Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.
Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;

· Tatizo sugu la kuharisha
· Kupata kinyesi kigumu
· Ujauzito
· Uzito kupita kiasi (obesity)
· Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
· Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
· Umri mkubwa


Dalili za bawasiri


· Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
· Maumivu au usumbufu
· Kinyesi kuvuja
· Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
· Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
· Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa



Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri


· Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
· Strangulated hemorrhoids


http://www.tanzmed.com/wp-content/uploads/2011/05/hemorrhoids-2.jpgVipimo na uchunguzi


· Digital rectal examination
· Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
· Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)


Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri


· Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
· Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
· Coagulation (infrared, laser and bipolar)
· Upasuaji;
· Hemorrhoidectomy
· Stapled hemorrhoidopexy


Njia za kuzuia Bawasiri


· High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
· Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
· Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.

KUNA DAWA AMBAZO ZINATIBU KABISA TENA HATA HAITAJIKI KUFANYIWA OPERATION CALL 0683672508
I WILL HELP U




 

Attachments

  • images.jpg
    2.3 KB · Views: 642
Dah! Hii kitu niliipata nikiwa safarini kikazi, unapata maumivu makali sana, nilidhani ndo mwisho wa uhai wangu coz maumivu yalisababisha nikawa nashindwa kutembea na hata kulala...Ilikuwa mbaya sana, nilipewa dawa fulani za kuingiza sehemu ya aja kubwa hata hivyo bado hali ilikuwa mbaya...Mwisho nikapewa dawa za kutuliza maumivu ambazo nimezitumia kwa muda wa mwezi mzima mpaka nilipomaliza safari hiyo ya kikazi ambayo ilikuwa ya mwezi mzima. Baada ya kurejea, niliwaona wataalam pale Regency na wakatipatia dawa kadhaa ambazo nimekuwa nazitumia na ninaendelea vizuri....
 
Njia za kuzuia Bawasiri


  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa
 
leo siku yatatu namaumivu makali sana sehemu yahaja kubwa kwandani kidogo,naogopa hata kujisaidia ndio balaa hata kukaa nakaa kwashida.kwenda hospitali naona aibu,nimegoogle nimeona anal fissure inalingalingana maelezo yake na ninavyo umwa mimi naomba msaada wenu wamaelezo nadawa!
 

mkuu pole sana. mimi sio daktari ila niexperience yangu kwako. Kama haya maumivu yalianza baada ya kwenda haja kubwa basi huo ugonjwa unaitwa hemorrhoids au piles. Kuna veins huwa zinavimba na kuhifadhi damu ndani ya sehemu ya kutolea haja kubwa au nje. Cha kufanya jaribu kula matunda kwa wingi na hasa mapapai ili choo kiwe laini. Pili jitahidi kunywa maji mengi ambayo yatazuia constipation. Dawa za kutumia ni Anusol cream unapakaa kama ni nje na pia nunua (suppositories ) hivi ni kama vidonge lakini sio vya kumeza. Ni vya kuingiza sehemu ya haja kubwa kwa ndani. Dawa nyingine nzuri ni Scheriproct ointment pamoja na vidonge vyake vya kuingiza.
 

asante sana mkuu,ubarikiwe sana.
 

Acha ushoga mkuu
 

Ati kwenda hospitali unaona aibu?? Mmmh... Bado hujaumwa wewee..!!
 
Huuuyu jamaaa anatanuliwa linda ndo maaaana anaogopa host na haata polis
 
kisu kilifikaje huko? dah haya maajabu. weka picha
 
Huuuyu jamaaa anatanuliwa linda ndo maaaana anaogopa host na haata polis

ndio ushauri wako huo,umejiona mjanja sana kwahaya maneno yako...jf is for gt only nandio maana kuna hili jukwaa.
 
BAWASIRI (HEMORRHOIDS)



Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri
Nje: Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?
Bawasiri husababishwa na;
  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu na kinyesi wakati mwengine kutokwa damu kisha ndio kupata kinyesi
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa
Dalili za bawasiri
  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa
Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri
  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids


Vipimo na uchunguzi
  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)
Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri
  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy
Njia za kuzuia Bawasiri
  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji ya Uvuguvugu mengi kwa siku (glasi sita hadi nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.
Kutibu kwa kutumia njia Mbadala Maradhi ya BAWASIRI:

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo uchague nyengine

TIBA 1: MAKAL-ARZAK

Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).

Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

MWIKO : Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.

TIBA 2:
Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

TIBA 3:
Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au "castor oil". Mkuu.@gedoTumia kisha unipe Feedback.
 
Unatoka damu kwenye njia ya haja kubwa? Hïi inaweza kuwa anal fisure au thrombosed hemorrhoids. Anal fissure hutokea baada ya kuta za mk.undu kuchanika kutokana na kunya ma.vi magumu au straining wakati wa kunya. Pia inaweza kutokea kutokana na kuingiza vifaa vigumu kwenye njia ya haja kubwa mf wakati wa uchunguzi wa njia ya haja kubwa. Thrombosed haemorrhoids hutokea pale piles zinapokatiwa blood supply. Hiyo husababisha maumivu makali sana. Nenda hospitali ukachunguzwe ni aina ipi ya tatizo unalo. Kujificha sio suluhu ya tatizo lako.
 
Pole sana usiogope kwenda hospitali. Ondoa aibu ili uokoe afya yako.
 
hii ni anal fissure,yaelekea unatatizo la "choo kigumu"unfortunately ukala vitu kama dagaa au samaki na kuswaga vichwa vya samaki so wakati inaji~stiff kukawa na combination ambayo very stiff <umepata mkwaruzo kwa ndani kula mbogamboga sana+ampicilline after 7 days u'l be fine
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…