Ambition plus,
Mkuu
Ambition plus najua unapata tabu kwa sababu unaumwa, lakini angalia usiwe desperate ukafanyia kazi kila ushauri, elewa kitu kimoja, elimu ya darasani ni nzuri sana lakini wakati mwingine haijithibishi kwenye mazingira halisi. Uzoefu ama experience ni mwalimu mzuri sana kwani kwenye uzoefu, mazingira halisi yanahusika kwa aslimia 100.
Sidharau ushauri wake ila naomba kwa sasa usiufanyie kazi kwa hali uliyo nayo.
kwa haraka haraka ngoja nikupe sababu;
tangawizi ina ukali fulani ambao kwa hali yako ya sasa itaongeza maumivu kila unapotumia
kitunguu swaumu hii ndio usijaribu kabisa kwa sasa, ione tu ikiwa imepikwa ila kama ni kuila mbichi ni kali mno, hata kwa mtu ambaye sio mgoonjwa bado inampa shida sembuse wewe na hali yako ya sasa.
mtindi - hapa napo bado, ingawa mtindi unasifika kurejesha hali ya tumbo kuwa sawa lakini kwa hali ya sasa acha kwanza mpaka utibu hao H.Pilori
apple vinegar --> hii ina acetic acid nyingi na unahitaji kuwa makini pia kwenye viwango vya utumiaji, kwa hali ya tumbo lako kwa sasa sikushauri mkuu.
green tea hii pia ina madhara ya kama kiungulia na nevoursness ambayo si nzuri kwa hali yako ya sasa kwani tayari umesema una hasira na stress ni sehemu ya mtu mwenye hasira mara nyingi
kabichi --> Hii tumia, ni tiba pia kama wengi walivyoshauri.
embe TAMU - definishen ama maana ya tamu hapa ni nini? utajikuta unakula ili mradi yameiva na ukumbuke kuna aina nyingi za maembe na mengine ni machachu tu hata kama yameiva hivyo kama utaamua kutumia, kuwa makini kwenye kuchagua hilo tamu ila kwa ushauri wangu usitumie maembe kwa hali yako ya sasa
asali ni sawa kwa sababu mazingira ya tumbo yashabadilika lakini jaribu ule mchanganyiko wa yai.
Kuna mazingira mengine ukishauriwa, inabidi uwe mvumilivu kusikiliza na uwe jasiri na shupavu kutoutumia huo ushauri kulingana na hali halisi.
Naomba uendelee kuwa makini katika kila ushauri, lakini usipuuze hata neno moja, hii ni shule na ni fursa kwa wengine na walimu ni wengi na watumia fursa pia ni wengi.
Naomba kama ukiweza, ukiitwa PM kupata ushauri usiende, waambie waanike yote hapa wengi wapone kama ni wa kupona na wengi pia wajifunze.
Ahsante