Habari ndugu,
Nina mtoto wangu wa kike mwenye umri wa miaka miwili sasa.Tangu alipozaliwa alikuwa na matatizo ya upungufu wa damu(anaemia) na baadae kugundulika kuwa ana tatizo la sickle cell (Hbss).Kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuanzishiwa cliniki pale muhimbili.
Kwa maelezo ya daktari pale muhimbili hakuna tiba ya ugonjwa huu kwa sasa,kinachofanyika ni kuudhibiti (control) tu kwa kumpatia mtoto vidonge vya folic acid and penicilin-V,je
1-hakuna tiba mbadala juu ya tatizo hili?
2-Kwa kuendelea kutumia dawa hizi,mtoto anaweza kukua na kufikia kuwa mtu mzima bila matatizo?
3-Kwa maelezo ya daktari sisi(yaani mimi na mke wangu) tuna chance ya kupata mtoto mmoja mwenye sickle cell kwa kila watoto wanne(kwa kuwa ni carrier yaani HbAs),na kwa vile mtoto wetu wa kwanza tayari anatatizo hili,je waliobaki (watatu) hakuna chance ya wao kupata tatizo hili?
Nitashukuru sana kupata majibu au ufafanuzi wa mambo haya.
Asanteni sana.