Ugonjwa wa Kuota Vinyama Sehemu za Siri (Bawasiri/ Hemorrhoids): Chanzo, Dalili, Tiba na Kinga

Asante@mzizi mkavu.bt wanadai ukifanyiwa operation kukatwa huo uvimbe kidonda hakiponi na hata kikipona huuma kila ujisaidiapo je kuna ukweli ndn yake...???
Ukifanyiwa Operation unapona na ukisha fanyiwa hiyo Operation uwe unakula sana matunda ,maji ya uvuguvugu na mboga za maji ili kufanye tumbo lake liwe linalainisha chakula kwa njia ya urahisi zaidi.

Fijili ndo kitu gani boss, maana huu ugonjwa ulishakuwa ni sehem ya maisha yangu ni mwaka wa tatu sasa nahangaika. Perhaps hii dawa yaweza nisaidia.
Mbegu za figili ( celery ) inapatikana hapo Mjini Dares-Salaam nanda kaulize kwenye maduka ya dawa za kisunna utapata angalia picha hapo chini

Attachments

  • Celery_seed mbegu za figili.jpg
    71.9 KB · Views: 424
  • Majani ya figili.jpg
    43.1 KB · Views: 418
Mtalaamu anaefahamu ugonjwa huu anisaidie kabla sijaharibikiwa,kuna vinyama vimeota kwenye unyeo wangu *puru*kama ilivyo kwenye picha hapo naomba mnijuze japo dawa yake.
===============================================================================================================
 
Mkuu hii inaitwa bawasir, kuna somo moja hapa nilisoma la MziziMkavu naona lingekusaidia. Pole sana hebu mtafute kwanza
 
Last edited by a moderator:
Mtalaam anaefahamu ugonjwa huu anisaidie kabla sijaharibikiwa,kuna vinyama vimeota kwenye unyeo wangu *puru*kama ilivyo kwenye picha hapo naomba mnijuze japo dawa yake.

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje:
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani
: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri

  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri

  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.

DAWA ZA TIBA MBADALA YA KUTIBU BAWASIRI VINYAMA VILIVYOTOKA KATIKA

TUNDU YA HAJA KUBWA

Kila Tiba kati ya zifuatazo ni yenye kujitegemea.Chagua iliyo rahisi kwako.Isipokufaa ndipo

uchague nyengine

TIBA 1:
MAKAL-ARZAK

Chukua 100grm kwa kila lita moja na robo ya maji (1250ml).

Chemsha mpaka ibakie lita moja kamili.
Kunywa ujazo wa kikombe kimoja cha kahawa (50ml) kutwa mara tatu (1×3) mpaka dawa imalizike.

MWIKO
: Mgonjwa asitumie nyama nyekundu aina yoyote,asile pili pili na wala asitumie vitu vikali.Badala yake atumie kwa wingi mboga za majani,matunda,maziwa na samaki.

TIBA 2:

Changanya unga wa Habat soda na Asali safi ya nyuki vipimo vya sawa kwa sawa.Halafu kunywa kijiko kimoja kimoja mara kwa mara.Fuatilishia na kumywa maji glasi moja (250ml) kila umalizapo kunywa hiyo dawa.

TIBA 3:

Jipake mafuta ya Mbarika kwenye utupu wa nyuma ambapo ndipo bawasiri hutokea.Fanya hivyo mara kwa mara, kwa sababu huirudisha hiyo bawasiri ndani.
Mbarika hujulikana vile vile kwa majina ya mbono,nyonyo au
"castor oil". Tumia kisha unipe Feedback.

Attachments

  • bawasiri ya ndani.jpg
    12.3 KB · Views: 165
  • hemorrhoids-s10-illustration-of-thrombosed-external-hemorrhoids.jpg
    26.3 KB · Views: 2,705

Aisee alienda Hospitali gani..na mimi nina dalili ya hiyo..nimeamka asubuhi ninahisi kuna uvimbe pembeni ya anus..
 
Tafadhari madocta nasumbuliwa na tatizo hili na huwa napata maumivu sana nitembeapo kwani huwa nakuwa kama nawashwa sana....tafadhari naomba ushauri kwa hili
 
Acha au punguza pilipili mengine wataongezea pia tafuta Post za mzizi mkavu
 
Nenda hospital na utapatiwa matibabu,kama imefkia stage hyo utafanyiwa operation ndogo yakukatwa its better ukawah mapema coz huwa inaleta matatizo ya uzazi for both sex
 
Tumia dettol na maji ya moto. Weka kwenye beseni halafu kaa ndan ya besen kwa mda wa dkk 5-10. Mara 2 mpaka 3 kama inawezekana.
 
Jamani, niliwai omba ushauri juu ya shost yangu, alikuwa anajisaidia choo kigumu ushauri kauzingatia kwa kula matunda sana papai, parachichi, maji na juice ya ukwaju lakini tatizo bado choo chake ni cha shida alafu kigumu kinachotoka kwa maumivu anahisi kama kapata kidonda njia ya haja kubwa na pia anadai anakauvimbe kadogo akigasuka kanauma kanapelekea kupata maumivu hata anashndwa kukaa, anaomba ushauri je, tatizo hilo linatokana na kutoa choo kigmu?

Tiba yake ikoje?

Pia mzizi alishauri atumie mafuta ya habisoda yanapatikana wapi?
 
Can be either hemorrhoid or abscess, aende hospitali ndio ushauri wangu. Pole
 
BAWASIRI (HEMORRHOIDS)

Bawasiri ni mojawapo ya tatizo ambalo mara nyingi linapotokea humfanya mtu kuwa na aibu kuelezea au kwenda hospitali ili kupata tiba sahihi. Bawasiri au hemorrhoids husababishwa na kuvimba kwa mishipa ya damu aina ya vena katika eneo la mfereji wa haja kubwa.

Kuna aina mbili za Bawasiri

Nje:
Aina hii ya bawasiri hutokea katika eneo la mwisho kabisa la mfereji wa haja kubwa, na huweza kuambatana na maumivu, pamoja na kuwashwa kwa ngozi katika eneo hilo. Mara nyingine mishipa hiyo ya damu (vena) hupasuka na damu huganda na kusababisha aina kitaalamu inaitwa Thrombosed hemorrhoid.

Ndani
: Aina hii ya bawasiri hutokea ndani ya mfereji wa haja kubwa. Na huwa haimbatani na maumivu na wengi huwa hawatambui kuwa wanatatizo hili.
Aina hii imegawanyika katika mainisho yafuatayo:
Daraja I- Bawasiri kutotoka katika mahali pake pa kawaida
Daraja II- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na kurudi yenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja III- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na mtu kuweza kuirudisha mwenyewe baada ya tukio hilo.
Daraja IV- Bawasiri kutoka wakati wa haja kubwa na vigumu mtu kuirudisha baada ya tukio hilo.

Je bawasiri husababishwa na nini?

Bawasiri husababishwa na;

  • Tatizo sugu la kuharisha
  • Kupata kinyesi kigumu
  • Ujauzito
  • Uzito kupita kiasi (obesity)
  • Kupenda kufanya ngono ya njia ya haja kubwa (anal sex)
  • Kwa ujumla mambo yanayo ongeza shiniko katika tumbo.
  • Umri mkubwa

Dalili za bawasiri

  • Damu kunuka kinyesi wakati wa kujisaidia (hematochezia)
  • Maumivu au usumbufu
  • Kinyesi kuvuja
  • Kijiuvimbe katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Ngozi kuwasha katika eneo la tundu la haja kubwa
  • Kujitokeza kwa kinyama (bawasiri) wakati wa haja kubwa

Matatizo yanayoweza kutokana na Bawasiri

  • Upungufu wa damu mwilini (Anemia)
  • Strangulated hemorrhoids

Vipimo na uchunguzi

  • Digital rectal examination
  • Kipimo cha njia ya haja kubwa (Proctoscope)
  • Kipimo cha utumbo mpana (Sigmoidoscope)

Matibabu
Matibabu hutegemea na hali na aina ya Bawasiri

  • Rubber band ligation - Hapa mishipa hufungwa na rubber band ili kuzuia damu kwenda kwenye eneo liloathirika, na hutumika kwenye aina ya ndani ya bawasiri.
  • Sclerotherapy- Hapa kemikali huwekwa kwa njia ya sindano
  • Coagulation (infrared, laser and bipolar)
  • Upasuaji;
    • Hemorrhoidectomy
    • Stapled hemorrhoidopexy

Njia za kuzuia Bawasiri

  • High fibre diet, kula mboga za majani, matunda, na nafaka kwa wingi.
  • Kunywa maji mengi kwa siku (glasi sita had nane kwa siku)
  • Punguza kukaa kwa muda mrefu sana hasa ukiwa chooni, kwa sababu unaweza kuongeza shinikizo katika mfereji wa haja kubwa.

KUJITIBU BAWASIRI KWA NJIA YA TIBA MBADALA DAWA ZA MITISHAMBA NA ZA KISUNNA.

Hemorrhoids, Pils, MARADHI YA BAWASIRI (MGORO) FUTURU: Haya ni maradhi ambayo humsibu mgonjwa sehemu ya haja kubwa ambayo humsababisha kupata maumivu. DALILI ZAKE:

(1) Kupata choo kigumu.

(2) Kutokwa damu sehemu ya haja

kubwa baada ya kujisaidia.

(3) Muwasho au maumivu na joto kali sehemu ya bawasiri.

(4) Kupata maumivu wakati unapokaa.

(5) Vidonda au kutokwa nje na kijinyama sehemu ya kutokea haja kubwa.

(6) Upungufu wa nguvu za kiume.

TIBA: Jambo la kwanza

kabla ya tiba mgonjwa aweze kutibiwa maradhi ya kutopata choo vizuri ikiwa anayo kwa sababu huzidisha maradhi haya. Pia epuka kula Nyama hasa ya ngombe, Pilipili na vitu vikali. Halkadhalika usinywe maziwa kwa wingi.

Kanuni ya kwanza:
Kunywa juisi ya tikiti maji asubuhi kabla ya chakula na usiku kabla ya kulala.Dawa hii hutibu na kuondoa maumivu ya bawasiri.

Kanuni ya pili:
Chukua Asali nusu lita , unga wa kamun Aswad vijiko vitatu vikubwa,unga wa Habat soda

vijiko vitatu vikubwa na unga wa kamun abyadh (Binzari nyeupe)vijiko viwili vikubwa. Vitu vyote hivi

vichanganye pamoja kwa kuvikoroga kwa kijiko. Chukua vijiko viwili vikubwa vya mchanganyiko huu kisha

ukoroge ndani ya kikombe cha maji ya moto. Yakishapoa uchuje halafu unywe kikombe kimoja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Ikiwa ni bawasiri ya kutoka nje au yenye vidonda, paka mafuta ya nyonyo au mafuta ya lozi. (Almond oil).

MARADHI YA KUTOPATA CHOO KIKUBWA KWA NJIA YA URAHISI. AU CHOO KIGUMU KUPATA (CONSTIPATION)

Haya ni maradhi ambayo mgonjwa huwa hapati choo kwa wepesi. Haja kubwa inaweza kutoka baada ya siku moja au mbili au zaidi na ikitoka huwa ni kigumu na hutoka kwa shida na wakati mwingine huwa kama

cha mbuzi. Wagonjwa wengine hupata maumivu wakati wa kwenda haja kubwa. Mtu mwenye afya nzuri hupata haja kubwa kwa kiwango cha chini mara moja kwa siku. Na choo huwa laini na hutoka bila matatizo.

SABABU ZA MARADHI HUSIKA:
(1) Upungufu wa vitamini mwilini hasa vitamin B. (2) Maradhi ndani ya

utumbo mpana. (3) Kula vitu vigumu na vikavu kama vile vyakula vya ngano. (4) Upungufu wa ulaji matunda na mboga. (5) Kutokunywa maji ya kutosha. (6) Upungufu wa fibre kwenye chakula zinazopatikana kwenye maganda ya mahindi. (7) Ukosefu wa kufanya mazoezi ya viungo.

TIBA: Kanuni ya kwanza:

Chukua glasi moja ya maziwa freshi baridi uchanganye na vijiko viwili vikubwa vya asali na kijiko kimoja kidogo cha mafuta ya habitsoda. Kunywa glasi moja kutwa mara mbili asubuhi na jioni. Dawa hii hufanya choo kuwa laini na kupata haja kubwa kwa wepesi.

Kanuni ya pili:
Unga wa sanamaki kijiko kimoja kikubwa, Unga wa tangawizi kijiko kimoja kikubwa, Unga wa habasoda kijiko kimoja kikubwa, na Asali robo lita. Dawa hizi zote zichanganye pamoja kwa kukoroga kwa kijiko. Kula kijiko kimoja kutwa mara tatu.

Kanuni ya tatu:
Asali robo lita, na Unga wa Arki susi vijiko vinne vikubwa. Kula vijiko viwili vikubwa kutwa mara mbili.

Kanuni ya nne:
Kunywa kwa wingi maji ya kunywa ya kutosha na pia ule kwa wingi matunda na mboga.

Kanuni ya tano:
Kula kila siku asubuhi tende saba kabla ya chakula cha asubuhi. Tende hufanya choo kuwa laini.
 
Attachments

  • stock-photo-the-metaphor-of-gastrointestinal-problems-like-constipation-or-diarrhea-45045751.jpg
    26.3 KB · Views: 125
asante mzizi lakin naomba unifahamishe hayo mafuta ya habitsoda hupatkana wap! Kwenye maduka ya dawa au? Nimala ya ng ya kwanza kuyaskia
 
asante mzizi lakin naomba unifahamishe hayo mafuta ya habitsoda hupatkana wap! Kwenye maduka ya dawa au? Nimala ya ng ya kwanza kuyaskia
Nenda katika maduka wanayouza Dawa za kisunna kaulize utapata hayo Mafuta ya Habbat Sawda kwa kiingereza yanaitwa Black Seed oil au Nigella Sativa seed Oil angalia picha hapo chini .

Attachments

  • 264px-Nigella_sativa_oil.jpg
    21.9 KB · Views: 999
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…