We kumbe huijui hii nchi yani bora awamu hii ya huyu magu ila jua ya kuwa wao hawakuombi rushwa moja kwa moja ila mizinguko yao hata uende polisi tena wao ndio Bora uhamiaji watataka chochote usipowapa wataanza kujifanya wanamambo mengii ukienda sijui kwa Mkuu wa wilaya atakwambia nenda polisi utashughulikiwa yaan kuna baadhi wanafanikiwa ila ukijifanya mjuaji ndo unaweza kubambikiwa kesi ya mkimbizii mpaka uombe poo. Kuna rafiki yangu mwengine alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi aliwahi kufuatilia passport basi walipoanza kumsumbua akaanza kuwashtaki sijui polisi takukuru kilichomtokea mpaka leo ni Historia amepewa kesi kuwa yeye ni mkimbizi kwakuwa babu yake hajulikani alipozaliwa yaan mpaka leo mshahara wake umesimamishwa mwaka wa tatu anamaisha magum saana ashaenda mpaka ofisi Za wizara ya mambo ya ndani ila hakuna chochote anabaki kujisemea ningelijua ila ndo ivo. Ukwel ni kuwa unaweza kuwashtaki ukapewa haki au usipewe wakakukomoa. Nchi hii haki ni bahati ya mtu na sio et We unafuata sheria
Elimu ya uraia hii nchi imekaa hovyo kabisa ...
Wewe Ni sampuli na mfano tosha kuwa nchi hii imejaa raia wasioelewa haki zao...
Narudia tena Kama unajijua umekamilisha kila kitu na uko kwenye haki hupaswi kulialia ...
Naomba uniambie huyo ndugu yako Ni kweli ni raia au sio raia ??? Kama ni raia sema mkoa gani walimsumbua .... Mkuu wa mkoa gani alimsumbua ... Kituo kipi Cha polisi kilimsumbua ....
Weka hizo taarifa zako hapa.... Halafu tuone Kama kitashindikana Kitu...
Mtaaani kumejaa Entities kibao zinatoa msaada wa kisheria bure kabisa mnashindwa hata kwenda kutafuta haki zenu .. Unaijua Tawla ??? Unaijua LHRC ? Na zingine nyingi.
Unamjua Abdul nondo ??? Yule kijana anatokea ujiji na chimbuko la babu zake Ni Congo japo walizamia tanganyika miaka na miaka ... Unadhani kwanini alichomoka hizo shutuma kuwa sio raia ... Alisimamiwa na hao LHRC na Taasisi ya haki za binadamu ambazo huduma zao Ni burw kabisa ....
Halafu unaposema eti hawakuombi rushwa ila wanakuzungusha !!! Unajua forms za rushwa ???? Au hujui hata kuchelewesha huduma kwa raia ni kosa ... Daaaah hii nchi elimu ya uraia bado Sana ....
Mimi nakuomba uweke hizo taarifa nilizokuomba hapa Ilimradi Huyo mtu awe ana uhakika ni raia wa Tanzania .. Kwa maelezo zaidi Chukua katiba Soma nini maana ya mtanzania na akiona ameingia kwenye hiyo tafsiri ajue ananyimwa Haki zake .. Aanze mara moja kufuatilia haki yake.. Nimempa baadhi ya ofisi hapo juu...
Na huko wizarani aliyeyushwa tu amtafute waziri husika , hivi hujui hata wizarani kumejaa vijeba ...
Akishindwa afunge safari hadi Chamwino ....