Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Pale migration aisee bila rushwa hupati passport uwe una renew au ndo unaomba mara ya kwanza.
 
Haya Huyo mtu anaitwa Festo Malabe ninzaliwa wa kigoma maeneo ya gungu alikuwa anafundisha wilaya ya Buhigwe nitakutumia namba zake za sim alaf nitakuwa namuulizia..
 
Haya Huyo mtu anaitwa Festo Malabe ninzaliwa wa kigoma maeneo ya gungu alikuwa anafundisha wilaya ya Buhigwe nitakutumia namba zake za sim alaf nitakuwa namuulizia..
Anza na Hawa..


MAWASILIANO LHRC

EMAILlhrc@humanrights.or.tz
PHONE NO+255 22 2773038 / +255 22 2773048
WEB ADDRESShttp://www.humanrights.or.tz



MAWASILIANO TAWLA

TAWLA House, Plot 33 Ilala Sharif Shamba
+255 222 852856
tawla.information@gmail.com / info@tawla.or.tz
P.O. Box 9460 Dar es Salaam
 
Labda huenda umefumba macho ukijisi unaona.. Hivi unajua katika nchi hiihii kunawatu wananyimwa haki zao na niwasomi huenda kuliko wewe? Nikupe mfano tu wa kawaida unajua kuwa kila raia anahaki ya kufanya siasa popote katika nchi hii? Ila unahabari kuwa kwa sasa hiyo haki haipo na mikutano haitakiwi ila kwa mtu ambae ni kiongozi wa eneo husika? Unajua kuwa kunawatu wanadhulumiwa haki zao za kupanda madaraja kazini? Hivi hao watu hawajui kuwa ni haki?.. Narudia hata hao unaiwasema wakiingilia kati itabaki ni bahati ya mtu na wakiamua asipate haki hapati tuu na hawatofanywa lolote
 
Hii hoja iko Sawa, maana hata mimi yamenikuta pass yangu imeisha wakati inaelekea ukingoni nikaenda kuulizia utaratibu wakurenew nilichoambiwa sasa nikabaki kushangaa!!!!! Eti natakiwa nipate barua ya mwaliko kutoka huko ninapotaka kwenda na sababu zake nikabaki kujiuliza hivi ndo ninaanza kuaplai upya?!!! Nikaona bora hata ya leseni ya udereva naomba serikali kama itaweza basi hata passport nayo iwe kama leseni ya udereva kwa wale ambao wameshaipata.
Vinginevyo ni usumbufu tu.
 
Unadhani hicho ulichosema ndio kinaondoa umbumbumbu wa watanzania ?? Hayo uliyosema unadhani yanaweza fanyika kwenye nchi iliyo na UPUNGUFU wa raia wasio na uelewa na haki zao???


Jibu Ni Lile lile Watanzania sisi Ni mazwazwa.Full Stop.


Masuala ya mikutano Ni political affiliated... Kama hutaki kudai haki yako kwasababu vyama vya siasa havifanyi mikutano endelea kudidimizwa Hadi Ukome.


Kama kutopandishwa madaraja kwa watumishi ni sababu ya wewe kutokusotea haki yako endelea kulala tu.


Licha ya watu kutopandishwa madaraja na vyama vya siasa kutofanya mikutano Kuna watu wamepata Haki zao kwa kulazimisha hata kuonana na raisi na mijitu kutumbuliwa ...

Sasa wewe endelea kukaa mguu juu eti utadai haki zako siku watu wakipandishwa madaraja ..
 
Ukiona Mizengwe jua wanatengeneza Mazingira uwape rushwa.

Wakiomba rushwa tu toa taarifa Takukuru.
 

Wanakwamisha watu makusudi ili uende kwa vishoka wao wanacharge 300,000 passport moja kwa usumbufu wa passport Anna Makakala jitathimini
 
Kwa upande mmoja nakubaliana na mtoa hoja ila upande mwingine namponga,
Watanzania tumekuwa wepesi sana kutukuza ugeni, wengi humu wanachojadili ni kulinganisha Tanzania na mataifa ya ulaya Jambo ambalo alitatokea leo wala kesho.

Jiulize kitambulisho cha Taifa Duniani kilianza kutolewa mwaka gani na sisi tulianza lini na kwa watu wangapi?

Jiulize hao Uhamiaji wanamfanano wa taarifa za Kila mtanzania yaani Wana taarifa zako toka siku unazaliwa Hadi leo?

Mimi Kati ya kitu ambacho ninakipiga Vita Ni kuwapa wageni pasipoti kwa sababu tu Wana cheti Cha kuzaliwa, kitambulisho Cha Taifa na wamesoma Tanzania....Mimi Nina marafiki zangu walikuwa wakimbizi kigoma lakini nilikutana nao Canada na mwingine Australia wakiwa na pasipoti za Tanzania na walipofika kule wakazichana/wengine wakazificha na kuomba ukimbizi...

Tunawalalamikia Kila siku kuwa kuna wahamiaji haramu ( neno la kibaguzi kabisa kulitumia),hivi hao wahamiaji haramu wanasoma wapi? Wanatumia document gani Kama siyo kujifanya Watanzania?

Waacheni wafanye kazi yao la sivyo wasipochuja vizuri kwa presha za kusema pasipoti zitolewe na TRA au mamlaka nyingine ipo siku tutakuta wakongo, warundi, wakenya, wanigeria, wahindi wanatamba na pasipoti zetu huko nje.

Mbona yukiomba visa hatulalamikiage balozi ? Mtu anatoka nje mwaka anakuja kabadili Hadi lafudhi kisa aonekane mzungu...lazima Uhamiaji wakipige kuanzia lafudhi Hadi mashauzi. Kenya wanaumizwa na alshababu kwa sababu tu hawakuchuja ipasavyo.

Mimi nakubaliana na mchujo unaofanywa na uhamiaji kwa sababu najua wapo waliojipatia pasipoti zetu kwa rushwa lakini si Watanzania, wapo waliofoji vyeti.......jiulize wale watumishi feki walitumia majina na documents gani kuomba pasipoti?Leo wakija kubadilishwa waendelee kuruhusiwa kutumia majina ya vyeti vyetu....,....tuache UBINAFSI, hapa naiunga serikali mkono kwa sababu tukicheza kwenye pasipoti au kuweka siasa sisi wanyonge na vizazi vyetu ndo tutaumia.
 
Kwa usumbufu wa hao uhamiaji wametufahamisha kuwa kitambulisho cha taifa ni upuuzi tu maana unaulizwa maswali yaleyale tena
 
Wanaoletewa usumbufu kwenye kupata pass ni wale wenye haki nazo na hao unaowaita wanyonge. Hao wageni au wakimbizi wala hawapati usumbufu huo tunaokutana nao sie raia wenye haki.Na huo usumbufu wa uhamiaji wala hauna lengo la kudhibiti chochote zaidi ya uzembe na kutengeneza mazingira ya rushwa tu
 
Siku hizi uhamiaji naona kama wako pouwa tu na ufanisi wao umeongezeka mana nilijaza form na pamoja viambatanishi vyote nilienda mara moja kupeleka na siku hiyo nilichukuliwa vidole na baada ya wiki moja passport yangu ilitoka.

Wala sikumuhonga mtu hata centi moja na baada ya hapo niliwasaidia watu wengine watatu kwa nyakati tofaut kujaza form online na kuwaambia nini wanatakiwa wawe navyo na pia kuwasisitizia wasiweka hela mbele au kutengeneza mazingira yoyote yale ya hela zaid ya ile 150,000/= tu na kwel wote walipata bila usumbufu wowote tena baada ya siku saba za kazi.
 
Idara ile naamini ni kubwa yenye viongozi. Malalamiko haya wamefikishiwa yakiwa bado 'hot' na wakashindwa kuyatatua? Nahofia kusiwe na kukuza mambo kusiko sahihi

Hujawahi kwenda uhamiaji wewe! Haya ni mambo ya wazi kabisa yanafanyika mchana kweupe, Miaka nenda miaka rudi Uhamiaji is rotten!

Tatizo la nchi hii washamba wengi sana! washamba wamejazana maofisini basi tabu tupu, Elimu ya kukariri haijawasaidia kitu, ustaarabu mdogo, exposure ndogo maendeleo tuendelee kuyasikia tu Nchi za watu.
 
Yani hawa jamaaa ni vimeo kweli kweli, ni kitu hata Mimi nilibaki najiuliza sana, pass yangu nshaitumia kuingia nchi kibao, na sio kwamba hata imeisha muda ila nataka ya electronics , unaenda unaanza kuulizwa maswali ambayo hayana maana, pia hata barua ya mtendaji ya nini tena au Mwenyekiti wa mtaa ya nini kama nina national ID? Hiyo NIDA haina taarifa zangu? Unaniambia nilete leseni ya biashara na tiketi ya ndege, yani kama vichaa, nikakate tiketi ya ndege mapema kisa nataka ku renew passport? Si waafrika bado sana, hata reasoning capacity yetu INA uwalakini, ndio maana sometimes Magufuli anawatukana hawa maboss wa hizi taasisi, utafikili wana akili za kushikiliwa.
 
Hivi mwisho wa kutumika passport ya zamani ni tarehe ngapi wakuu
 
Haya Mambo yanatakiwa yatatuliwe na vyombo vya upelelezi lkn nao wamelala lzm Mambo yaende kombo.. waje wadabishe Wala rushwa uone patanyooka tu..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…