Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

Hizo fitna anazofanya ni Kama zipi tujue?
 
Chunguza vizuri hao wote ulowataja nani anaanzaga kumzingua mwenzake.... Isijekuwa unachuki zako jombaa.
 
Tatizo mna bonga Sana , Harmonize akifanikiwa mnamrushia dongo Diamond na kumcheka , wakat 80% ya watu wenye uelewa na mambo ya mtandao na Wana passion na mziki wa bongo ni fan kidanki danki wa mond ....na konde boy anategemea hao hao ndo wamtoe , aendelee Tu kucheza twist , wanigeria hawana unafiki huo....
 
Umeongea kitu kikubwa sana Mzee ila team Wcb watakuponda na watakukebei sana

Kama Diamond angebaniwa wakati anatoka sidhani kama angefika hapo alipo, Team ina meneja anajisifu kwa kujiita kamati ya Fitina
Diamond alibaniwa Sana na hao mawingu wako na wahuni kibao waliokuwa wanajifanya bongo fleva ni yao, ikabid atobokee Nigeria chini ya kamanda Sallam Sk , kitu kikawaka MTV , kila mmoja apambane kivyake endeleeni kumsuport konde boy mwacheni mond na fans wake
 
Tatizo kila msanii anataka afanane na Mond , asipomfikia anachukia anaona anabaniwa , diamond ni Baba Yao , Ni Mungu wao ndo aliwaumba , ?? Wapambane kivyao
 
Yaan kinacholalamikiwa hapa ni kuwa fans wa WCB wanambania konde boy Kwa influence ya Mond , inadaiwa wamemkimbia kisa katoka WCB na lawama zote zinamwangukia Diamond
 
WCB ni Diamond peke yake, ukiwa katika Lebal hiyo mashabiki wake ndio watakua wako, ukiondoka unabakia na mashabiki wa Muziki pekee, wale wenhine wanabaki nae na kukuchukia wewe.

Naamini hivi kwasababu, wanaojitoa WCB sio member wa kundi au Band kusema tuwaone peke yao watafanyaje?

Na kama Nyimbo alizozitoa nje ya WCB angezitoa akiwa hajajitoa amini zingekua habari nyingine, mfano UNO na ingekua na Collable ya Mond ndani yake.

Sisi wabongo ni wavivu so inapotokea mtu kufanikiwa huchukia wengine kuwa juu yake ili kutokana na uvivu wake asije kuanza kutumwa.

Hali hii inasababisha Tasnia nzima kukosa uwazi na yote ni woga wakushuhudia wengine wakipata mafanikio.

Mfano. Thamani ya msanii mmoja mmoja hajulikani, malipo wanayoyapata katika tour, social media au shows hawayaweki wazi. Maisha yao tuu ni siri wengi hatujui wanaishi vp...

kwa vile ni kibongo bongo utaambiwa unafuatilia mambo ya watu ambao wengi wao hawana maisha ya majina yao. Lakini maisha yakina jigga tunayajua hadi mtaa anaoishi na kwa mwaka kaingiza shing ngapi na ni mmoja wa mabilionea.

Kwahiyo naamini katika uwazi kama chachu yakuchochea wengine wapambane zaidi na hatimae kupatikana wasanii wengi wenye mafanikio. Kuliko hivi sasa wenhi wanaogopana kutokana na njaa.




Sent using Jamii Forums mobile app
 
Na haya yote ni matokeo ya wimbo wa kwangwaruu , hamna kingine
 
Hapo kwa BurnaBoy mtoa tafadhali

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Me sipo kwa Diamond wala Harmonize, me nipo tu kama mchambuz wa mziki , nachojiuliza ni kwamba mfano USA yan Chriss Brown amwachie nafasi August Alsina aachie ngoma ili nae ashine ? Mbona Marekan kila mtu kwa Muda wake anaachia ngoma zake anaacha jamii ichague, Yan Cardi B asubir Nicky Minaji avumee ye ndio aachie ngoma ? Nope thats not true, ila hata hivyo Bongo kuna tatizo, kama uchawi upo kweli(which i dont believe) watakuwa wanarogana sana, Kitu kibaya kwenye mziki wa Tanzania ni kwamba Diamond ambae ndio mkubwa hataki wenzake wafanikiwe sasa huwa simwelewi kwakweli, we angalia jambo moja mtu alijitoa lebo ukataka alipe hela ili awe na copyright ya ngoma zake kalipa me nlidhan after payment they were supposed to be good, Yan bado kuna kwere tu ? Nakumbuka Birdman, Lil wayne alivyojitoa cash money alidemand hela na alipolipwa wakawa wako poa tu na birdman na kuna ngoma wamefanya pamoja na ndio birdman alikubali kuachia the carter IV.

SOMO LA KUJIFUNZA

Kwenye maisha hapa duniani tusiwe watu wa roho ya kwanini, hata tukiwa successful hatuwez kuwa na baraka, kuna leo na kesho jitahidini kuwa humble one way or the other...BE HUMBLE....


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Huu wimbo una uhusiano gani na domo na zari?

Yaani unawashwa washwa balaa.
Diamond na Zari washaachana na maisha lazima yaendelee ila una chuki Sana as if we ndo ulitoka kimapenzi na mondi badala ya Zari
 
Watu kwa lawama!

kelphin kepph
 
Harmonize aache kulalamika, kwa namna alivyojiondoa WCB amemnufaisha Diamond, mashabiki wamekuwa na huruma zaidi kwa Diamond wakidhani ndie alitendwa, kinyume chake mashabiki wamekuwa na chuku juu yake wakiamini ni mshenzi asiye na fadhila.

Imekuwa mapema sana kwake kuungana na maadui wa Diamond, hii inaendelea kuwafanya mashabiki wamuone yeye against Diamond, matokeo yake wameamua kumuadhibu.

Binafsi naona atazidi kushuka vile yuko peke yake ni vigumu kukaa midomoni na machoni mwa watu siku zote. Pole yake ila namuombea mazuri.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hio video nimepost bila kuquote mtu wala kuandika caption mbona unajishtukia kama umetiwa doko?
Hata tukija kwenye Hiyo video niambie video ipi hapa bongo ambayo maudhui yake au scenes zake hazifanani na video yoyote duniani?
 
Lack of originality.

Mmakonde 98% anamuiga Diamond , hana ubunifu ndio maana anazidi kufeli kila kukicha.

Na bado [emoji23]
 
Kwani kabla Diamond hajakua kimziki mziki ulikuaje? Ulikua umekua?
ulikua mzuri sana kila mtu alipewa nafasi yake kwa ukali wake.
Ndo mana unaona hata diamond amefika alipofika
kwa sasa kuna namna mziki umetengenezwa haupendezi tena
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…