Ugonjwa wa Selimundu (Sickle Cell anaemia): Dalili na matibabu yake


Hizo siyo emotions ndugu yangu. Ni reality.
Scince haijawahi kuweza kutoa majibu ya vitu vyote hapa duniani.
Jaribu na kusoma vitabu vya madaktari wakubwa kama Ben Carson na wanasayansi wengine waliofikia point ya kukubali GOD's existence.
 

Ndugu yangu, nimewahi kupona ugonjwa ambao madaktari hawakuona haya kuwaambia wazazi wangu kwamba hakuna tiba.
Hakuna mtu asiyekuwa na imani hapa duniani. Hata kuamnini katika science 100% ni imani pia
 
Hizo siyo emotions ndugu yangu. Ni reality.
Scince haijawahi kuweza kutoa majibu ya vitu vyote hapa duniani.
Jaribu na kusoma vitabu vya madaktari wakubwa kama Ben Carson na wanasayansi wengine waliofikia point ya kukubali GOD's existence.

Suala la kuwepo au kutokuwepo kwa Mungu ni jambo binafsi. Ila suala la kuwepo ugonjwa mahali na kama unatibika ni public issue na ndiyo maana inafall under public health discipline.

Kama tunaongea kwa misingi ya kisayansi na wewe unatumia imani ambayo ni personal, naamini hatuko kwenye ukurasa mmoja. The best way is to agree to disagree and move on..

Vinginevyo tutabishana "until cows come home" and we will never reach the end!

Babu DC!!
 
Ndugu yangu, nimewahi kupona ugonjwa ambao madaktari hawakuona haya kuwaambia wazazi wangu kwamba hakuna tiba.
Hakuna mtu asiyekuwa na imani hapa duniani. Hata kuamnini katika science 100% ni imani pia


The fact kwamba ulipona, tukipeleka wagonjwa 100 kwa huyo Pastor aliyekuponya, wangapi watapona?

That's what science is all about...to be able to replicate the experiment or intervention.

Babu DC!!
 
The fact kwamba ulipona, tukipeleka wagonjwa 100 kwa huyo Pastor aliyekuponya, wangapi watapona?

That's what science is all about...to be able to replicate the experiment or intervention.

Babu DC!!

Sijaponywa na pastor, nimeponywa na MUNGU kupitia jina la YESU ndugu.
In fact, I was a kid (5 to 6 years) and it was mum who prayed for me day and night till I got healed.
Sihitataji experiment, ninachomaanisha ni kwamba, "there is always a chance for anything that seems impossible before science".
Huu sio mjadala wa kidini, pointi yangu ni kwamba haipaswi kumkatisha tamaa mtu. Hata baadhi ya madaktari huwashauri wagonjwa wao kujaribu njia mbadala na sio kuwaambia wakakae nyumbani kwa kuwa hakuna scientific medication/treatment.
 
Msimchanganye Mbofu jamani!!!! Tiba ya Sickle cell IPO na wagonjwa wanapona kabisa na kuondokana kabisa na athari mbali mbali za ugonjwa huo.

Nashukuru BAK kwa taarifa,

Siyo kwamba hatujui kuwa stem cell implant inaweza kumsaidia ila ni kwamba hii siyo conventional therapy ambayo Daktari wa kawaida pale Muhimbili au hospitali yoyote anawe ku-prescribe.

Kama ungeweka na gharama yake, ungeweza kujua kwa nini wengine hatuiongelei kabisa hii tiba...but it is there!

Babu DC!!
 
Reactions: BAK
Mwana FA kwani nae anasumbuliwa na huu
ugonjwa Mkuu,ila nadhani yuko vema tu.

Unapofikisha miaka 21 huu ugonjwa unaanza kutoweka taratibu mimi nina mdogo wangu kwa mwaka nadhani miezi nane anamalizia hospitali lkn sasa yupo normal kabisa ingawa hana kinga ya kutosha mara nyingi anasumbuliwa na maralia na kwa sasa ana miaka 30

Sent from my HTC Desire S using Tapatalk 2
 
Tiba hii imegunduliwa miaka ya karibuni sidhani kama imetimiza hata miaka 15 tangu igunduliwe na gharama yake ni SIFURI. Ila kwa kuwa sina uhakika kama inapatikana nchini kama haipatikani basi kuna gharama za kusafiri, malazi na chakula kutegemea na hiyo hospitali husika.

Kwa jinsi ugonjwa huu unavyowasumbua watoto wengine hata shule wanashindwa kusoma kwa kuwa karibu kila wiki ni wagonjwa na wamelazwa hospitali na wengi kufariki dunia katika umri mdogo sana hii option ya kupandikiza adult stem cells/cord kwa ushauri wangu ndiyo nzuri kuliko zote katika kupambana na ugonjwa huu hata kama kuna gharama hasa ukitilia maanani gharama kubwa na msongo wa kimawazo kumuona motto wako kila siku yuko hospitali akitobolewa ili apatiwe blood transfusion na wakati mwingi mahudhurio yake shule ni hafifu kiasi cha Walimu kukataa motto kuendelea na darasa la juu kwa sababu tu mahudhuruio yake labda yalikuwa ni 25% tu au hata chini ya hapo.

CC: Mbofu


 
Last edited by a moderator:
Mkuu JF ni kisima cha elimu katika mambo mbali mbali ikiwemo tiba za magonjwa mbali mbali. Badala ya kumshauri Mbofu tu pembeni weka maelezo ya kina ya hiyo bidhaa ili wengi wafaidike na maelezo hayo.

Good day

Tunaweza kuwasiliana kwa ajili ya ushauri na kumpatia tiba kwa bidhaa asili ambazo zitamsaidia na ataweza kupona tatizo hilo kabisa. Kwa ushauri zaidi piga 0768 955 185
 
Last edited by a moderator:

Ahsante sana mkuu BAK kwa maelezo yako...

Nimekuwa nikifanyakazi kwa karibu na watu wa Sickle Cell foundation na sijasikia wakiongelea uwezekano wa kutumia hii njia. Sijui kwa nini.

Nikipata jibu nitaliweka hapa.

Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Reactions: BAK

Ohhh kumbe kuna dawa despite how many millions it might cost!!!! ????
 
Pole sana. Kubaliana na hali hiyo. ni tatizo lamaisha.

Mtafute Daktari Bingwa wa Sickle Cell Dr. Jane Makani hapo Muhimbili. wana mradi maalamu utapata ushauri wote.
 
Fuatilia Mkuu Dark CITY na kama Tiba hii haipatikani nchini basi ipigie debe la nguvu sana huko SCF kwa sababu italeta mabadiliko makubwa sana nchini (hasa ukitilia maanani kwamba Tanzania ni nchi ya nne kwa kuwa na wagonjwa wengi wa ugonjwa huu baada ya Nigeria, India na DR Congo) katika kupambana na huu ugonjwa ambao naweza kabisa kuuita killer disease na kuwapa furaha kubwa wazazi, ndugu, jamaa na marafiki pale watakapoona mgonjwa wao amepona kabisa na kamwe hatasumbuliwa tena na ugonjwa huu.


Ahsante sana mkuu BAK[/B[/URL]] kwa maelezo yako...
Nimekuwa nikifanyakazi kwa karibu na watu wa Sickle Cell foundation na sijasikia wakiongelea uwezekano wa kutumia hii njia. Sijui kwa nini.
Nikipata jibu nitaliweka hapa.
Babu DC!!
 
Last edited by a moderator:
Pole sana. Kubaliana na hali hiyo. ni tatizo lamaisha.

Mtafute Daktari Bingwa wa Sickle Cell Dr. Jane Makani hapo Muhimbili. wana mradi maalamu utapata ushauri wote.

Sorry,

Anaitwa Julie Makani...siyo Jane. Na Daktari anayeendasha kitengo cha kuhudumia wagonjwa anaitwa Deo Soka.

Babu DC!!
 
Ohhh kumbe kuna dawa despite how many millions it might cost!!!! ????


Tumesema kuwa hiyo dawa inaweza kutoa radical cure ila pia tukaweka caveats kwamba haijaanza kutumika hapa nchini. Tutajaribu kufuatilia hili jambo na kutoa taarifa.

Babu DC!!
 
Moja ya matatizo yanayoathiri sana jamii kubwa ya watanzania hususani watoto ni ugonjwa wa sickle cell. Ugonjwa huu wa kinasaba huathiri hemoglobin, sehemu iliyo muhimu sana katika muundo na ufanisi wa chembe nyekundu za damu.


Kazi kuu ya hemoglobin katika chembe nyekundu za damu ni kubeba, kusafirisha na kusambaza wa hewa ya oksijeni katika mwilini.


Watu wenye ugonjwa huu, hupata mabadiliko ya vinasaba ambayo hutokea katika nafasi ya sita ya mnyororo wa beta globin (beta chain) katika hemoglobin ambapo kiasili cha valine ambacho ni mojawapo ya tindikali muhimu za amino (amino acid) huchukua nafasi ya kiasili cha glutamate na hivyo kubadili kabisa umbo la chembechembe nyekundu za damu na kuzifanya zishindwe kufanya kazi zake vile inavyopaswa.


Kuna aina mbali mbali za sickle cell, nazo ni HbSS, HbAS, HbSC, HbSD na HbSO. HbSS huwaathiri watu wengi zaidi wakati wenye HbAS huitwa carriers au sickle cell traits kwa vile ndiyo wanaobeba tatizo hili la kijenetekia na kueneza kwa wengine ingawa wao mara nyingi kama siyo zote hawaoneshi dalili zozote za ugonjwa huu.


Dalili za ugonjwa wa sickle cell ni zipi?


Dalili za ugonjwa wa sickle cell hutegemea sana na kiwango cha uathirikaji wa chembe nyekundu za damu.

Kiujumla dalili zinaweza kuwa ni zile zinazohusiana na upungufu wa chembe nyekundu za damu mwilini yaani anemia, unaotokana na kuharibika kwa chembe hizo. Hizi ni pamoja na

  • Kushindwa kupumua vizuri
  • Kizunguzungu
  • Maumivu ya kichwa
  • Ubaridi katika viganja na miguuni
  • Unjano katika macho na ngozi au jaundice
  • Weupe katika viganja, na eneo la macho liitwalo conjuctiva, ulimi na midomo
  • Maumivu ya tumbo
  • Homa
  • Maumivu ya viungo (joint pains)
  • Maumivu ya kifua
  • Damu katika mkojo (hematuria)

Matatizo yanayotokea wakati wa ugonjwa wa sickle cell (sickle cell crisis)


Wakati fulani, wagonjwa wa sickle cell hupatwa na hali ya maumivu makali katika sehemu kadhaa za mwili. Hali hii huendana pia na upungufu mkubwa wa damu. Sickle cell
crisis hutokea katika mishipa midogo ya damu, wengu, viungo vya mwili na hata kwenye mapafu. Matatizo haya ni


  • Matatizo ya kuziba kwa mishipa midogo ya damu (Vaso-occlusive crisis): Kutokana na umbile lake, kiini mundu au sickle cell huwa rahisi sana kuvunjika vunjika pindi zinapopita katika mishipa midogo midogo ya damu. Hali hii hupelekea kuziba kwa mishipa ya damu na hivyo kusababisha maumivu makali na kuzuia usambazaji wa oxijeni katika sehemu zilizozibwa, na hivyo kuathiri viungo vingine mwilini.
  • Matatizo ya damu kujilundika kwenye wengu (Splenic sequestration crisis): Katika hatua hii, wengu huathirika na huwa kubwa kuliko kawaida na pia huwa na maumivu makali. Hukusanya damu nyingi na kuvunja chembe nyekundu zote zilizoathirika na kusababisha upungufu wa ghafla wa damu mwilini.
  • Matatizo ya kupungua kwa damu (Aplastic crisis): Katika hatua hii, upungufu wa damu huzidi kuongezeka na kusababisha, mapigo ya moyo kwenda kwa kasi zaidi na hivyo kuvuruga kitendo cha kutengeneza chembe chembe nyekundu za damu au erythropoeisis kwa kuvamia na kuharibu vyanzo vyake.
  • Matatizo ya kuvunjwa vunjwa kwa chembe nyekundu za damu (Hemolytic crisis): Katika hatua hii, chembe chembe nyekundu za damu huvunjwa kwa wingi zaidi na kusababisha upungufu mkubwa wa damu.
  • Matatizo ya maumivu katika viganja (Dactylitis): Maumivu katika viganja vya mikono na miguuni hutokea mara nyingi kwa watoto wenye umri wa kuanzia miezi sita na zaidi.
  • Matatizo ya ghafla ya kifua (Acute chest syndrome): Katika ali hii, mgonjwa hupata homa, maumivu makali ya kifua, ushindwa kupumua vizuri, na iwapo mgonjwa atafanyiwa kipimo cha x-ray ya mapafu, kipimo kitaonesha mabadiliko yasiyo ya kawaida (pulmonary infiltrates).

Ugonjwa wa Sickle Cell husababisha madhara (complications) gani?


Madhara (complications) za ugonjwa huu yanaweza kutokana na maambukizi ya bakteria mwilini kwa sababu ya upungufu wa kinga au yale yanayohusiana moja kwa moja na kuvunjwa vunjwa kwa chembe nyekundu za damu.

Madhara haya ni pamoja na


  • Maambukizi hasa ya bacteria wa jamii ya Streptococcus pneumonia na Haemophilus influenza
  • Kiharusi
  • Mawe katika nyongo na maambukizi katika kifuko cha nyongo
  • Maambukizi ya bacteria jamii ya Salmonella katika mifupa hasa mifupa mirefu.
  • Kupungua kwa kinga mwilini kutokana na wengu kushindwa kufanya kazi ipasavyo.
  • Mafigo kushindwa kufanya kazi (chronic renal failure)
  • Uume kuwa mgumu na kuuma (Priapism)
  • Shinikizo la damu katika mapafu
  • Wakati wa ujauzito: kutoka kwa mimba (spontaneous abortion) au kudumaa kwa mtoto tumboni kwa mama yake (intra-uterine fetal retardation)
  • Maumivu sugu (chronic pain)

Uchunguzi na Vipimo vya sickle cell

Uchunguzi wa ugonjwa wa sickle cell huwa na malengo ya kugungua uwepo wa ugonjwa huu pamoja na madhara yake. Mgonjwa huchunguzwa kwa kuangalia dalili na viashiria vya sickle cell kabla ya kufanya vipimo kadhaa kuweza kutambua tatizo hili na madhara yake. Vipimo hivi hujumuisha

  1. Kupima damu
    1. Damu hupimwa kwa lengo la kuchunguza uwepo wa sickle cell. Kipimo hiki huitwa Sickling test.
    2. Damu pia hupimwa kwa nia ya kuchunguza aina ya sickle cell inayomuathiri mgonjwa. Kipimo hiki huitwaHemoglibin electrophoresis
    3. Damu pia itatumika kupima Full Blood Picture
  2. X-ray ya kifua
  3. Pamoja na vipimo vingine kama itakavyoshauriwa na daktari

Matibabu ya Ugonjwa wa Sickle cell


Matibabu ya ugonjwa huu hutegemea sana na hali ya mgonjwa. Pamoja na hayo, kiujumla


  • Iwapo mgonjwa atakuwa na matatizo katika mishipa yake midogo ya damu (Vaso-occlusive crisis), inapaswa kupewa maji kwa njia ya mishipa (dripu za normal saline na 5% dextrose), na pia dawa za kupunguza maumivu kama vile morphine, paracetamol au Diclofenac kulingana na atakavyoona daktari kuwa inafaa.
  • Iwapo mgonjwa atakuwa na matatizo ya ghafla katika kifua (acute chest syndrome) au matatizo ya kupungukiwa damu (aplastic crisis), anapaswa kuongezewa damu.
  • Iwapo mgonjwa atakuwa na acute chest syndrome au matatizo yeyote ya ugonjwa huu (any sickle cell crisis), atapaswa kupewa hewa ya oksijeni ili kuongeza kiwango cha hewa hiyo katika mzunguko wa damu.
Aidha wagonjwa wote hupewa dawa za folic acid kwa ajili ya kuongeza damu, antibayotiki kwa ajili ya kupambana na maambukizi ya vimelea wa bacteria, na dawa za Hydroxyurea ambayo husaidia kupunguza kuvunjika vunjika kwa chembe nyekundu za damu.
Kwa sehemu zilizoendelea, watu wenye ugonjwa huu hufanyiwa upandikizi wa supu ya mifupa (bone marrow transplantation) ambao umeonesha kuwa na manufaa makubwa hususani kwa watoto.
Kwa makala za magonjwa na utatibu

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…