Sijaelewa kidogo mtoa mada kwa hiyo hao manabii waliopita wote walikua wanafuata dini ya kiyahudi ila wayahudi si watu au jumuiya ya watu kama tunavyosema wasukuma je walikua dini gani au dini yao haikua na jina ndiyo dini ya kiyahudi ambayo ndiyo waliomsulubu yesu??
Hiyo point ya pili hapo so mungu alishuka duniani akiwa amejivika mwili wa mtu ambae ndiyo yesu kuja kuikamilisha torati ila maandiko yanasema mungu hana mfano wake hakuna kitu chochote cha kukilinganisha na yeye hazai hali wala hanywi na yeye ndiyo mkuu sasa alivyosulubiwa msalabani dunia ilikua inajiongoza au kulika na mungu mwingine anaiongoza??
Haya mambo ya dini huwa yananifanya niwe berserk sielewi elewi naomba unieleweshe mkuu
Ok kwa haraka haraka
JIBU LA KWANZA
Dini ni nini?
>Dini ni mapokeo ya wanadamu,namna wanadamu walivyolipokea neno la Mungu then wakaanzisha dini(njia) yao namna ya kulitafsiri,kulitenda,kuliamini,kulitii neno la Mungu,
>Dini zinatofautiana ila neno la Mungu ni Moja halitofautiani kwa-mfano wakristo woote wanaamini Yesu alizaliwa na bikira mariam,akahubiri injili,akasulubiwa msalabani,akafa akazikwa,siku ya tatu akafufukana yuko hai mpaka leo ila tunakuja kutofautiana namna ya kutafsiri sasa injili ya Yesu,na wanafunzi wake ndio hapo Dini zinakuwa tofauti,kuna watu hawaamini kuwa Yesu ni Mungu (wanajiita wao wakristo),kuna dini haziamini katika Roho mtakatifu(wanajiita wao wakristo),kuna dini haziamini katika uponyaji(wanajiita wakristo),kuna dini zinashika sabato(wanajiita wakristo)so dini ni mapokeo tu ya wanadamu juu ya neno la mungu
“Mnaiacha amri ya Mungu, na kuyashika sana mapokeo ya wanadamu.” —
Marko 7:8.
sasa kabla ya Yesu kulikuwa na dini mbalimbali za Miungu mbalimbali lakini dini ya kweli ilikuwa dini iliyokuwa inafuata Torati na vitabu vya manabii na iliyokuwa inaamini katika Mungu wa israel,isaka na yakobo dini hii ndio ilikuwa inafuatwa na wana wa Israel na baadaye Wayahudi
Sasa unapochanganya ni jina wayahudi na dini,ukisema wayahudi unamaanisha taifa linaitwa Judea ambalo ndani yake kuna makabila mawili (Benjamini na Yuda) na mji wake mkuu ulikuwa unaitwa Yerusalemu (kumbuka mwanzo taifa la israeli lilikuwa na kabila 12,then kabila 10 zikaasi Mungu akazitupilia mbali,hizi kabila 10 zilizo asi zilianzisha taifa lao ambalo lilibaki na jina la Israel na mji wake mkuu ulikuwa Samaria,na hizo kabila 2 zilizo baki nimezitaja hapo juu zilianzisha taifa lao lilikuwa linaitwa Yudea(Judea) na mji wake mkuu ulikuwa Yerusalemu! so hadi Yesu anakuja haya mataifa yalikuwa hivyo,utofauti nikuwa Taifa la Yedea(judea)Wayahudi waliendelea kushika maagizo ya MUNGU (TORATI na vitabu vya manabii na taifa la Samaria hawakuwa wanafuata hiyo misingi)
So unavyosema dini ya kiyahudi ni ile Dini ya lile taifa la Judea lililokuwa linafuata mafundisho ya Torati na vitabu vya manabii(AGANO LA KALE),na unaposema WAYAHUDI unamaanisha ni taifa ambalo lilimeguka kutoka katika taifa la israeli na ambalo ndani yake lilikuwa na makabila mawili YUDA na Benjamini kwapamoja walikuwa wanajiita WAYAHUDI na mji wao mkuu ulikuwa unaitwa Yerusalemu ya uyahudi
Wayahudi(dini ya kiyahudi) nikweli walimsulubisha Yesu msalabani,na Yesu alitoka katika kabila la YUDA miongoni mwa hizo kabila mbili zilizokuwa zinaunda hilo taifa la israel,sasa swala la kwanini walimsulubisha msalabani wakati alikuwa myahudi mwenzao na alikuwa ni Mungu,na alikuja kuwakomboa hao hao wayahudi nadhani unalijua
JIBU LA PILI
1Timotheo 3:16 inasema hivi ".............
Mungu alidhihirishwa katika MWILI............."
So swala la yeye kuzaliwa kama wanadamu,bikira maria kupata mimba kwa uweza wa roho mtakatifu hizo ni fomality tu za kujidhihirisha katika mwili asinge shuka tu hivi hivi kutoka mbinguni sababu angefanya hivyo dunia yoote ingetawanyika hakuna kitu kingebaki kwasababu angeshuka na ule utukufu wake pasingetosha duniani(kumbuka kile kisa kipindi cha Musa wana wa israel walipoomba kuongea na Mungu ana kwa ana na sio kupitia Musa so akawaambia jitakaseni siku 7 then atashuka so wakati anaanza kujikusanya huko mbinguni kushuka kuja kuongea nao palitokea umeme,radi,ardhi inataka kukimbia milima inatawanyika,matetemeko na shoruba zoote unazoweza kuzitaja wana wa israeli wakamwambia basi asishuke awe anaongea na Musa tu then wao wataamini maneno yatakayotoka kwa Musa unaweza kusoma kutoka 20:19)
Sasa concept yake ilikuwa ni nini?
nikwamba Mungu ni msafi sana hakai sehemu ambayo ina dhambi na akiona dhambi mbele yake anaua so mtu yoyote anayekwenda mbele za Mungu anapaswa kujitakasa ndio ile dhana makuhani walipokuwa wanaingia hekaluni kwenye chumba cha patakatifu pa patakaifu kwenda kukutana na Mungu kutoa dhabinu walikuwa wanafungwa kamba Mguuni ili akiwa na dhambi akakutana na Mungu huko anakufa so kwakuwa hakuna wa kuingia kumtoa wanachofanya wanamvuta kupitia ile kamba sasa kama Mungu angeshuka mwenyewe kama alivyo kutoka mbinguni kuja pale Yerusalemu kuhubiri injiri hakuna ambaye angekaa so ilitakiwa aje kwa taratibu za kibinadamu aje kama ilivyotabiriwa na nabii isaya kuwa mwanamke bikira atachukua mimba na kumzaa Masihi wa Bwana ndiomaana Yesu alisema kaja kutimiza Torati na sio kuitengua(so alianza kutimiza kuanzia namna atakavyozaliwa hadi atakavyo hukumu ulimwengu),
Na kwakuwa Yesu alikuwa Mungu aliyejidhihirisha katika mwiliilibidi kabla ya kuja kwake wana wa israeli wawe safi,wajitakase asikute uchafu(dhambi)mwingi miongoni mwao otherwise angewafutilia mbali so Mungu akamtuma Yohana mbatizaji(ELIYA) kuja kuwabatiza wayahudi woote ndiomaana Yohana mbatizaji alisema yeye ni kama sauti ya aliye nyikani ananyoosha tu njia ya huyo mkubwa ajaye ambaye yeye hastahili hata kufungua kamba za kiatu chake! hapo alikuwa anazungumza habari za kuja Yesu kuwa yeye yohana anawasafisha tu watu (kuwatakasa) ili Mungu akija akute ni wasafi na hakuna uchafu (dhambi) ndani yao!!!
so alivyosulubiwa msalabani ule ni mwili tu ulikuwa pale lakini roho na nafsi yake bado vilikuwa mbinguni ndiomaana Yesu pale msalabani wakati anakaribia kukata Roho alisema "baba yangu baba yangu mbona umeniacha" inamaana Mungu bado alikuwa incontrol