Ntele Bhn
New Member
- Dec 26, 2017
- 4
- 11
Dar es Salaam, jiji kubwa na kitovu cha uchumi wa Tanzania, limeendelea kukumbwa na uhaba mkubwa wa maji safi na salama kwa matumizi ya binadamu
Jana nimemsikia Waziri Mkuu Mwigulu Nchemba akiwa mto ruvu anadai tatizo la maji ni tatizo la kidunia.Pia Waziri wa Maji kwa Nyakati tofautitofauti amekua akidai mabadiliko ya tabia ya nchi ndio chanzo cha uhaba wa maji.
Changamoto hii ya maji imekuwa ya kudumu kiasi cha kuzoeleka, jambo linaloibua maswali mazito kuhusu ufanisi wa uongozi na usimamizi wa sekta ya maji.
Kitaalamu upatikanaji wa maji hupimwa kwa vigezo kama idadi na ukubwa wa vyanzo vya maji, renewable water resources,uwepo wa mito,maziwa na maji ya chini ya ardhi
Hali hii inashangaza ukizingatia Tanzania imebarikiwa kuwa na vyanzo vingi vya maji ikiwemo Bonde la mto Ruvu, Ziwa Victoria, Ziwa Tanganyika, Ziwa Nyasa.
Dar es Salaam ina rasilimali nyingi za maji kuliko majiji kama Kigali, Windhoek na Dakar.
Kwa kiwango cha hydrology, Senegal ina water stress kubwa kuliko Tanzania iliyopo ukanda wa sahel lakini Jiji la Dakar limepiga hatua kubwa kwa kuwekeza katika usambazaji wa maji kutoka Ziwa Lac de Guiers kwa mipango ya muda mrefu na uwazi wa usimamizi.
Windhoek Namibia mji wenye maji machache zaidi duniani, ukame na mvua chini ya 300mm kwa mwaka lakini upatikanaji wa maji ni bora zaidi kuliko Dar es Salaam kwa kutumia teknolojia ya direct potable water reuse.
Rwanda haina maziwa wala mito mikubwa kama Tanzania lakini imefanikiwa kuboresha upatikanaji wa maji mjini Kigali kupitia usimamizi thabiti wa vyanzo vya mito kama Nyabarongo na uwekezaji katika miundombinu na kupunguza upotevu wa maji.
Kitaalamu Tanzania ipo kwenye kundi la nchi zenye utajiri wa maji (water abundance) lakini Jiji kubwa la Dsm maji yamekua mtego wa umaskini.Hii inaonyesha wazi kuwa tatizo sio maji, bali ni kukosa uongozi wenye kujali maisha ya watu.
Kwa akili ya kawaida nchi yenye vyanzo vingi vya maji haiwezi kushindwa kuhudumia wananchi wake kwa huduma ya msingi kama maji isipokuwa pale kunapokuwepo na sera dhaifu, mipango mibovu na uongozi usiojali maslahi ya watu.
Bonde la Mto Ruvu, ambalo kwa miongo mingi limekuwa chanzo kikuu cha maji kwa Dar es Salaam, halijawekewa uwekezaji unaolingana na ongezeko kubwa la watu na shughuli za kiuchumi.
Miundombinu yake ni chakavu, upotevu wa maji ni mkubwa, na mipango ya vyanzo vipya imekuwa ikichelewa au kutekelezwa bila ufanisi.
Wakati wananchi wakikosa maji, Serikali imeonekana kuelekeza rasilimali katika matumizi ya anasa na mambo yasiyo na msingi wa moja kwa moja kwa maisha ya watu.
Misafara mikubwa ya viongozi wakizurura kwa madai ya kwenda kusikiliza kero za wananchi, hafla za kifahari, miradi ya mapambo na matumizi makubwa ya posho za vikao, kalmati na bagia huku kukikosekana vyanzo mbadala vya maji, vituo vya kusafisha maji vikifanya kazi chini ya uwezo, na maeneo mengi ya jiji yakitegemea maji ya ratiba.
Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) matumizi ya maji kwa mtu mmoja ni kati ya lita 150 - 300, hivyo Wananchi wa Dar es Salaam wanaendelea kuteseka wakinunua haki yao kwa wastani wa 20,000 kwa siku.
Kitendo cha wananchi kununua maji badala ya kuchangia gharama kidogo za uendeshaji ni ushahidi wa wazi wa serikali isiyotoa kipaumbele kwenye maisha ya watu.
Katika hali isiyokua ya kawaida Waziri wa Maji anaonekana akizurura na misafara mirefu kupiga picha na kufanya maigizo kwa ajili ya kuhadaa umma huku changamoto halisi za maji zikibaki palepale.
Maigizo ya kisiasa hayawezi kuchukua nafasi ya mipango ya kitaalamu, utafiti wa kina, uwekezaji wa kimkakati na uwajibikaji wa kweli. Katika karne ya 21, Tanzania kukosekana kwa maji safi na salama ni kituko cha karne.
Kama tungekua na serikali makini inayojali maisha ya watu, Waziri wa maji ilipaswa apumzishwe nyumbani na wizara kufumuliwa na kujengwa upya maana wanakula kodi za Watanzania bila aibu.
Baada ya zaidi ya miaka 60 ya uhuru, ni jambo la kusikitisha na la kuaibisha kuona Mtanzania bado anategemea kuchota maji kwenye mabonde, akitumia madumu na ndoo, na kusimama foleni ndefu kwa ajili ya maji.
Kupata maji kwa ratiba katika jiji kubwa kama Dar es Salaam ni aibu ya dunia na kielelezo cha kushindwa kwa uongozi kutekeleza wajibu wake wa msingi kwa wananchi.
Uhaba wa maji Dar es Salaam si tatizo la kijiografia wala la kiasili au mabadiliko ya tabia ya nchi kama inavyodaiwa bali ni zao la uongozi usio na maono, sera dhaifu, kutojali maisha ya wananchi na ukosefu wa uwajibikaji.
Tanzania ina rasilimali zote za kutosha kumaliza tatizo la maji kabisa. Kinachokosekana ni uamuzi wa dhati wa kisera na uongozi unaoweka maslahi ya wananchi mbele.
Uhaba wa maji Dar es Salaam si tatizo la kiasili (natural scarcity), ni tatizo la kiutalawa (governance failure)
Endeleeni kunywa amani,Mabeberu wamekausha maji Dar es Salaam.
Ntele
Katibu Chadema Kanda ya Pwani