kwa njia ya upasuaji au kwa kutumia dawa mbadala kwa kipindi cha kuanzia wiki sita na kuendelea, inategemea imejijenga kiasi gani.

Bawasiri husababishwa na nini?

Hakuna sababu ya moja kwa moja inayojulikana kisayansi kwamba ndiyo husababisha bawasiri, bali mambo yafuatayo yanaweza kukufanya ukapata ugonjwa huu:

Kufunga choo au kupata choo kigumu kwa muda mrefuUjauzito; wakati wa ujauzito watu wengine wanaweza kupatwa na bawasiri sababu ya msukumo wa mtoto karibu na sehemu ya kutolea haja kubwa.Kushiriki mapenzi kinyume na maumbileUzee; kadri miaka inavyosogea ndivyo inavyokuwa rahisi kwako kupatwa na ugonjwa huu kwa baadhi ya watu.Sababu za kurithi; baadhi ya watu wanaweza kurithi udhaifu wa ukuta huo wa njia haja kubwa ingawa ni kwa asilimia ndogo.Kuharisha kwa muda mrefu.Kutumia vyoo vya kukaa.Kunyanyua vyuma vizito.MfadhaikoUzito na unene kupita kiasi.

Dalili zake

Ili kujua kama una ugonjwa huu ni lazima utasikia maumivu wakati wa kujisaidia haja kubwa, kinyesi kunuka damu wakati wa kujisaidia.

Dalili nyingine ni muwasho sehemu ya tundu la haja kubwa, uvimbe au kinyama kujitokeza sehemu ya tundu la haja kubwa na haja kubwa inaweza kutoka bila taarifa muda wowote.

Matibabu kwa njia ya asili

Matibabu haya yanategemea na umri wa mgonjwa na namna ugonjwa ulivyojijenga na kudumu, unaweza kuhitaji dawa moja au mbili au hata tatu kwa pamoja kati ya hizi zifuatazo. Hivyo, kabla ya kuzitumia ni muhimu kumshirikisha daktari wa tiba mbadala au kwenda hospitali kwa ajili ya uchunguzi zaidi ikiwezaka kufanyiwa upasuaji.

Habbat-Sawdaa

Chukua kijiko kikubwa kimoja cha unga wa Habbat-Sawdaa ukoroge ndani ya glasi moja ya maji na unywe yote. Fanya hivi kutwa mara mbili kwa wiki mbili mpaka tatu hivi.

Habbat-Sawdaa na asali

Changanya gm 500 za unga wa Habbat-Sawdaa na nusu lita ya asali. Lamba kijiko kimoja kikubwa cha chakula kila baada ya saa nne. Ukimaliza kulamba kunywa glasi moja ya maji ya kunywa ya joto la kawaida.

Aloe Vera Fresh

Chukua kipande cha jani la mmea wa Aloe vera fresh (mshubiri) na kikate ukimenye kidogo ukitumia kidole kupata kama utomvu hivi au maji maji yake na upake sehemu ya utupu wako wa nyuma baada ya kuoga kutwa mara tatu.

Jipake nyingi tu na uiache hivyo kwa saa kadhaa au mpaka utakapaoenda kuoga tena.

Tengeneza pia juisi ya mmea huu na uchanganye nusu glasi dawa hii na nusu glasi nyingine ya juisi yoyote ya matunda uliyotengeneza nyumbani ili kupata glasi moja iliyojaa na unywe glasi moja kutwa mara mbili kwa wiki tatu hadi nne. Juisi ya aloe vera ni nzuri kwa kuongeza kinga ya mwili na kutoa taka zote za ndani ya mwili.


Mafuta ya nyonyo

Pakaa mafuta ya nyonyo mara mbili mpaka tatu kwa siku sehemu ya utupu wako wa nyuma kwa wiki tatu hadi nne.

Mambo muhimu ya kuzingatia ili kuepuka bawasiri

Kuzingatia vyakula ni jambo la muhimu mno unapohitaji kupona ugonjwa huu. Mgonjwa anapaswa kula vyakula vingi vyenye faiba, kunywa maji mengi kila siku ili kusafisha mwili na kuepuka kufunga choo, kula mboga majani na matunda kwa wingi, tumia mafuta ya mzaituni (olive oil) kwa wingi kwenye vyakula na epuka kufanya mapenzi kinyume na maumbile.
 
Unamaanisha sehemu gan ya mgomba? Utomvu wa matawi au ule mhimili wake?
Asante
 
Exactly Mimi nilipona Kwa kutumia mixer ya utomvu WA mgomba na Maji maji ya malimao wiki moja tu hadi Leo hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mimi ambaye kinyama kinatokea wakati wa haja kubwa na baada ya dk10 kinarudi ndani dawa gani inanifaa!
 
Kuna UZI humu JF watu walikuwa wanalalamikia izo dawa za virutubisho wakisema hazitibu na unakuta wauzaji wapo kimaslahi tu unakuta dawa mmoja 180000 alafu izo dawa hazija dhibitishwa na Tfda
 
Wakuu... Ningependa kuwashirikisha dawa ya bawasiri iliyonisaidia na mpaka sasa ni miaka 2 tatizo halijajirudia.

Dawa ni hii "ALOVERA" Pasua kwa kulitawanya jani la alovera na hakikisha unaona ile sehemu ya katikati ya jani yenye utomvu.

Pakaa kwenye njia ya haja kubwa utomvu huo kila unapomaliza kuoga wakati wa usiku. Fanya hivyo kwa muda wa wiki 2 au 3 na utaona umepona au unaanza kupona.

Rudi katika ukurasa huu tupe majibu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwa mimi ambaye kinyama kinatokea wakati wa haja kubwa na baada ya dk10 kinarudi ndani dawa gani inanifaa!
Mkuu, huwezi kusoma comments za kuelewa? Watu watu wawili wamethibitisha kuwa utomvu wa mgomba ama ndizi ni dawa nzuri na inaponesha kwa mapema mno kuliko hayo madawa yanayotembea kwa wiki 3 mpaka 4.

Nadhani Mkuu ni vyema ukafuata njia ambayo wenzeko waliitumia maana wana uthibitisho.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…