Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Tanzania ya sasa imejaa vioja kila ofisi ya Serikali ina maswali ya kukatisha tamaa usumbufu wa kila Aina licha ya Rais magufuli kujinadi kuwa amemaliza urasimu kwenye ofisi za Serikali

Unashindwa kuelewa nini maana yake aisee..nilipeleka mtu kuomba passport yaani unabaki jiuliza hivi mimi ni mtanzania au hii kitu napewa bure?.
 
Sijawahi kujua kwa nin waTZ tunabaniwa sana kupata hizi passport mpya as if ni ticket ya kwenda mbinguni, ni culture ya kitaahira hii, uhamiaji pale kuna watu wapumbavu sana, nlienda kutafuta passport mpya kma walivyotuambia tubadilishe, jamaa ananiuliza unakwenda huko kufanya nin, nkamwambia boss matembezi binafsi na kutalii tu, akagoma eti nilete uthibitisho ticket ya ndege, shwain kabisa....... nlirudi ofisini nkadraft barua ya safari za kufoji na partner company za nje ndo nikasikilizwa.

Mbaya zaid dawati la malalamiko/complains hata halifanyi kazi wahuni tu.

Nchi zingine wenye kasi ya maendeleo hawana mda wa kujua matumizi ya mmiliki wa passport bali wao huzingatia ni Raia halisi tu na kupatiwa passport, huu ujinga wa kutaka kujua sababu za kuhitaji passport upo Tanzania pekee, kama wanataka kuendelea na usumbufu watoe passport bure kusiwe na kulipia tshs 150,000\= lakini kama mtu analipia pesa zake bado wanamsumbua huo ni ukosefu wa nidhamu kwa mteja na Mtanzania anayehitaji passport
 
Mimi kuna kaka aliniambia, "kupata passport sio kitu kirahisi dada unatakiwa kuihangaikia. Wenzio wanakujaga mara 30 na wanakosa, wewe mara mbili tu unalalamika".

Wameshaona kusumbua watu hata kwa makosa yanayosababishwa na kupishana kwao maelezo basi ni sawa tu.
Walinikasirisha mpaka midomo ikawa inacheza.

Sema nikatumia kujuana kwangu nikaipata week tu na sikutoa hela yoyote zaidi ya hela halali inayolipwa
Naomba unipe mchakato wa kupata maana na mimi nataka nianze kufwatilia. Ni wapi naanzia na gharama ni shi ngapi!?
 
Doooh.

Sasa wakishakwambia siyo Raia ndiyo hawakupi kabisa Ppt au wanakutikisa tu ili uwape chochote kitu?

Mi hizi kero nikifikaga pale nakamata mmoja namvutia Laki yake na nusu namwambia niko kwenye kibanda cha chips pale nje, utaniita zamu yangu ikifika.. Na ppt unaondoka nayo the same Day.
Mkuu sisi raia pia kupenda shortcut na hizo laki laki ndo tunachangia mazingira pale yamekuwa magumu kupindukia. Jamaa kule ndani wana coordinate na hawa wa nje wanapiga pesa kisengerema tu. Tuache hizi watanyooka, au kma vipi unamshikisha za PCCB akanyee debe huko.
 
Kama wameshathibitishwa uraia wao, zengwe la nini kuwapatia pasipoti. shubamiit!
 
Idara ile naamini ni kubwa yenye viongozi. Malalamiko haya wamefikishiwa yakiwa bado 'hot' na wakashindwa kuyatatua? Nahofia kusiwe na kukuza mambo kusiko sahihi
 
Sio ubabe, mi naitaga ushamba. Kuna siku moja pale mutukura navuka mpaka kuingia Uganda.
Nikapita ofisini kwao ili kugonga paspoti kuna bwanamdogo mshamba nikamuliza jambo fulani akanifokea.

Nilimtukana mbele ya watu huku nikiongea kwa ukali kumsogelea.

Kwa vile wenzake waliona naongea kwa ukali tena kwa confidence wakawa wadogo na kuniomba radhi.

Uhamiaji bado huduma Bora bado sana.

Kwanza wanaongea kibabe sana jamani. Hawana lugha laini ya kumjibu mtu. Huu usumbufu wanawapa watu ni kuonyesha tu ubabe wao ndio maana vitu vidogo tu mtu anasumbuliwa navyo hata mara 5
 
Idara ile naamini ni kubwa yenye viongozi. Malalamiko haya wamefikishiwa yakiwa bado 'hot' na wakashindwa kuyatatua? Nahofia kusiwe na kukuza mambo kusiko sahihi
Kukuza mambo kusiko sahihi ndiko kupi!? Hii kero hauioni? au wewe hujakutana na hizo kero?
 
Sio ubabe, mi naitaga ushamba. Kuna siku moja pale mutukura navuka mpaka kuingia Uganda.
Nikapita ofisini kwao ili kugonga paspoti kuna bwanamdogo mshamba nikamuliza jambo fulani akanifokea.

Nilimtukana mbele ya watu huku nikiongea kwa ukali kumsogelea.

Kwa vile wenzake waliona naongea kwa ukali tena kwa confidence wakawa wadogo na kuniomba radhi.

Uhamiaji bado huduma Bora bado sana.

Uhamiaji hawaendi na kasi kama magufuli anavyotaka yafaa wamulikwe kwa jicho la tatu
 
Wao kila kichwa laki 4 au laki2 laki 4 mpaka million 1 waarabu wahindi wasomali wazaliwa wa hapa hapa ndio wanatolewa pesa nyingi tena unaambiwa kalete karatasi ya kuzaliwa ya babu yako na bibi yako wakati wewe una umri miaka 65 unaambiwa ya babu na bibi ulete tanzania nchi ya matatizo kweli.hivi kitambulisho cha taifa hakina dhamani kwao uhamiaji?
Watu milion 10 tu wakinunua pasiport kwa tshs 150, 000 Serikali itaingiza Tilion 1.5 na zaidi ukichunguza kiundani utagundua Serikali wanapoteza pato kubwa kwa usumbufu wa wafanyakazi wa uhamiaji, maswali ya msingi yabakie kwa yule Mtanzania anayeomba passport kwa mara ya kwanza, lakini Mtanzania ambaye ana passport ya zamani anataka mpya waacha usumbufu, watumie kumbukumbu za zamani kumpatia passport mpya. Huu ujinga ndiyo umeludumaza Taifa hili, uhamiaji badilikeni mwende na wakati.
 
Mimi kuna kaka aliniambia, "kupata passport sio kitu kirahisi dada unatakiwa kuihangaikia. Wenzio wanakujaga mara 30 na wanakosa, wewe mara mbili tu unalalamika".

Wameshaona kusumbua watu hata kwa makosa yanayosababishwa na kupishana kwao maelezo basi ni sawa tu.
Walinikasirisha mpaka midomo ikawa inacheza.

Sema nikatumia kujuana kwangu nikaipata week tu na sikutoa hela yoyote zaidi ya hela halali inayolipwa
Ebu niunganishe na mimi nibadili hii passport ya zamani dada [emoji847]
 
Nilimpeleka mwanangu kutoa passport mpya yeye anayo ya zamani ana renew mpya halafu anaenda kusoma nje ya nchi umri miaka 19 nikamwambia ishughulikie mwenyewe mimi nipo nje nakusubiri aliishughulikia na akamalizana akaenda kwenye finger print akamaliza akaambiwa baada ya wiki mbili akachukue na alikuwa alimshughulikia na kumsaidia kumuelekeza kijana mmoja magreshen yupo ndani . Alikuwa ana kila kitu karatasi yake ya kuzaliwa ya mama yake na baba yake na bibi mzaa mama na bibi mzaa baba na passport yske ya zamani na kitambulisho na vyeti vya shule amemaliza form six mwaka huu mwezi wa 7. Sasa tatizo alipo toka nje tuondoke na yule magresheni akawa kamaliza kazi katoka nje si akaniona mimi nipo na mwanangu akamuuliza huyu mzazi wako mwanangu akasema ndio aliniona mimi ni mwarabu mtoto nimezaa na myamwezi alichofanya kesho yake nikuitoa karatasi zote za mwanangu na kumpelekea jaamaa mmoja mkubwa na kumwambia huyu mtoto baba yake mwarabu .baada ya wiki 2 hutukupata pass ilibidi yule magreshen atupeleke kwa boss wake ana ngao akasema mtoto anafanana na msomali nikamwambia karatasi zote zipo usomali utoke wapi mama myamwezi mimi mwarabu ilibidi lipe elfu 50 baada ya kubembeleza sana
 
Dahhhh! Una damu ya ki Nigeria wewe!!!
Sijawahi kujua kwa nin waTZ tunabaniwa sana kupata hizi passport mpya as if ni ticket ya kwenda mbinguni, ni culture ya kitaahira hii, uhamiaji pale kuna watu wapumbavu sana, nlienda kutafuta passport mpya kma walivyotuambia tubadilishe, jamaa ananiuliza unakwenda huko kufanya nin, nkamwambia boss matembezi binafsi na kutalii tu, akagoma eti nilete uthibitisho ticket ya ndege, shwain kabisa....... nlirudi ofisini nkadraft barua ya safari za kufoji na partner company za nje ndo nikasikilizwa.

Mbaya zaid dawati la malalamiko/complains hata halifanyi kazi wahuni tu.
 
Nilimpeleka mwanangu kutoa passport mpya yeye anayo ya zamani ana renew mpya halafu anaenda kusoma nje ya nchi umri miaka 19 nikamwambia ishughulikie mwenyewe mimi nipo nje nakusubiri aliishughulikia na akamalizana akaenda kwenye finger print akamaliza akaambiwa baada ya wiki mbili akachukue na alikuwa alimshughulikia na kumsaidia kumuelekeza kijana mmoja magreshen yupo ndani anaitwa saidi ni mzanzibari. Alikuwa ana kila kitu karatasi yake ya kuzaliwa ya mama yake na baba yake na bibi mzaa mama na bibi mzaa baba na passport yske ya zamani na kitambulisho na vyeti vya shule amemaliza form six mwaka huu mwezi wa 7. Sasa tatizo alipo toka nje tuondoke na yule magresheni said mzanzibar akawa kamaliza kazi katoka nje si akaniona mimi nipo na mwanangu akamuuliza huyu mzazi wako mwanangu akasema ndio aliniona mimi ni mwarabu mtoto nimezaa na myamwezi alichofanya kesho yake nikuitoa karatasi zote za mwanangu na kumpelekea jaamaa mmoja mkubwa na kumwambia huyu mtoto baba yake mwarabu .baada ya wiki 2 hutukupata pass ilibidi said mzazibar atupeleke kwa boss wake ana ngao akasema mtoto anafanana na msomali nikamwambia karatasi zote zipo usomali utoke wapi mama myamwezi mimi mwarabu ilibidi lipe elfu 50 baada ya kubembeleza sana
Inasikitisha sana, watu tunaowakabidhi ofisi wanakua na Xenophobia iliyopitiliza dhidi ya watu wanaofanania na mataifa mengine au ngozi nyeupe.
Kuna rafiki yangu ana asili ya Oman ni Watanzania wa enzi ya ukoloni kabisa na hana connection na uarabuni.
Vielelezo vyake vyote vipo, kuanzia vyeti vya wazazi hadi mabibi...ila akaambiwa sio raia.
Baada ya kuwaomba wamtajie ye ni raia wa nchi gani wakamjibu hawezi kuwa raia kwa sababu ya rangi ya ngozi yake.
Watu wa magharibi mwa Tanzania Kigoma, Tabora na Kagera ni kundi lingine linalokandamizwa na uhamiaji.
Kama jina lako ni la kihaya, kinyambo, kisubi, kiha, kihangaza, kibembe, kimanyema na makabila ya magharibi mwa nchi inabidi uwe na moyo mpana.
Maneno utakayoambiwa yanaweza kukupa presha.
 
  • Thanks
Reactions: R.K
Naunga mkono hoja...Ongeza na hili, mtu yoyote akienda kuomba passport lazima wamwambie sio raia pamoja na maneno ya kukatisha tamaa.
"Rudi kesho", " unatusumbua", "kwanza unafanana na Wakenya utakua Mkenya wewe". Uhamiaji kuna haja ya kuufanyia mabadiliko.
Napendekeza uhamiaji wafanye kazi ya kuthibitisha uraia halafu passport zitoke TRA kama walivyofanya kwenye leseni za udereva
Uhamiaji watoe fomu,uthibitisho nida passport TRA kwisha kazi.
 
Uhamiaji ni jipu lililooza, linanuka uvundo wa rushwa tupu pale Arusha paspoti za East n Central Africa ni tshs 20,000 single journey ila kama huna 50,000 sahau kuipata, utawekewa vikwazo hadi uamue uitoe hiyo 50,000 ama uahirishe safari , huu ni unyama ukizingatia once ukirudi utahitaji kukata pass nyingine haijalishe ulisafiri kwa matibabu ama ujasiriamali mdogo mdogo, yawezekana mama I mean boss wao kawashindwa ama wanamkomoa ili aonekane kashindwa kazi, serikali ina mkono mrefu tumeni watu wenu kwa muda muafaka mtajua nini wananchi tunasema
 
Usumbufu wote ili utoe kitu kidogo Mzee hakuna cha zaidi.
 
Yaan bora nyie huko sisi hiku KIGOMA yaan wanatuona wote ni warundi kwanza ukisafiri migration wamejaa kila kituo kusimamishwa kuulizwa maswali sijui unaitwa nani unaenda wapi kufanya mwwenyekiti wako nani na blabla nyingii pamoja na kitambulisho. Sasa usiende kutafuta passport ndo utaomba poo
Kunarafiki yangu alienda kufuatilia passport mpaka leo hana ham maana walihoji familia nzima akaambiwa akawalete wajomba mashangazi sijui akawaonyeshe kaburi la babu na bibi yake sijui apeleke cheti cha kuzaliwa cha babu yake yaan mwishoni akawaambia mi basi nimechoka na usumbufu wenu sasa yaan Kama ndo kawazidishia wanaendelea et kimfuatilia kwanini aache huenda We ni mkimbizi anawaambia nimeacha kwa sababu ya usumbufu wenu kama na kitambulisho cha taifa na taarifa zote nimezijaza af mnanisumbua si bora niache tuu? Kumbe wanataka rushwa tuu. Hapa mimi cjui nitafanyeje maana nahis kunamtu anaenda kuvunjwa mguu
 
Back
Top Bottom