Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

Ugumu anaoupitia Harmonize ni kielelezo tosha kwanini sanaa yetu haikui. WCB inaua wasanii nje ya lable yao

Mbona diamond kawasaidia wasanii wengi amempa connection shetta kufanya collabo na kcee, chege na run town, amemlipia video ya dully Sykes inde, kamsaidia dj ommy kumpa connection mpaka kumwezesha kufanya vizuri medani za kimataifa.Pia angekuwa ni mbinafsi Kama unavyosema harmo asingekuwa msanii wa kimataifa, Asingemtoa Rayvanny, Lavalava na mbosso
Ndiyo maana nasema huyu jamaa ni boya sana....hajui kama bila Diamond hakuna Konde Boy
 
Japo mimi sio shabiki wa Diamond lakini huwa nashangaa sana mtu anaposema sijui Diamond mbinafsi, anataka kuwa juu peke yake, anatengeneza beef na wasanii wengine nk. Msanii anabaniwa vipi na Diamond kama yeye mwenyewe hajitumi, hana uthubutu, hajui kuutangaza mziki wake, hatafuti angalau collabo na wasanii wakubwa wa nje ambapo watamtangaza zaidi au muziki wake kuvuka border.

Muziki ni biashara kila mtu anahangaikia upande wake unabaniwa vipi na msanii mwingine? Harmonize kuondoka WCB binafsi hata mimi nilipongeza nikijua ataleta changamoto kubwa katika mziki wa bongo. Sasa iweje aonekane anabaniwa wakati lebo aliyokuwepo mwanzo ndio inaongoza kubaniwa na media nyingi?

Wakati yupo WCB anatoa hit songs haikua Clouds Media, East Africa Radio/TV, eFM, Millard Ayo ambazo zilikua zikimsampoti leo hii media hizo zinamsapoti Harmonize hapa anabaniwa vipi? Tayari wakati yupo WCB alishafanya International Collabo nyingi ambazo zimeshafanya atambulike zaidi Africa hapa napo nini kinamzuia asiwe mkubwa zaidi ya Diamond?

Pengine hii ndio ingekuwa fursa kwake kutoa hit songs nyingi na kujiongezea fan base kwasababu yupo huru, hebu nielewesheni labda sielewi wakuu maana ya msanii kubaniwa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nigeria hawabebani.Kuna wasanii wengi wa Nigeria walifanya vizuri na wakaporomoka na kupotea na wengine wanasurvive.Music ni survival for fittest.Ukitoa nyimbo lazima uibrand ili iendelee kuwa juu.Kama Konde Gang walijua maisha ya music ni rahisi kiivyo basi walipotoka maana music unakutaka uwe juu always ndivyo Nigeria wanafanya.Kila mtu anapambana kuwa bora ,yeye management yake.Sasa leo huku majungu tu .Kila mtu ale kwa urefu wa kamba yake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Diamond katengeneza kundi la misukule kama KIBWETERE, hata akiwakojolea mdomoni utasikia huyo ni SIMBAAAAAA

Yale yale ya mashabiki wa KIBA hata afanye UJINGA gani wanamwimbia huyo ni KING.

Binafsi naona Tanzania ina viraia ambavyo viko easily controlled and radicalised

Ni rahisi tu mtu kujitengenezea kikundi cha watu wa kukuabudu. No wonder hata Nabii Tito alikuwa na wafuasi.

Muziki wa Tanzania hauwezi kukua kwasababu MEDIA HOUSES, RECORD LABELS, WASANII na PROMOTERS siyo watu HURU.

MEDIA inamiliki wasanii na ndio inayoandaa SHOW, so kama wewe hutumiki na media hiyo HUPATI SHOW na kama hutumiki na media hiyo basi hawana FAIDA na wewe na hivyo hata nyimbo zako HAWAPIGI.

Jambo la msingi HARMONIZE kujitoa WCB ajue kabisa alianzisha VITA maana pesa aliyokuwa anawaingizia ni kubwa na ndio maana pamoja na kujipendekeza kote bado wana CHUKI naye TENA KUBWA tu.
 
ze keke

Afanye mziki wake aache majungu,kaanza Hainishtui watu kimya,kaja Hujanikomoa WCB wamekaa kimya ,sababu wameona ujumbe umekaa kimafumbo labda hauwahusu wao.

Juzi tena kapost video kuna kiemoro kinakunywa,huku kinacheza nyimbo yake ya hainishtui,kakifananisha na meneja wake wa zamani ambaye anapenda bata (Sallam ) naona wenzake nao wamereact,sasa hivi anatafuta huruma.

Yy afanye mziki wake kama ameamua kumove on,akina Kiss Daniel,Lil Kesh,Tiwa Savage,Wizkid wametoka kwenye label zao za zamani lakini hawana madongo wala mafumbo kutoka kwenye label zao zilizo watoa na kuwasaidia.

Nigeria hamna mziki wa kuachiana nafasi haupo,ila wenzetu wanabebana sana,Burna boy kaachia nyimbo imehit kuliko wenzake,lkn mwaka jana Wizkid kaachia nyimbo,Olamide kaachia nyimbo,Davido kaachia nyimbo,Naira Marley,Zlatan,Patoranking,Simi,Adenkule gold,Rekardo Bank,Joeboy,Fireboy wote wameachia nyimbo.

Na kwa mwaka jana msanii alifanya vizuri Nigeria ni Naira Marley,akifuatiwa na Zlatan.Burnaboy alifanya vizuri 2018 na ndio maana mwaka jana alikusanya tuzo nyingi sana.
 
Asilimia kama 70 za media kubwa Tz hazipigi muziki wa Wcb, wasanii waliobaki music wao unachezwa na media zote, sasa unaanzaje kulialia kuwa Wcb wanasababisha msanii fulani asisogee!!

Visingizio vya kitoto sana hivi, wakati Diamond media kubwakubwa zilipogoma kucheza muziki wake mbona aliendelea na harakati zake!?
Kulialia hakuwezi kukusaidia kitu katika kusaka mafanikio yako! Pambana!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nmefatilia kwa undani mikiki anayopitia kondeboy toka ajiengue WCB.. Kiukweli hajashuka Kama tunavyolazimishwa tuamini. Kwanza official songs katoa UNO na KUSHOTO KULIA, na zote zimefanya vyema you tube. Hainshtui na Hjanikomoa ni bonus track wakati anajiandaa kuachia album Yake. Inashangaza sana kuwa nchi yenye watu million 50 tunataka msanii awe DIAMONDPLATINUM TU. wenzetu Nigeria international artist ni wengi kwa sababu wanaachiana nafasi. Huku tz tunapambana kusushana yaani mpaka media za YouTube hazipost show za harmonize ili tu akose mvutoo. Wenzetu wamefanikiwa kwa kuachiana nafasi...SASa hivi wamemwachia nafasi BURNABO.Hata hapa watu watakavyojibu ni kwa kumkatisha tamaa kondeboy.
Duh duh!!! ama kweli tuna watu!!! sasa waachiane zamu au kila mtu anatakiwa apigane kubaki juu!! kwani wakongo man walikuwa wanaachiana zamu!!! zamu unataka ipangwe na nani! kwahiyo MC NICE ,FERUZI wamebaniwa au wametolewa kwenye zamu......mawzo yako bwana
 
Back
Top Bottom