Uhamiaji Badilikeni: Acheni kufanya kazi kwa mazoea

Saa zingine najiuliza hizi NIDA za kazi gani maana unakuwa nacho ila usumbufu unakuwa mwingi
 
Kukuza mambo kusiko sahihi ndiko kupi!? Hii kero hauioni? au wewe hujakutana na hizo kero?
Sijakutana nazo/nayo. Na popote ninapokutana na kero katika huduma za serikali najitahidi kupata suluhu palepale na sio kuja kutatulia tatizo Jamiiforum.
 
Huyu jamaa anasema walienda Jana
Immigration ndio hayo yakamkuta. Hivi mmesahau jana ilikuwa ni PH?
Mwongo hana rangi aisee. Kakimbilia Jamiiforums na kuliacha tatizo palepale Uhamiaji, kama kweli lipo. In short anataka tuamini majungu
 
Mshachukua hatua zipi nyie wenye exposure mlipokutana na hizi kero? Mlisubiri kuja Julia huku? Tunatatizo mahala
 
Saa zingine najiuliza hizi NIDA za kazi gani maana unakuwa nacho ila usumbufu unakuwa mwingi
Uhamiaji usumbufu huwepo hata kama utakuwa na kila kitu bado watasaka kisingizio kingine
 
Mwongo hana rangi aisee. Kakimbilia Jamiiforums na kuliacha tatizo palepale Uhamiaji, kama kweli lipo. In short anataka tuamini majungu

Jamii forum ni sehemu muhimu ya kutolea kero za kijamii ambazo huwa zimeshindikana, huko uhamiaji huwezi kusikilizwa hata ulalamike vipi ndiyo maana mleta mada akaamua kuja JF akiamini hata viongozi wa Uhamiaji watapita humu na kuona malalamiko yote kisha kuyafanyia kazi.
 
Sijakutana nazo/nayo. Na popote ninapokutana na kero katika huduma za serikali najitahidi kupata suluhu palepale na sio kuja kutatulia tatizo Jamiiforum.

Usipadharau JF na kama unaona siyo sehemu sahihi ya kutolea kero ambayo wewe binafsi haijakutana nazo ni vyema uache wenye kero wapate kutema nyongo zao ili viongozi wa uhamiaji wapate kujirekebisha
 
Sasa Kama mtu ni mkimbizi kwanini apewe passport ???


Wao hawana tracking mechanism ya kujua Huyo Kama Ni mkimbizi au laah ?? Wakimbizi wote si wapo kwenye database za UNHCR wameshindwa vipi kuweka majina kwenya database ya un kujua Kama hao Ni wakimbizi...


Kambi zote ziko chini ya Wizara ya mambo ya Ndani na uhamiaji wapo Kama mtu anashukiwa Ni mkimbizi kwanini wasitrack ??

Kwahiyo mnaona Raha kutreat watanzania na kuwapa shida za kupata pass zao kisa Kuna wakimbizi ???


Hivi mnadhani Tanzania ndio nchi pekee yenye wakimbizi ??? Mbona kuna baadhi ya nchi zina wakimbizi na michakato ya kupata passport iko vizuri na wazi. Na hao wakimbizi wakithubutu kuomba wanabambwa.

Unajua Kuna vitu vinaendeshwa hii nchi Hadi unajiuliza watu wanakula hela za bure tu na hawafanyi kazi ipasavyo...




Haiwezekani uwepo wa wakimbizi umfanye mtanzania wa kawida kupata shida kwenye zoezi la kupata passport yake...


Kuna watanzania wana kila aina ya vigezo wanazungushwa.


Niishie hapa , inatosha japo ninatamani nizungumze zaidi ya hapa.

Sent using Jamii Forums mobile app
 


Mikwala na comment ndefu nikajua wewe ni mtu mzito unataka kutoa msaada kwa huyo ndugu yake , kumbe na wewe kanjanja tu unaongea kama sio Mtanzania bwana wakati hizo Shida ni zipo wala huyo mkuu wa wilaya hawezi kutoa msaaada mpaka Maghufuli atoe tamko
 
Nyinyi ndo mnakaa nyuma ya viti na kusumbua watz wenzenu kwa kisingizio cha kukwepa kusajili wakimbizi

yaani wewe umesomea mambo ya uhamiaji halafu huwezi kubaini nani raia na nani ni haramu hadi usumbue kila anayekuja mbele yako!?

duuh maajabu hayataisha tz hii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Naunga mkono hoja asilimia 100. Navyojua mimi kama unamiliki kama unamiliki pasipoti halali haitakiwi usumbuliwe. Vinginevyo kama mtu ndio anaanza kuomba kwa mara ya kwanza. Ukiona unamiliki pasipoti na unataka ku-renew wakikusumbua fahamu wanataka rushwa. Dawa yao wawekee mtego wa PCCB. Watanaswa kiulaini
 
Binafsi sioni kama uhamiaji kuna tatizo ila naamini sisi ndio tuna matatizo, kama kweli wewe ni Mtanzania na una vigezo kwanini usiwe na documents ambazo zitadhibisha na kuona kweli unastahili kupata Passport!!?

Nilienda uhamiaji mida ya saa Saba mchana nimejipanga haswaa hasa katika swala la documents, yule Brother alie nishughulikia alisema unastahili na huna sababu ya kuto kupewa Passport.

Nikapewa tarehe kweli nikaenda kuchukua wizara ya mambo ya ndani, yani faster tu hata Wife alinishangaa akasema eti Mimi kijukuu cha Mtume ila ukweli nilijipanga kwa vigezo na sikutoa hata rushwa mia.

Serikali naipongeza kwa hatua zake maana hapa Bongo kambi za wakimbizi ni nyingi na asilimia kubwa wakimbizi wana ongea kiswahili kizuri.. Binafsi nawapongeza sana Uhamiaji na nampongeza JPM kwa hatua za kumpa heshima Mtanzania na Passport mpya.

Wengi wenu mlipata Passport za zamani kimaghumashi mkubali mkatae, kwa taratibu za sasa lazima mrudishwe kwasababu mlizoea kutoa rushwa Passport zinawafata majumbani sasa hivi ngumu.

Asante Mh Rais na Uhamiaji kwa kuleta heshima ya Mtanzania tutaelewana tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe utakuwa ni mfanyakazi au Mtumishi wa uhamiaji umeamua kuwatetea kijanja lakini utambue kuwa unalea Ugonjwa mbaya wa kuendeleza usumbufu usio na Tija unaolikosesha Taifa mapato
 
Uhamiaji wanakosa mapapato watanzania wengi wanataka passport lakini kutokan na usumbufu wameamua kukata Tamaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…