Uhai wa Taifa Letu unategemea Uwepo wa CCM Madarakani Muda Wote.

Uhai wa Taifa Letu unategemea Uwepo wa CCM Madarakani Muda Wote.

Lucas Mwashambwa

JF-Expert Member
Joined
Jul 28, 2022
Posts
28,722
Reaction score
20,610
Ndugu zangu Watanzania,

Ni lazima ifike wakati tukubaliane na ukweli mchungu ya kuwa CCM ndio Moyo wa Taifa letu,ndio Mapafu ya Taifa ,ndio damu ya Taifa na ndio OKSIJENI ya Taifa letu. Hakuna amani wala utulivu wala umoja wala mshikamano wala masikilizano wala upendo wala kuzungumza lugha moja pasipo uwepo wa CCM Madarakani.

Pasipo CCM hakuna amani wala utulivu ,hakuna mipango wala Dira kwa Taifa letu,hakuna kesho iliyo njema na yenye matumaini pasipo uwepo wa CCM Madarakani. Ni CCM pekee yenye uwezo wa kuliongoza na kulivusha Taifa letu katika nyakati ngumu,ni CCM pekee yenye uwezo wa kuwaunganisha watanzania wa Dini zote,rangi zote,jinsia zote,makabila yote na wa kanda zote.ni CCM pekee yenye uwezo wa kuwaletea pamoja watu wa rika zote.

Ndio maana ndani ya CCM na serikali yake utawakuta viongozi kutoka Dini zote, makabila yote,rika zote,makundi yote,jinsia zote na wenye kila aina ya Elimu. Kila mmoja ndani ya CCM anayo nafasi sawa na mwanachama mwingine.Ndio maana unaweza kuwa kiongozi ndani ya CCM hata kama wazazi wako hawakuwa viongozi.kwa sababu kinachoangaliwa ndani ya CCM ni uwezo wa mtu kiuongozi,sifa na uwezo wa kumudu majukumu na kukubalika kwa watu.

Ni CCM pekee yenye uchungu na Maisha ya watanzania na Taifa letu kwa ujumla wake. Ni CCM pekee yenye uwezo wa kumsikiliza kila mtu,kupokea maoni na mawazo ya kila mtu, kumvumilia kila mtu pasipo kumbagua mtu. Ndio maana wapo wengine ndani ya CCM unaweza kuhisi ni wapinzani au watahamia upinzani kesho ,lakini huwezi ukaona wakifukuzwa chamani.

Ni CCM pekee yenye kujiendesha kitaasisi .tofauti na vyama vingine kama CHADEMA. ambavyo vimewekwa mifukoni mwa mtu mmoja tu aliyeamua kujimilikisha chama Utafikiri kitega uchumi cha Familia .na kwamba ni yeye tu mwenye akili kuliko wanachama wengine wote na kwamba wengine hawana akili na ni mambumbumbu wa uongozi na hawana haki ya kuongoza chama.

Embu jaribu kuangalia Ingetokea CHADEMA ipo madarakani? Unafikiri nini kingetokea? Kwanza wangewagawa sana watanzania na kuwabagua.ndio sababu ya sera yao ya Majimbo,pili wangeleta ukabila sana hapa nchini nakuona makabila fulani kutoka ukanda fulani ni bora zaidi na yenye kupaswa kupewa nafasi za juu za uongozi. na kwamba makabila mengine kutoka kanda zingine ni washamba tu wanaopaswa kuongozwa na kuamuliwa kwa kila kitu.

Wangekuwa wamelipasua na kulisambaratisha kabisa Taifa. Kusingekuwa na habari za Muungano wala Umoja wa kitaifa. Ni muhimu sana watanzania kuendelea Kuiweka CCM madarakani na kuendelea kuiamini .kwa sababu imekuwa na usikivu, unyenyekevu na kujali Maisha ya watu pamoja na kutanguliza mbele masilahi ya Taifa letu na ustawi wa wananchi.

Kazi iendelee, Mama Ametufikia na kuwafikia watanzania kwa utumishi wake uliotukuka wa kugusa maisha ya watanzania wanyonge wasio na Sauti.

Lucas Hebel Mwashambwa, Mama ANATOSHA kuendelea kuliongoza Taifa letu kwa muhula wa pili.
 
Taifa linamtegemea Mungu wa Mbinguni we Simbilisi 😄
Mungu Hutumia watu wake kuongoza waja wake kwa kuwainua na kuwapatia kibali..Ndio maana Mungu amekuwa akituinulia watu sahihi na chama sahihi cha CCM kuliongoza Taifa letu. Mungu hajawahi kutuacha wala kutupungukia. Kama alivyowainulia Musa Na Yoshua wana islaeli.ndivyo alivyotuinulia CCM na kuipatia Kibali.
 
Tanganyika na Tanzania zilikuwepo kabla ya CCM na zitaendelea kuwepo after CCM. Wewe unaipa CCM umuhimu ambao haina chief.
Kwa vile yeye ni PS wa UWT Wilaya CCM inamlipa mshahara anaona kila mtu anaitegemea CCM badala ya MUNGU, jitu jinga haswa. CCM ni kusanyiko la takataka
 
Mungu Hutumia watu wake kuongoza waja wake..Ndio maana Mungu amekuwa akituinulia watu sahihi na chama sahihi cha CCM kuliongoza Taifa letu. Mungu hajawahi kutuacha wala kutupungukia. Kama alivyowainulia Musa Na Yoshua wana islaeli.ndivyo alivyotuinulia CCM
Shetani usie na aibu, labda biblia ya UWT
 
Tanganyika na Tanzania zilikuwepo kabla ya CCM na zitaendelea kuwepo after CCM. Wewe unaipa CCM umuhimu ambao haina chief.
Angalia CCM imetokea wapi ndugu yangu.unafahamu ya kuwa CCM ndio TANU na Ndio ASP? CCM ndio Tanzania na Tanzania ndio CCM.huwezi kuvitenganisha.
 
Mungu Hutumia watu wake kuongoza waja wake..Ndio maana Mungu amekuwa akituinulia watu sahihi na chama sahihi cha CCM kuliongoza Taifa letu. Mungu hajawahi kutuacha wala kutupungukia. Kama alivyowainulia Musa Na Yoshua wana islaeli.ndivyo alivyotuinulia CCM
Yoiongea na Mungu akasema Amewatuma CCM?
 
Back
Top Bottom