Nadhani huyo dogo wa immigration anasoma huu uzi na hii reply ni yake kama ifuatavyo...
Nasema "hii dunia ni moja, haya mataifa yametokana na dhambi zilizosababishwa na wewe, hiyo nafasi hapo uhamiaji ni cheo cha muda, hawa binadamu wapo na hawataisha, tunakuja na kuondoka, kesho anaota/birth mwingine as huyo kijana uliyesababisha akazaliwa nchi uliyotaka wewe"...
Kumbuka, ... "lolote unalomfanyia mwenzako hujirudi kwa njia nyingine na kukuadhibu ukiwa umesahau matendo uliyomfanyia mwenzako. Tabia kama hiyo ya kukomalia jambo ambalo kwa elimu ya darasani kwenye mambo ya uhamiaji sidhani kama uliwahi fundishwa kukomaa na mtu mwenye hujauzito"...
Na ... "baada ya tukio la kumsababishia hali ile ukakimbia ila nafsi yako najua inavyokusumbua na huna la kufanya although unajipa moyo ulikiwa kazini ukitekeleza wajibu, wajibu gani ambao unaona kabisa kuna hali ya hatari?."
Haya ni maisha mdogo wangu afisa uhamiaji na hizi ni nchi za Afrika Mashariki mnazojipambanua kuwa na ushirikiano wa jumuiya, mwisho "hata wewe unajiita kidume ukiwa mkoa nje ya Mara au nje ya Tanzania huwa unaparamia mabinti wa watu, siku unaondoka hujui kama ulipandikiza mbegu"
Asante.