Ugumu wa maisha ni jambo la kusadikika halipo kiuhalisia na sijawahi kuliona na halitatokea

Nani kakwambia nina maisha magumu?

Wewe huwezi hata kufanya fikra dhahania.

Unafikiri mimi kukupinga wewe ni kwa sababu nina maisha magumu.

Huelewi kuwa ninaweza kuwa na maisha mazuri kuliko wewe, na bado nikakupinga.

Juzi nimefanya muamala mmoja tu wa $50,000.

Maisha magumu gani unayoyaongelea kwangu mimi?
Sasa unapinga nini! Unamtetea nani aliyekwambia ana maisha magumu! Umetambua wajibu wake kwenye hayo maisha yake!?
Nyuma ya maisha kuna uzembe wa kutumia mazingira!
Na wazembe wote ndo hao walibuni huo msemo wa maisha magumu!

Maisha magumu huwa wanayalinganisha na ya nani?

Kama ni ishu ya kulinganisha basi hata ukiwa Rais ukikutana na maRAIS wenzio utasema una maisha magumu!

Neno maisha magumu ni kichaka cha kujificha wajinga wengi
 
Shida siyo kuzaliwa kwenye familia maskini, shida nikutumia mazingira ulipozaliwa kutoka kwenye umaskini!
Mtu akizaliwa kiwete, Tena azaliwe kwenye familia ya kimaskini isiyo jiweza kwa lolote,

Je atatumiaje hayo mazingira, yamtoe kwenye umaskini pasipo kuhitaji msaada wa watu wengine?
Kama wewe ni mjinga wa kutumia mazingira hata ukizaliwa na matajiri wakafa utauza vyote urudi kuwa maskini!
Mazingira ni nini?
Hoja iliyopo hapa ni namna ya kutatumia mazingira kuishi!
Ungezaliwa kiwete huna mikono wala miguu, Ungetumiaje hayo mazingira yakusaidie?

Pasipo kuhitaji msaada wa mtu yeyote yule. Yani utumie tu hayo "mazingira" ufanikiwe kuishi.

Hebu eleza hapa.
 
Sasa unapinga nini! Unamtetea nani aliyekwambia ana maisha magumu! Umetambua wajibu wake kwenye hayo maisha yake!?
Nyuma ya maisha kuna uzembe wa kutumia mazingira!
Na wazembe wote ndo hao walibuni huo msemo wa maisha magumu!

Maisha magumu huwa wanayalinganisha na ya nani?

Kama ni ishu ya kulinganisha basi hata ukiwa Rais ukikutana na maRAIS wenzio utasema una maisha magumu!

Neno maisha magumu ni kichaka cha kujificha wajinga wengi
Unaweza kuongelea hoja kama hoja bila ya kui personalize?

Unaweza kufafanya fikra dhahania, abstract thought?
 
Naomba nikuulize Wewe hapo unaweza kuthibitisha hapa maisha yako magumu unayapimaje?
Hahaha! Naona unakwepa maswali yangu. Lakini haijalishi. Mimi nitajibu yako na wewe utajibu yangu.

Maisha magumu hayana vipimo, ni hali ya mtu kushindwa kukidhi mahitaji muhimu ya binadamu yoyote wa kawaida mwenye akili timamu ili kuishi kwenye jamii husika. hakuna SI unit au universal scale ya kupimia ugumu wa maisha wa kila mtu na kila kiumbe. Je, hilo jibu ni adequate enough au nitoe na mifano?

Sasa ni zamu yako kujibu maswali yangu.
Unajuaje unachokiamini wewe ni uhalisia? Na uhalisia ni nini au una maana gani kwako?
 
Mtu akizaliwa kiwete, Tena azaliwe kwenye familia ya kimaskini isiyo jiweza kwa lolote,

Je atatumiaje hayo mazingira, yamtoe kwenye umaskini pasipo kuhitaji msaada wa watu wengine?

Mazingira ni nini?

Ungezaliwa kiwete huna mikono wala miguu, Ungetumiaje hayo mazingira yakusaidie?

Pasipo kuhitaji msaada wa mtu yeyote yule. Yani utumie tu hayo "mazingira" ufanikiwe kuishi.

Hebu eleza hapa.
Kwahiyo viwete wote ni maskini ndo unachosema!
Kuna nyoka anaitwa chatu hana mwendo lakini kapewa uwezo wa kukamata kulingana na mazingira!
Hao walemavu wana kazi zao, wana magari yao, wana baiskeli zao!

Kuna walemavu wametusua kibao kwa jitihada ..wee unaekazana kulalamika maisha magumu na viungo vyote unavyo, huoni kwamba ulemavu upo akilini na siyo mwilini?
 
Hahaha! Naona unakwepa maswali yangu. Lakini haijalishi. Mimi nitajibu yako na wewe utajibu yangu.

Maisha magumu hayana vipimo, ni hali ya mtu kushindwa kukidhi mahitaji muhimu ya binadamu yoyote wa kawaida mwenye akili timamu ili kuishi kwenye jamii husika. hakuna SI unit au universal scale ya kupimia ugumu wa maisha wa kila mtu na kila kiumbe. Je, hilo jibu ni adequate enough au nitoe na mifano?

Sasa ni zamu yako kujibu maswali yangu.
Unajuaje unachokiamini wewe ni uhalisia? Na uhalisia ni nini au una maana gani kwako?
Sasa ushajijibu hapo juu kwamba HAYANA KIPIMO! maana yake siyo halisi! Ni ya kufikirika! Sasa hapo ndugu unataka nini tena!
 
Kwahiyo viwete wote ni maskini ndo unachosema!
Acha kupindisha na kukwepa maswali.

Nakuuliza hivi, Kiwete aliyezaliwa kwenye familia ya kimaskini isiyo jiweza kwa lolote, Atatumiaje hayo mazingira yamsaidie pasipo kuhitaji msaada wa mtu yeyote yule?
Kuna nyoka anaitwa chatu hana mwendo lakini kapewa uwezo wa kukamata kulingana na mazingira!
Hao walemavu wana kazi zao, wana magari yao, wana baiskeli zao!
Kwa hiyo kila kiwete duniani ana kazi?

Kila kiwete duniani ana gari lake?

Kila kiwete duniani ana baiskeli yake?

Hivi wewe unafikiri sawasawa kweli?
Kuna walemavu wametusua kibao kwa jitihada ..wee unaekazana kulalamika maisha magumu na viuongo vyote ndiyo mlemavu
Wapi nimekazana kulalamika maisha magumu?

Unajua wewe ni Tabularasa Mpumbavu.

Hujibu ulicho ulizwa, Unajibu usivyo ulizwa.

Nakuuliza hivi,

Mtu maskini anayezaliwa bila mikono wala miguu, Au mtu kipofu atatumia jitihada gani pasipo kuhitaji msaada wa mtu mwingine yeyote yule kujitafutia maisha katika mazingira?

Atatumiaje hayo mazingira yamtoe kwenye umaskini pasipo kuhitaji msaada wa mtu mwingine yeyote yule?
 
Sasa ushajijibu hapo juu kwamba HAYANA KIPIMO! maana yake siyo halisi! Ni ya kufikirika! Sasa hapo ndugu unataka nini tena!
Good!

Huo ni uhalisia wako wewe. Kukosa kipimo hakuondoi uhalisia wa kitu. Ni kama unavyofanya wewe sasa hivi.

Sasa niambie ni unajuaje huo "uhalisia" wako ni sahihi? Na kwako uhalisia ni nini au una maana gani?

Jibu maswali yangu ili tuwe na intelligent debate as gentlemen.
 
Acha kupindisha na kukwepa maswali.

Nakuuliza hivi, Kiwete aliyezaliwa kwenye familia ya kimaskini isiyo jiweza kwa lolote, Atatumiaje hayo mazingira yamsaidie pasipo kuhitaji msaada wa mtu yeyote yule?

Kwa hiyo kila kiwete duniani ana kazi?

Kila kiwete duniani ana gari lake?

Kila kiwete duniani ana baiskeli yake?

Hivi wewe unafikiri sawasawa kweli?

Wapi nimekazana kulalamika maisha magumu?

Unajua wewe ni Tabularasa Mpumbavu.

Hujibu ulicho ulizwa, Unajibu usivyo ulizwa.

Nakuuliza hivi,

Mtu maskini anayezaliwa bila mikono wala miguu, Au mtu kipofu atatumia jitihada gani pasipo kuhitaji msaada wa mtu mwingine yeyote yule kujitafutia maisha katika mazingira?

Atatumiaje hayo mazingira yamtoe kwenye umaskini pasipo kuhitaji msaada wa mtu mwingine yeyote yule?
Yaani shida iko kwako! Nimekwambia wengi wanaolalamika maisha ni magumu ni kutokana na kushindwa kutumia mazingira walipo!

Sasa unataka nitoe elimu kila ulemavu na njia hapa! Hakuna njia moja ya mafanikio inategemea huyo kipofu yuko mazingira gani!

Baadhi ya ulemavu ni afya na zingine ni laana huwez tatua njia moja
 
Kinamna fulani nakubaliana na mleta uzi, siku zote hard work na uaminifu vinalipa, hata wahuni wakishajua mwana mchapa kazi na mwaminifu watakuletea deal tuu, na ndio namna ya kujenga mazingira mazuri
 
Yaani shida iko kwako! Nimekwambia wengi wanaolalamika maisha ni magumu ni kutokana na kushindwa kutumia mazingira walipo!

Sasa unataka nitoe elimu kila ulemavu na njia hapa! Hakuna njia moja ya mafanikio inategemea huyo kipofu yuko mazingira gani!

Baadhi ya ulemavu ni afya na zingine ni laana huwez tatua njia moja
Je hao vipofu hawatakuwa na maisha magumu?

Je hao vipofu walitaka wawe vipofu wawe na maisha magumu

Je hao vipofu watatumiaje hayo mazingira yawasaide ili wasiwe na maisha magumu?

Pasipo kuhitaji msaada wa mtu mwingine yeyote yule.
 
Back
Top Bottom