Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Mipakani ndio balaa kabisa yaani kitu kidogo tu utasumbuliwa kma mhaini
Nakumbuka siku moja kwenye mpaka ... "Kapuni" Baada ya kumsalimia afisa na kumkabidhi pasi akaniuliza... Unakwenda kufanya nini?.. Nikamjibu > Naenda kutembea!.. Akajanijibu: Naona wewe ni mtalaam, unaenda kutafuta kazi huko?, Huku kwetu mbona kazi nyingi tu?. Nikamjibu... Naenda kutalii na nikipata fursa ya kufanya kazi huko nitaangalia maslahi yako vipi. Akagonga pasi na kunitakia safari njema.

Upande wa pili nakutana na afisa ambaye inaonekana amejifunza namna ya kuhudumia wateja kwa bashasha umakini na kuzingatia sheria, Jengo moja huduma ile ile lakini upande mmoja huduma kwa wateja kwa kiwango cha chini kabisa.
 
Hawa jamaa wanakera sana, sanaa
 
Hela ya nini mtoto mashalah! Watu huwa wanaweka stock for future.
 
Ni kweli mkuu,kuna Dada aliamua kuacha kufuatilia nida I'd baada ya kuambiwa mambo kama hayo,kutoka kigoma imekuwa ni kesi sasa.

1.je huko walishaanza kutoa namba za vitambulisho vya nida?
2.unapatikana maeneo gani hapo mkoani mkuu?
Hayo tu,wasalimie kigoma nyumbani kwetu.
 
Acheni upumbavu na Ujinga watanzania ... Hivi watanganyika vichwa vyenu vikoje ...


Kuna mawasiliano ya kamishna was uhamiaji kwanini msipige na mumpe lawama ... Kuna namba ya Waziri wa Mambo ya Ndani kwanini hatuwapigii Hawa wakuu wao??.


Kuna Mkuu wa wilaya na mkoa kwanini msijikusanye muende kutoa huu upuuzi wa hiyo ofisi....



On top Kuna ofis za PCCP kila mkoa hivi mnashidwa vipi kwenda kutoa hizi shutuma maana zimekaa kirushwa rushwa ... Alieturoga watanzania ameshakufa na kuoza ... hivi inawezekana vipi umekamilisha matakwa yote na unazungushwa halafu unaridhika huu Ni ujinga na unanipa hasira saaaaaana natamani nikutandaze viboko ....



Mimi kila ofisi ya Umma ninayoingia huwa najitahidi Sana kukamilisha vigezo na masharti ila ukianza kunizungusha lazima nitafute haki yangu Pccb, bosi wako , RPC, RC na mawaziri... Simu yangu ina namba ya mawaziri wote ...



Hivi mnashindwaje Nyie wananchi huwa nashangaa Sana mnashindwa kuwakaanga hao wapuuzi ...
 
Uhamiaji Uhamiaji Uhamiaji,
Mwakani nakuja kurenew passport yangu sasa ole wenuuuuu
Ama zangu, Ama zenu,
[emoji1320][emoji35]
 
We kumbe huijui hii nchi yani bora awamu hii ya huyu magu ila jua ya kuwa wao hawakuombi rushwa moja kwa moja ila mizinguko yao hata uende polisi tena wao ndio Bora uhamiaji watataka chochote usipowapa wataanza kujifanya wanamambo mengii ukienda sijui kwa Mkuu wa wilaya atakwambia nenda polisi utashughulikiwa yaan kuna baadhi wanafanikiwa ila ukijifanya mjuaji ndo unaweza kubambikiwa kesi ya mkimbizii mpaka uombe poo. Kuna rafiki yangu mwengine alikuwa ni mwalimu wa shule ya msingi aliwahi kufuatilia passport basi walipoanza kumsumbua akaanza kuwashtaki sijui polisi takukuru kilichomtokea mpaka leo ni Historia amepewa kesi kuwa yeye ni mkimbizi kwakuwa babu yake hajulikani alipozaliwa yaan mpaka leo mshahara wake umesimamishwa mwaka wa tatu anamaisha magum saana ashaenda mpaka ofisi Za wizara ya mambo ya ndani ila hakuna chochote anabaki kujisemea ningelijua ila ndo ivo. Ukwel ni kuwa unaweza kuwashtaki ukapewa haki au usipewe wakakukomoa. Nchi hii haki ni bahati ya mtu na sio et We unafuata sheria
 
Ungejifanya kujishusha wangekusumbua haswa. Watu wa hivyo ukiwakazia wanakuaga wapole sana
 
Mi sikutumia connection mwanzoni ila nilikua na uwezo wa kuipata ndani ya siku moja. Walivyonikwaza mara ya pili nikasema acha nitumie connection. Na vile nilikua nasafiri siku hiyo nimeenda peleka form nikamwambja ntaifuata after a week. Hata week haikuisha passport ikawa mezani.
Wapo wenzako wajanja zaidi hupata hata kwa masaa au siku Hiyo hiyo, connection ndiyo imeshika kasi kuliko chochote.
 
Huyo si aende kutoa ushuhuda Bungeni iweje ateswe hivyo na akawa kimya?
 

Humu JF watumishi wa Uhamiaji wapo wataona jinsi wachangiaji walivyowatuhumu itakuwa ni njia mojawapo ya kuwazundua waache usumbufu
 
May b kuna wakati wanasumbua sana ila MIMI NILITUMIA OFISI ZA MWANZA WAKO POA HALACU WANAELEKEZA VIZURI SEMA WAMEKAA MKAO WA HELA HELA
 
Elimu ya uraia hii nchi imekaa hovyo kabisa ...


Wewe Ni sampuli na mfano tosha kuwa nchi hii imejaa raia wasioelewa haki zao...


Narudia tena Kama unajijua umekamilisha kila kitu na uko kwenye haki hupaswi kulialia ...


Naomba uniambie huyo ndugu yako Ni kweli ni raia au sio raia ??? Kama ni raia sema mkoa gani walimsumbua .... Mkuu wa mkoa gani alimsumbua ... Kituo kipi Cha polisi kilimsumbua ....


Weka hizo taarifa zako hapa.... Halafu tuone Kama kitashindikana Kitu...


Mtaaani kumejaa Entities kibao zinatoa msaada wa kisheria bure kabisa mnashindwa hata kwenda kutafuta haki zenu .. Unaijua Tawla ??? Unaijua LHRC ? Na zingine nyingi.

Unamjua Abdul nondo ??? Yule kijana anatokea ujiji na chimbuko la babu zake Ni Congo japo walizamia tanganyika miaka na miaka ... Unadhani kwanini alichomoka hizo shutuma kuwa sio raia ... Alisimamiwa na hao LHRC na Taasisi ya haki za binadamu ambazo huduma zao Ni burw kabisa ....




Halafu unaposema eti hawakuombi rushwa ila wanakuzungusha !!! Unajua forms za rushwa ???? Au hujui hata kuchelewesha huduma kwa raia ni kosa ... Daaaah hii nchi elimu ya uraia bado Sana ....



Mimi nakuomba uweke hizo taarifa nilizokuomba hapa Ilimradi Huyo mtu awe ana uhakika ni raia wa Tanzania .. Kwa maelezo zaidi Chukua katiba Soma nini maana ya mtanzania na akiona ameingia kwenye hiyo tafsiri ajue ananyimwa Haki zake .. Aanze mara moja kufuatilia haki yake.. Nimempa baadhi ya ofisi hapo juu...


Na huko wizarani aliyeyushwa tu amtafute waziri husika , hivi hujui hata wizarani kumejaa vijeba ...

Akishindwa afunge safari hadi Chamwino ....
 
Idara ile naamini ni kubwa yenye viongozi. Malalamiko haya wamefikishiwa yakiwa bado 'hot' na wakashindwa kuyatatua? Nahofia kusiwe na kukuza mambo kusiko sahihi
Huyu jamaa anasema walienda Jana
Immigration ndio hayo yakamkuta. Hivi mmesahau jana ilikuwa ni PH?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…