Uhalisia wa taifa la Israeli

Uhalisia wa taifa la Israeli

Haikupeliki Mbinguni kujua nani fake na nani original na pia kuibariki wala kuto kuibariki haikupeleki mbinguni isipokuwa ni miongoni mwa hatua za kukujenga katika safari ya mbinguni ipo hv, Hosea 4:6 inasema "watu wangu wanaangamia kwa kukosa maarifa", Yohana 8:32 "wataijua kweli na kweli itawaweka huru" hivi sasa wakristo weengi sana wamekuwa watumwa wa hili taifa la israel siwalaumu bado hawajaijua kweli siku wakijua watakuwa huru kutokana na hilo taifa wanaloshinda kila siku kuliombea,kulisaidia nk wengine wamebandika hadi mabendera ya israel kwenye magari yao ni utumwa tu wakuto kujua maandiko na ukijua sio ndio tiketi ya kuingia mbinguni hapana na sio kila andiko unalolijua litakuingiza mbinguni hapana ila linakusaidia kukujenga kiroho,kiimani na kimwili pia! Njia ni moja tu yakukuingiza mbinguni nayo ni kumfuata Yesu kristo
Kweli kabisaaa mkuu hayo mengine ni kujilisha upepo!!
 
1.Huwezi kumjua Mungu na Yesu Bila kujijua wewe mwenyewe bwana John Q upoje! kwasababu Biblia imesema wazi Mwanzo 1:26,Mungu alikuwa anasemezana na kitu kingine na kukubaliana "na TUMFANYE mtu kwa mfano Wetu"! angekuwa pekeyake asingesema "Tumfanye" angesema "nifanye" hapo katumia wingi na sio umoja! sasa kujua Mungu alikuwa anasema na nani inatakiwa tumjue huyo mtu aliyeumbwa na Mungu kwa mfano wake ndio tutapata picha ya huyo aliyekuwa anasema naye hapo awali namna ya kumuumba mtu kwa mfano wao!
Namna Mtu alivyo, hapa nitatumia mfano wako mwenyewe, Wewe kama John i mean mtu John upo katika sehem tatu,Una Roho (binadamu woote wana Roho),una Mwili na pia una Nafsi soma Warumi 8:23 Na 2 Wakorintho 7:1, sasa Roho Hukaa ndani ya Nafsi (matendo 20:28,waebrania 4:12) na kwapamoja nafsi na roho hukaa ndani ya mwili ndio unakuwa wewe bwana John-Q,sasa wewe John Q una vitu vitatu una mwili ndio huo unao uona na ndani yako una roho na nafsi na ukitizama kwa makini huwa wakati mwingine mnabishana na hivyo viwili vilivyopo ndani yako,mwili wako unaweza ukawa unatamani kufanya jambo fulani lakini roho haipo tayari! au kinyume chake,mwili ni dhaifu siku zoote lakini sio roho (soma Mathayo 26:41) sasa tunaposema mtu kafariki ni pale Nafsi na roho vinauacha Mwili vinatengana ule mwili unabaki pekeyake hapa Duniani ukirudi mavumbini roho ndio inatangulia huko mbele kwenda kwenye hukumu,ndiomaana Biblia inasema tusijitaabishe na vya mwilini! mwisho wa siku tutaviacha!
Kwahiyo binadamu aliyeumbwa kwa mfano wa Mungu ana hivyo vitu vitatu Roho,Nafsi na Mwili so na Mungu naye pia ana hivyo Vitu vitatu!
1.Mungu ana "NAFSI" (Mwanzo 22:16,1Samweli 2:27),ndio Mungu Baba huyo
2.Mungu ana "ROHO" ndio Roho mtakatifu,Roho wa Bwana (Mwanzo 6:3,waamuzi 3:10 Hapa kuna maandiko Mengi sana yanayo elezea Roho wa Mungu)
3.Mungu ana MWILI,hapa ndipo penye utata! mwili wa Mungu ndio Yesu kristo!,Biblia imesema wazi kabisa kabla Mungu hajaumba chochote kile aliuumba mwili wake,alimuumba Yesu kristo ,Wakolosai 1:15-16 "Ni mzaliwa wa kwanza wa viumbe vyoooote" ndiomaana Mungu alimwita Yesu kama Mwanawe wa pekee "Yohana 3:16",Yesu alikuwepo tangia zamani(Yohana 8:58),Yesu ni Mungu katika mwili "1Timotheo 3:16!,Yesu ni Mungu kati yetu "Mathayo 1:23,Yesu ni Neno na neno ni Mungu!,Yohana 1:1-3,Mwanzo 1:1,Yesu alimtokea Ibrahimu wakati Mungu anataka kuangamiza Sodoma na Gomora "Mwanzo 18,Yohana 8:56,Yesu alionekana pamoja na Shadraka,Abednego na Meshaki katika tanuru la Moto" Daniel 3:23-25, kuna vifungu viingi vinavyoongelea U-Mungu wa Yesu ni wewe mwenyewe kusoma na kuamini katika biblia.

2.Jibu la swali lako la pili.,
Wakristo wengi wamekuwa kama Nyumbu hawasomi maandiko na kuyachunguza wanapokea kile wanachoambiwa na wachungaji wao kama kilivyo,kumbuka sio kila wachungaji unaowasikia na kuwaona ni watumishi wa Mungu,wachungaji wengi sana sikuhz ni mapandikizi ya shetani wanapewa na kuambiwa cha kufanya na kuhubiri kutoka chini,mithali 14:15 "mjinga huamini kila neno bali mwerevu hayachunguza" sio kila unaloambiwa kanisani lipo sawa nenda kalichunguze kabla ya kuliamini tunaishi nyakati za mwisho hizi Uongo ni mwingi makanisani,

3.Jibu la swali lako la tatu
Lengo la kuja Yesu ni kuikomboa dunia yoote kutoka kwenye utumwa wa dhambi na sio wayahudi tu,na ukisoma kabla ya kuja Yesu ilikuwa ni kuhusu taifa moja tu la israel na sio mengine ilikuwa ukombozi kwa wana wa israeli tuna sio wana wa mataifa yoote,mafundisho ya agano la kale kipindi kile yalikuwa kwa ajili ya wale wana wa israel na mafundisho ya agano jupya baada ya yesu kuja plus na yale ya agano la kale ni kwaajili ya kila mtu kujifunza ndiomaana Yesu aliwaagiza wanafunzi waki wakaihubiri injili mataifa Yooote na sio wayahudi tu! maagano yoote la kale na jipya yoote ni neno la Mungu lile lile linafaa kwa mafundisho,yesu alisema hakuja kuitengua torati bali kuitimiliza Mathayo 5:17
Samahani mtoa mada naomba kuuliza according to your explanation hapo kuhusu yesu alikua mungu so unamaana kuna miungu wa tatu na hiyo point ya mwisho mchangiaji aliuliza walikua dini gani hao manabii waliopita na kwanini yesu afuate mafundisho yao wakati yeye ni mungu
 
Mengine umeandika vizuri lakini kusema kwamba waMisri ni weusi nimeshindwa kukuelewa. Unaweza kuwa na point lkn ukiandika kiushabiki na umbumbumbu taarifa inakosa maana na hatima yake ni kukataliwa. Unataka niwaonee huruma wapalestina!!! nitafaidika nini? si heri niwatambue wayahudi hata kama sio sahihi maana angalau kuna maendeleo naweza faidika kuliko kuhubiri ugaidi wakati wote.
Mkuu misri ni nchi ya black siyo hawa waarabu wa leo. Ni like Amerika haikuwa ardhi ya wazungu
 
Kwahiyo wale wayahudi wote siyo halisi? Halisi ni wapi sasa na wako utumwani nchi gani? Vipi kuhusu wale ethiopian Jews waliorudishwa Israel mwaka 1991, je na wao siyo halisi? lakini pia vipi kuhusu wale aliowaua Adolf Hitler kule Ujerumani wakati wa WW2 hawakuwa halisi? duuh! Kumbe Adolf Hitler aliua wayahudi fake? Nauliza tu!
tatizo sio kusoma tu!bali kuna tofauti pia ya kuelewa jambo!
 
Samahani mtoa mada naomba kuuliza according to your explanation hapo kuhusu yesu alikua mungu so unamaana kuna miungu wa tatu na hiyo point ya mwisho mchangiaji aliuliza walikua dini gani hao manabii waliopita na kwanini yesu afuate mafundisho yao wakati yeye ni mungu
jibu la swali la kwanza kuhusu uungu wa Yesu

1.Kuna Mungu mmoja tu ambaye anamwili(Yesu),ana Roho(Roho Mtakatifu) na ana Nafsi(Mungu) kwa pamoja hivi vitatu vinafanya Mungu Mmoja na nimakosa kutenganisha au kusema
'Mungu BABA,Mungu Mwana Na Mungu roho mtakatifu'!
Hakuna kitu kama hicho kuna Mungu mmoja tu ambaye amejidhihirisha katika sehemu tatu hizo nimezitaja hapo juu
ukisoma 1Timotheo 3:16 inasema hivi
"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.Mungu alidhihirishwa katika MWILI,akajulikana kuwa na haki katika ROHO,akaonekana na malaika,akahubiriwa katika mataifa,akaaminiwa katika ulimwengu,akachukuliwa juu katika UTUKUFU"
Ukianza ku Break-Down(Kuuchambua) huo mstari utagundua amemzungumzia Yesu kuwa ni Mungu ambaye kajidhihirisha kwetu katika Mwili!,alishuka duniani katika mwili! yaani ni Mungu katika mwili,pia alionekana kuwa mwenye haki katika roho,na yupo juu katika utukufu!,YESU mwenyewe alisema "MIMI NA BABA TU WAMOJA" hakusema yeye ni Mungu mwana halafu kuna Mungu BABA!,Yohana 14:7 "kama mngalinijua mimi,mngalimjua baba,tangu sasa mnamjua,tena mmemwona" maana yake Yesu ni Mungu ila alijidhihirisha ktk mwili na walikuwa wanamuona wazi wazi na wasimtambue!!! (soma hizo comment zangu hapo juu nimeweka vifungu vingi sana vinavyoonyesha Uungu wa Yesu nikiweka hapa tena nitakuwa navirudia tu japo nimejitahidi kurudia vya muhimu)

2.Jibu la swali la pili ni hivi
Manabii woote waliopita (kabla na baada ya Yesu) hawakuwa na Dini tofauti(mwanzo walikuwa wanafuata dini ya kiyahudi,baadaye wakwa wanafuata dini yenye mafundisho ya Yesu) lakini walikuwa na imani katika Mungu mmoja wa Israeli,isaka na Yakobo na baadaye YESU kristo kupitia kanisa na sio miungu wengine,dini ni taratibu tu za kibinadamu tulizojiwekea hapa duniani kwa watu wenye misimamo inayofanana kuhusu jambo flani ndiomaana dini zikitofautiana kuhusu maswala ya msingi ya kiimani hutengana na ndiomaana tuna dini nyingi sana tangia enzi na enzi na dini haimpeleki mtu mbinguni bali matendo Yakobo 1.27 inaeleza dini gani safi
Yesu hakuwa anafuata mafundisho ya hao manabii wa zamani sababu hayo mafundisho yeye kama Mungu ndio aliyatoa kwao ili yafuatwe na sisi binadamu sio yeye,ndiomaana walikuwa wanamuona kama anavunja maandiko ya torati,akawaambia hakuja kuivunja torati bali kuitimiliza!!!! sababu yoote yalioandikwa na torati lazima yatimie ndio yeye sasa kaja kuyatimiliza ndiomaana unaona vitu vingi sana alikuja kuvitenda kinyume na torati hii ikiwemo SABATO,kuhubiria mataifa,kusamehe 7x70,ndoa ya mke mmoja,kuleta meza ya Bwana nk..... kiuhalisia sio rahisi Mungu kufuata mafundisho ya manabii ambayo yametoka kwake yeye mwenyewe, Kimsingi yale yaliyokuwa yanasemwa na manabii kabla ya Yesu kuja duniani yalikuwa yanatoka kwake mwenyewe kwa Mungu! so ni yakwake tu sio ya manabii

Sijaelewa kidogo mtoa mada kwa hiyo hao manabii waliopita wote walikua wanafuata dini ya kiyahudi ila wayahudi si watu au jumuiya ya watu kama tunavyosema wasukuma je walikua dini gani au dini yao haikua na jina ndiyo dini ya kiyahudi ambayo ndiyo waliomsulubu yesu??

Hiyo point ya pili hapo so mungu alishuka duniani akiwa amejivika mwili wa mtu ambae ndiyo yesu kuja kuikamilisha torati ila maandiko yanasema mungu hana mfano wake hakuna kitu chochote cha kukilinganisha na yeye hazai hali wala hanywi na yeye ndiyo mkuu sasa alivyosulubiwa msalabani dunia ilikua inajiongoza au kulika na mungu mwingine anaiongoza??

Haya mambo ya dini huwa yananifanya niwe berserk sielewi elewi naomba unieleweshe mkuu
 
Ok kwa haraka haraka
JIBU LA KWANZA
Dini ni nini?
>Dini ni mapokeo ya wanadamu,namna wanadamu walivyolipokea neno la Mungu then wakaanzisha dini(njia) yao namna ya kulitafsiri,kulitenda,kuliamini,kulitii neno la Mungu,
>Dini zinatofautiana ila neno la Mungu ni Moja halitofautiani kwa-mfano wakristo woote wanaamini Yesu alizaliwa na bikira mariam,akahubiri injili,akasulubiwa msalabani,akafa akazikwa,siku ya tatu akafufukana yuko hai mpaka leo ila tunakuja kutofautiana namna ya kutafsiri sasa injili ya Yesu,na wanafunzi wake ndio hapo Dini zinakuwa tofauti,kuna watu hawaamini kuwa Yesu ni Mungu (wanajiita wao wakristo),kuna dini haziamini katika Roho mtakatifu(wanajiita wao wakristo),kuna dini haziamini katika uponyaji(wanajiita wakristo),kuna dini zinashika sabato(wanajiita wakristo)so dini ni mapokeo tu ya wanadamu juu ya neno la mungu
“Mnaiacha amri ya Mungu, na kuyashika sana mapokeo ya wanadamu.” Marko 7:8.
sasa kabla ya Yesu kulikuwa na dini mbalimbali za Miungu mbalimbali lakini dini ya kweli ilikuwa dini iliyokuwa inafuata Torati na vitabu vya manabii na iliyokuwa inaamini katika Mungu wa israel,isaka na yakobo dini hii ndio ilikuwa inafuatwa na wana wa Israel na baadaye Wayahudi
Sasa unapochanganya ni jina wayahudi na dini,ukisema wayahudi unamaanisha taifa linaitwa Judea ambalo ndani yake kuna makabila mawili (Benjamini na Yuda) na mji wake mkuu ulikuwa unaitwa Yerusalemu (kumbuka mwanzo taifa la israeli lilikuwa na kabila 12,then kabila 10 zikaasi Mungu akazitupilia mbali,hizi kabila 10 zilizo asi zilianzisha taifa lao ambalo lilibaki na jina la Israel na mji wake mkuu ulikuwa Samaria,na hizo kabila 2 zilizo baki nimezitaja hapo juu zilianzisha taifa lao lilikuwa linaitwa Yudea(Judea) na mji wake mkuu ulikuwa Yerusalemu! so hadi Yesu anakuja haya mataifa yalikuwa hivyo,utofauti nikuwa Taifa la Yedea(judea)Wayahudi waliendelea kushika maagizo ya MUNGU (TORATI na vitabu vya manabii na taifa la Samaria hawakuwa wanafuata hiyo misingi)
So unavyosema dini ya kiyahudi ni ile Dini ya lile taifa la Judea lililokuwa linafuata mafundisho ya Torati na vitabu vya manabii(AGANO LA KALE),na unaposema WAYAHUDI unamaanisha ni taifa ambalo lilimeguka kutoka katika taifa la israeli na ambalo ndani yake lilikuwa na makabila mawili YUDA na Benjamini kwapamoja walikuwa wanajiita WAYAHUDI na mji wao mkuu ulikuwa unaitwa Yerusalemu ya uyahudi
Wayahudi(dini ya kiyahudi) nikweli walimsulubisha Yesu msalabani,na Yesu alitoka katika kabila la YUDA miongoni mwa hizo kabila mbili zilizokuwa zinaunda hilo taifa la israel,sasa swala la kwanini walimsulubisha msalabani wakati alikuwa myahudi mwenzao na alikuwa ni Mungu,na alikuja kuwakomboa hao hao wayahudi nadhani unalijua

JIBU LA PILI
1Timotheo 3:16 inasema hivi ".............Mungu alidhihirishwa katika MWILI............."
So swala la yeye kuzaliwa kama wanadamu,bikira maria kupata mimba kwa uweza wa roho mtakatifu hizo ni fomality tu za kujidhihirisha katika mwili asinge shuka tu hivi hivi kutoka mbinguni sababu angefanya hivyo dunia yoote ingetawanyika hakuna kitu kingebaki kwasababu angeshuka na ule utukufu wake pasingetosha duniani(kumbuka kile kisa kipindi cha Musa wana wa israel walipoomba kuongea na Mungu ana kwa ana na sio kupitia Musa so akawaambia jitakaseni siku 7 then atashuka so wakati anaanza kujikusanya huko mbinguni kushuka kuja kuongea nao palitokea umeme,radi,ardhi inataka kukimbia milima inatawanyika,matetemeko na shoruba zoote unazoweza kuzitaja wana wa israeli wakamwambia basi asishuke awe anaongea na Musa tu then wao wataamini maneno yatakayotoka kwa Musa unaweza kusoma kutoka 20:19)
Sasa concept yake ilikuwa ni nini?
nikwamba Mungu ni msafi sana hakai sehemu ambayo ina dhambi na akiona dhambi mbele yake anaua so mtu yoyote anayekwenda mbele za Mungu anapaswa kujitakasa ndio ile dhana makuhani walipokuwa wanaingia hekaluni kwenye chumba cha patakatifu pa patakaifu kwenda kukutana na Mungu kutoa dhabinu walikuwa wanafungwa kamba Mguuni ili akiwa na dhambi akakutana na Mungu huko anakufa so kwakuwa hakuna wa kuingia kumtoa wanachofanya wanamvuta kupitia ile kamba sasa kama Mungu angeshuka mwenyewe kama alivyo kutoka mbinguni kuja pale Yerusalemu kuhubiri injiri hakuna ambaye angekaa so ilitakiwa aje kwa taratibu za kibinadamu aje kama ilivyotabiriwa na nabii isaya kuwa mwanamke bikira atachukua mimba na kumzaa Masihi wa Bwana ndiomaana Yesu alisema kaja kutimiza Torati na sio kuitengua(so alianza kutimiza kuanzia namna atakavyozaliwa hadi atakavyo hukumu ulimwengu),
Na kwakuwa Yesu alikuwa Mungu aliyejidhihirisha katika mwiliilibidi kabla ya kuja kwake wana wa israeli wawe safi,wajitakase asikute uchafu(dhambi)mwingi miongoni mwao otherwise angewafutilia mbali so Mungu akamtuma Yohana mbatizaji(ELIYA) kuja kuwabatiza wayahudi woote ndiomaana Yohana mbatizaji alisema yeye ni kama sauti ya aliye nyikani ananyoosha tu njia ya huyo mkubwa ajaye ambaye yeye hastahili hata kufungua kamba za kiatu chake! hapo alikuwa anazungumza habari za kuja Yesu kuwa yeye yohana anawasafisha tu watu (kuwatakasa) ili Mungu akija akute ni wasafi na hakuna uchafu (dhambi) ndani yao!!!
so alivyosulubiwa msalabani ule ni mwili tu ulikuwa pale lakini roho na nafsi yake bado vilikuwa mbinguni ndiomaana Yesu pale msalabani wakati anakaribia kukata Roho alisema "baba yangu baba yangu mbona umeniacha" inamaana Mungu bado alikuwa incontrol
 
jibu la swali la kwanza kuhusu uungu wa Yesu

1.Kuna Mungu mmoja tu ambaye anamwili(Yesu),ana Roho(Roho Mtakatifu) na ana Nafsi(Mungu) kwa pamoja hivi vitatu vinafanya Mungu Mmoja na nimakosa kutenganisha au kusema
'Mungu BABA,Mungu Mwana Na Mungu roho mtakatifu'!
Hakuna kitu kama hicho kuna Mungu mmoja tu ambaye amejidhihirisha katika sehemu tatu hizo nimezitaja hapo juu
ukisoma 1Timotheo 3:16 inasema hivi
"Na bila shaka siri ya utauwa ni kuu.Mungu alidhihirishwa katika MWILI,akajulikana kuwa na haki katika ROHO,akaonekana na malaika,akahubiriwa katika mataifa,akaaminiwa katika ulimwengu,akachukuliwa juu katika UTUKUFU"
Ukianza ku Break-Down(Kuuchambua) huo mstari utagundua amemzungumzia Yesu kuwa ni Mungu ambaye kajidhihirisha kwetu katika Mwili!,alishuka duniani katika mwili! yaani ni Mungu katika mwili,pia alionekana kuwa mwenye haki katika roho,na yupo juu katika utukufu!,YESU mwenyewe alisema "MIMI NA BABA TU WAMOJA" hakusema yeye ni Mungu mwana halafu kuna Mungu BABA!,Yohana 14:7 "kama mngalinijua mimi,mngalimjua baba,tangu sasa mnamjua,tena mmemwona" maana yake Yesu ni Mungu ila alijidhihirisha ktk mwili na walikuwa wanamuona wazi wazi na wasimtambue!!! (soma hizo comment zangu hapo juu nimeweka vifungu vingi sana vinavyoonyesha Uungu wa Yesu nikiweka hapa tena nitakuwa navirudia tu japo nimejitahidi kurudia vya muhimu)

2.Jibu la swali la pili ni hivi
Manabii woote waliopita (kabla na baada ya Yesu) hawakuwa na Dini tofauti(mwanzo walikuwa wanafuata dini ya kiyahudi,baadaye wakwa wanafuata dini yenye mafundisho ya Yesu) lakini walikuwa na imani katika Mungu mmoja wa Israeli,isaka na Yakobo na baadaye YESU kristo kupitia kanisa na sio miungu wengine,dini ni taratibu tu za kibinadamu tulizojiwekea hapa duniani kwa watu wenye misimamo inayofanana kuhusu jambo flani ndiomaana dini zikitofautiana kuhusu maswala ya msingi ya kiimani hutengana na ndiomaana tuna dini nyingi sana tangia enzi na enzi na dini haimpeleki mtu mbinguni bali matendo Yakobo 1.27 inaeleza dini gani safi
Yesu hakuwa anafuata mafundisho ya hao manabii wa zamani sababu hayo mafundisho yeye kama Mungu ndio aliyatoa kwao ili yafuatwe na sisi binadamu sio yeye,ndiomaana walikuwa wanamuona kama anavunja maandiko ya torati,akawaambia hakuja kuivunja torati bali kuitimiliza!!!! sababu yoote yalioandikwa na torati lazima yatimie ndio yeye sasa kaja kuyatimiliza ndiomaana unaona vitu vingi sana alikuja kuvitenda kinyume na torati hii ikiwemo SABATO,kuhubiria mataifa,kusamehe 7x70,ndoa ya mke mmoja,kuleta meza ya Bwana nk..... kiuhalisia sio rahisi Mungu kufuata mafundisho ya manabii ambayo yametoka kwake yeye mwenyewe, Kimsingi yale yaliyokuwa yanasemwa na manabii kabla ya Yesu kuja duniani yalikuwa yanatoka kwake mwenyewe kwa Mungu! so ni yakwake tu sio ya manabii

Matango pori, biblia moja ila tafsiri zinzotolewaga ni pasua kichwa kabla ya yesu kusulubiwa alisali mlimani kwenye mizeituni akalia kwa michozi ya damu na alikua anamuomba Mungu amuepushe ni kikombe cha mateso maana aliona mbele yake kuna nini kitafuata, na hata msalabani pia alisema eloi eloi Mungu wangu mbona umeniacha, swali kama yeye ni Mungu, huyo Mungu alokua anamuomba ni yupi?
 
Nilivyosoma tu ulivyoandika "Yesu alimuomba Mungu mlimani" na "akalia msalabani Mungu wangu Mungu wangu mbona umeniacha" nikajua tu wewe bado sana kuhusu maandiko na unasoma Biblia "LITERALLY" Unasoma kama Gazeti hv pasipo kutafsiri,nakushauri soma post zangu zoote kuanzia mwanzo hadi hii page ya mwisho sababu nimewajibu wenzio walioliza maswali kama wewe kwa maandiko na mifano na kwa ufasaha sana kama una moyo wa kuelewa utaelewa ila kama huna huo moyo wa kupinga na kusoma maandiko kama "KATIBA" utabakia hivyo hivyo ulivyo!
 
Wewe imani yako inakutuma kusema Yesu ni Mungu mimi nakataa na sababu zipo maandiko unayoyasoma ndio hayohayo nami ninayasoma wengi wanatumia kigezo cha roho mtakatifu kuitumia biblia kwa maslahi yao binafsi, bibliq inaweka wazi mambo mengi kumuhusu Yesu niishie hapa ukileta ukaidi nitaweka maandiko halafu uyakatae maandiko
 
nilijua umeweka maandiko kumbe ndio zile zile story kavu kavu plz njoo na maandiko hapa wacha maneno,usipoleta inamaana umeshakubali Yesu ni Mungu!
 
Soma Luk 22:42, Luk 23:34 Luk 23:46 Yoh 17:3 hayo ni baadhi yanayokataa waziwazi unacholazimisha watu wakiamini
 
basi kwa hivi vifungu vyako ulivyoweka hapa kama ndio ushahidi wa Yesu sio Mungu hii mada haikuhusu wewe endelea kuamini hivyo hivyo nadhani itakufaa zaidi
 
Hahahah ungesema kwa nini sio kupitia ivyo vifungu
 
Usiwaangalie wa misri wa sasahv kwani ndivyo walivyokuwa miaka zaidi ya 2000 iliyopita? Soma biblia inawazungumziaje wamisri wa kipindi kile jitahidi kuchunguza nilichokiandika na ukitafakari kwa maandiko!
Mkuu huko kote atachelewa atafute General history of Africa Abridged Edition cha Unesco chapter 1 page no 15 .
 
Back
Top Bottom