Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Ugonjwa wa Vidonda vya Tumbo (Peptic Ulcers Disease): Kinga, tiba na ushauri

Mengi yameshaongelewa, mm niseme tu pole sana kamanda..
Ukifuata ushauri mbali mbali za wadau utapona tu.
 
Kwa kuongezea, ale mchanganyiko wa kabeji, bamia na karoti uliochemshwa kidogo na kutiwa chumvi kiasi walau mara 2 kwa siku kwa muda wa mwezi mmoja
Halafu mbona kuna dokta nilinsikia redio flani alikua anahojiwa anasema kabeji ni mbaya kwa vidonda vya tumbo
 
micind, Ahsante kwa kutoa ushuhuda, na nimedurahi kusikia mama yako alipona.
Lakini baada ya kusoma andiko lako refu, bahati mbaya haujaitaja hiyo dawa ambayo mama yako aliichanganya na asali. Pia sijaona ukitoa sulihisho kwamba huyo Daktari wa miti shamba anapatikana wapi.
Ama ndio mambo za njoo PM?
 
Kwa bahati mbaya Sina mawasiliano na huyo mwenye dawa ila nitamuuliza bi mkubwa atanipa contact zake kwa mwenye uhitaji Basi nitampatia.
Asante mkuu, ukizipata ebu uziweka hapa tafadhali
 
micind,

Hongera kwa ushauri mzuri pia, ila hawa watu ambao waliwahi kutoa tiba ambayo ilileta ufanisi ni vema mngekua mnaweka maelezo kamili jinsi gani ya kuwapata.
Ukweli ni kwamba, watu wengi wana shida ya tiba kama hizi ila tu viwango vinatofautiana na wengine hawajaweza kusema yote.

Kwa niaba ya wote, naomba utupe namna ya kumpata huyo mtu mwenye dawa, utawasaidia wengi kuliko kushuudia kisha ukatuacha na ushuuda.

Ahsante
 
Ambition plus,
Pamoja na ushauri uliopewa jaribu kumwona huyu 0715660098 from Amana Hospital ametibu watu wengi sana kwa natural remedies au ushauri wa kitabibu zaidi
 
Hizi tiba za kukatazana kula vyakula fulani mimi siwezi huku nikuongezeana magonjwa mengine yanayotokana na kukosa viini lishe vinavyopatikana kwenye vyakula ulivyomkataza kula MWANASIASA HURU,
 
Najua hili suala ni changamoto kwa walio wengi ndo maana kila mtu anatoa maoni yake kulingana na kile acho kifahamu
Kuna baadhi ya hoja za wadau ni nzuri but si rahisi kwa mwenye tatizo kuzingatia haya kwa yote suluhisho ni kupata dawa sahihi. kwa wale wanaofuatilia masuala ya afya tuna fahamu vidonda vya tumbo vina hatua (3) na kuna aina tatu za vidonda vya tumbo.

But guys maranyingi vidonda vya tumbo vinatokana na life style/ mwendo mzima wa maisha ya kila siku kitaalamu haya magonjwa yanaitwa (non communicable diseases). Na miongoni mwa haya magonjwa ni pamoja na presha, kisukali, kansa, matatizo ya macho , reptic ulcers/ vidonda vya tumbo n.k

Swali je haya magonjwa yana tibika vp?
Kiukweli muathirika wa tatizo hili anaweza kutumia pesa nyingi zana hospitalini lkn asipone kabisa na hii tumeshuhudia watu wengi sana wakipata changamoto hiyo, na mara kwa mara mtu anayetumia dawa nyingi za hospitali zenye kemikali nyingi / sumu na hupelekea kuongeza tatizo na wengine wanaenda hadi kwa waganga wa kienyeji ili hali wapate suluhisho.

Mfano , mtu mwenye presha hawezi kupona kama atutumia dawa za hospitali hata hivyo mtu huyu atatumia dawa za hospitali maisha yake yote.

Je kwa wale wenye matatizo haya wanafanyaje ili waweze kupona na kuendelea na shughuli zao za kila siku.

Kama nilivyosema awali matatizo yote yanayosababishwa na life style/ non communicable diseases suluhisho lake ni tiba lishe amini hilo, but tiba lishe zip hapo ndo kuna changamoto kubwa kila mtu atajinadi kwa namna yake ila mhusika mwenyewe ataangalia.

Nataka nitumie hii chance kuwaasa watu kuwa hili tatz linatibika kabisa ni utayari wako tu. Kwa wale watakao pendezwa nitawasaidia kuwoongoza mahali ambapo unaweza kupata tiba lishe za uhakika . angalia hiyo picha chini
IMG-20190917-WA0063.jpeg
 
Ambition plus,

Mkuu Ambition plus najua unapata tabu kwa sababu unaumwa, lakini angalia usiwe desperate ukafanyia kazi kila ushauri, elewa kitu kimoja, elimu ya darasani ni nzuri sana lakini wakati mwingine haijithibishi kwenye mazingira halisi. Uzoefu ama experience ni mwalimu mzuri sana kwani kwenye uzoefu, mazingira halisi yanahusika kwa aslimia 100.

Sidharau ushauri wake ila naomba kwa sasa usiufanyie kazi kwa hali uliyo nayo.
kwa haraka haraka ngoja nikupe sababu;

tangawizi ina ukali fulani ambao kwa hali yako ya sasa itaongeza maumivu kila unapotumia

kitunguu swaumu
hii ndio usijaribu kabisa kwa sasa, ione tu ikiwa imepikwa ila kama ni kuila mbichi ni kali mno, hata kwa mtu ambaye sio mgoonjwa bado inampa shida sembuse wewe na hali yako ya sasa.

mtindi - hapa napo bado, ingawa mtindi unasifika kurejesha hali ya tumbo kuwa sawa lakini kwa hali ya sasa acha kwanza mpaka utibu hao H.Pilori

apple vinegar --> hii ina acetic acid nyingi na unahitaji kuwa makini pia kwenye viwango vya utumiaji, kwa hali ya tumbo lako kwa sasa sikushauri mkuu.
green tea hii pia ina madhara ya kama kiungulia na nevoursness ambayo si nzuri kwa hali yako ya sasa kwani tayari umesema una hasira na stress ni sehemu ya mtu mwenye hasira mara nyingi

kabichi --> Hii tumia, ni tiba pia kama wengi walivyoshauri.

embe TAMU - definishen ama maana ya tamu hapa ni nini? utajikuta unakula ili mradi yameiva na ukumbuke kuna aina nyingi za maembe na mengine ni machachu tu hata kama yameiva hivyo kama utaamua kutumia, kuwa makini kwenye kuchagua hilo tamu ila kwa ushauri wangu usitumie maembe kwa hali yako ya sasa

asali ni sawa kwa sababu mazingira ya tumbo yashabadilika lakini jaribu ule mchanganyiko wa yai.

Kuna mazingira mengine ukishauriwa, inabidi uwe mvumilivu kusikiliza na uwe jasiri na shupavu kutoutumia huo ushauri kulingana na hali halisi.

Naomba uendelee kuwa makini katika kila ushauri, lakini usipuuze hata neno moja, hii ni shule na ni fursa kwa wengine na walimu ni wengi na watumia fursa pia ni wengi.

Naomba kama ukiweza, ukiitwa PM kupata ushauri usiende, waambie waanike yote hapa wengi wapone kama ni wa kupona na wengi pia wajifunze.

Ahsante
 
Yes kama nikila embe, nanasi, (citrus zote) soda, majuis ya dukani, vitu vya baridi, viazi, nyama yaani kifupi sina chema tumbo linanivuruga wakati wote. Nikila kidogo tumbo linajaa gesi. Nimekua mkali kama pilipili. kila saa mahasira, nachukia vitu vya kijinga hadi wakati mwingine najishangaa.
Pole sana mkuu. Ndiyo nimeiona hii post yako leo. Nina ushauri ufuatao.
1. Uwe na tahadhari kubwa kwa watu wanakumabia kuna wataalam wa dawa za kienyeji. Wengi ni matapeli. Watakula fedha yako na hutapona. Kama ni dawa za kienyeji basi usilipe fedha nyingi. Dawa yoyote ya fedha nyingi ni utapeli.

2. Wengi wanaosema walikuwa wanaumwa vidonda vya tumbo halafu wakapona inawezekana isiwe walikuwa wanaumwa. Njia nzuri ya kugundua vidonda vya tumbo ni endoscopy uliyofanya.

3. Wataalam wanasema sababu kubwa ya vidonda vya tumbo na hao H- Bacteria uliokutwa nao. Bila kuwamaliza hao hutapona.

4. Hili ndilo hasa la wazo la msingi: Una uhakika dawa unazotumia siyo fake au zimeisha muda wake wakafanya kufoji? Nina cases za watu wangu wa karibu waliambiwa wana hao bacteria na baada ya kunywa dawa hawakupona. Hata baada ya kurudia hawakupona. Nina wasiwasi huenda Bongo kuna dawa nyingi feki. Mimi nilikutwa na hao bacteria nikaandikiwa dawa za siku saba tu na nikapona, ila ilikuwa nje ya nchi. Ndiyo maana nimekuwa na wasiwasi na dawa unazokunywa. Kitaalam wanasema ni course ya siku 14 au zaidi ila nilipopewa niliambiwa hizo dawa ni nzuri na siku saba zinatosha.

5. Kwenye cheti ulichoambatanisha inaoneka kama walichukuwa specimen kutoka tumboni halafu wakapima ndiyo ikakuwa hao bacteria. Unatibiwa hospital nzuri? Kuna uwezekana wa kuotesha hao bacteria na kuona wanakufa kwa dawa gani? Mwisho nizidi kusisitiza tena hakikisha unapata dawa za kuaminika. Ikiwezekena kama kuna mtu aliye nje ya nchi mwombe akuletee.
 
macho_mdiliko,
Mkuu nashukuru sana.Umenipa mwanga sana.Hospital ninayotibiwa ina eleweka.Hapo kwenye dawa ndio napata walakini.Inabidi nifanye kitu.Niagize kutoka nje.Ila kwa sasa kuna baadhi ya dawa nataka nitumie kwanza.Nisipopata nafuu nitaagiza.Asante
 
Namba ya huyo bi mkubwa anayetibu kienyeji ulcers kikamilifu ni 0787 832 510 kwa faida ya wengi badala ya kutafutana PM.
Healing process ya miili yetu inatofautiana. Binafsi, kipindi naelekezwa kwake nilikua na hali mbaya ya maumivu makali, lakini nilipata ahueni haraka na nikasahau maumivu na nikazingatia masharti. Kwa sasa nadunda!
Tuzidi kupeana tiba wandugu. Huu ugonjwa unaumwa jamani nikikumbuka mateso yake.
 
Tumia bamia kwa wingi hasa changa kidogo, zinasaidia kulainisha tumbo chakula kikiingia kiteleze na kisikwangue vidonda, nilisaidika
 
macho_mdiliko,
Mkuu inawezekana ulikua stage ya mwanzo kabisa ya ugonjwa. Mimi pia binafsi yangu nilifanya endoscopy. Na nilionana na Gastroentrologist pale Kairuki, Dr Ndile na ndiye ali-prescribe hiki kipimo. Nilitumia laki 2 kupata combination ya dawa aina tatu na ni za Europe; Sweden, Cyprus na South Africa. Nilitumia kwa wiki 1. Na kuna dawa nikaendelea nayo mwezi mzima. Hii ni tiba ya sasa ambayo Mganga Mkuu wa UK ameipendekeza kutibu H.Pylori tofauti na tiba ya zamani ya Heligo Kit ambayo kwa mujibu wa Mganga Mkuu wa Uingereza ni outdated - ina bacteria resistance.

Lakini, baada ya miezi 2 ugonjwa ulinianza tena. Na ulinianza immediately baada ya masiku kadhaa ya kutumia vyakula ambavyo vilikua ni troublesome. Hatimaye, nikatafuta tiba mbadala ambazo kiukweli zimenitibu. Na kumbuka ugonjwa nimeumwa for almost 6 yrs. Nimetumia sana omeprazole na injections za kutosha. Na kingine unachopaswa kujua, stool ndiyo pekee inayoweza kuonyesha kiwango cha bakteria ulionao tumboni. Endoscope inaonyesha madhara uliyonayo tumboni.
 
Back
Top Bottom