Uhamiaji Musoma, huyu mama kutoka Burundi angefariki damu yake ingewalilia

Mama mjamzito ametoka Burundi kwenda Kwa mume wake Kenya Juzi tarehe 25/02/2022. Alivyofika Musoma alikamatwa na uhamiaji sehemu ainayoutwa Kurumuli (Barrier) . Alijitetea kwa uchungu Sana mpaka tulio kuwa kwenye gari lile tulipata huruma.

Mama alijitetea kuwa anaenda Kenya kujifungulia huko kwa mchumba aliyempa ujauzito, asingeweza kujifungulia kwao maana hana msaada na hata hivyo hajapata chakula tangu aanze Safari akitokea Burundi Kupita mpaka wa BURUNDI na NGARA na hata hivyo alijitetea kwenye mpaka huo na akasikilizwa.

Afisa wa uhamiaji Musoma hakutaka kabisa kusikiliza na hakujali hali ya mama yule. Alishikiliwa mpaka akapata labour pain (Uchungu) akakimbizwa Kituo cha AFYA NYASHO .

Mama hakuwa na chochote hata nguo hana, kibaya zaidi alipaswa kufanyiwa upasuaji kwa sababu alipata uchungu pingamizi.

Maafisa uhamiaji waliomleta wakatokomea na hata walipotafutwa hawakuwa na msaada, maana kituo hawakuwa na vifaa vya kama surgical gloves, Dawa za baada na kabla ya upasuaji, drip n.k

Watumishi wa kituo hiki walichanga pesa wakamsaidia. Leo yuko wodini hata chakula anapewa na wagonjwa wenzie. Hana nguo anatumia mashuka ya Kituo.

"Hivi uhamiaji pamoja na Sheria za nchi kwa Hali kama hiyo hawakuwa na chakufanya kuanzia kwenye ukamataji"?
Hii nchi Ndugai ni kichaa lakini alisema ukweli kuwa ishauzwa
 
Mkuu wakati mwingine hizi huruma za kitanzania zinatuponza!!cha msingi hujaelezea tatizo lilikuwa ni nini, sio mambo ya eti alijieleza, wapi, mfano kama hana muhuri wa mpakani alipoingilia nchini, unategemea nini?!!hilo ni jambo dogo?!!Acheni lawama kwenye mambo ya msingi, wewe nenda RWANDA, DRC, BURUNDI, uingiaji wako huko uwe una mashaka, ndio utajua kuwa nchi ya watu sio kitongoji.
Sasa kama uingiaji wake nchini una kasoro washindwe kusimamia sheria ila watangulize ubinadamu zaidi?!!likija kulipuka huko utawaambia viongozi wako, eti nilitumia ubinadamu kupindisha sheria, tena kwa mgeni?!
Hujaelewa soma tena uzi

Umeelewa tunacholaumu ni kipi?
 
Umeelewa mada kweli?
Naona hajaelewa mada,na ndiyo maana maelezo yake yako nje ya mada hii!! Inaonekana hata kanuni na taratibu za uhamiaji Tanzania hazijui kabisa, ndiyo maana kabaki kulinganisha na uhamiaji wa Nchi zingine za ki Africa wanavyo wa treat wageni!!
 
Hamjalaumu kuhusu ukamataji, mmelaumu kuhusu nini ?

Kama unakubali kwamba alivyokamatwa ni sawa hapa tunabishania nini cha zaidi ???
Tunalaumu kumtelekeza mtuhumiwa wenu! Je Magereza au police nao wakiwa wanawatelekeza watuhumiwa wao baada ya kupata maradhi au ujauzito hali ingekuwaje unazani!?

Kamata mtuhumiwa wako,hata akipata tatizo la ki afya mpe huduma kwanza,alafu akisha pona waweza endelea na mashitaka yako!!
 
mmh maskini waafrika hatupendani. Hope Mama na mtoto watatoka salama hospital
huwa napata kigugumizi unakuta mkuu wa polisi anakaa front page kutangaza kakamata wahamiaji haramu 30 au 40 si upuuzi huo.
wale wanapita tu waende wanakokwenda si muwaache tu
 
Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchungu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Acha upuuzi wako, mambo mengine unatumia akili tuu sio kujifanya unafuata sheria za kufikirika na unauliza passport wakati wenye nazo hata one percent ya nchi nzima hawafiki
 
Mama mjamzito ametoka Burundi kwenda Kwa mume wake Kenya Juzi tarehe 25/02/2022. Alivyofika Musoma alikamatwa na uhamiaji sehemu ainayoutwa Kurumuli (Barrier) . Alijitetea kwa uchungu Sana mpaka tulio kuwa kwenye gari lile tulipata huruma.

Mama alijitetea kuwa anaenda Kenya kujifungulia huko kwa mchumba aliyempa ujauzito, asingeweza kujifungulia kwao maana hana msaada na hata hivyo hajapata chakula tangu aanze Safari akitokea Burundi Kupita mpaka wa BURUNDI na NGARA na hata hivyo alijitetea kwenye mpaka huo na akasikilizwa.

Afisa wa uhamiaji Musoma hakutaka kabisa kusikiliza na hakujali hali ya mama yule. Alishikiliwa mpaka akapata labour pain (Uchungu) akakimbizwa Kituo cha AFYA NYASHO .

Mama hakuwa na chochote hata nguo hana, kibaya zaidi alipaswa kufanyiwa upasuaji kwa sababu alipata uchungu pingamizi.

Maafisa uhamiaji waliomleta wakatokomea na hata walipotafutwa hawakuwa na msaada, maana kituo hawakuwa na vifaa vya kama surgical gloves, Dawa za baada na kabla ya upasuaji, drip n.k

Watumishi wa kituo hiki walichanga pesa wakamsaidia. Leo yuko wodini hata chakula anapewa na wagonjwa wenzie. Hana nguo anatumia mashuka ya Kituo.

"Hivi uhamiaji pamoja na Sheria za nchi kwa Hali kama hiyo hawakuwa na chakufanya kuanzia kwenye ukamataji"?
System ya majambazi tu!
 
Mimi naona uhamiaji inalaumiwa bure. Je, huyo mama alikuwa na passport ya Africa Mashariki akakataliwa kuendelea na safari? Tukitunga sheria lazima tuzifuate. Hatuwezi kuchagua sheria ipi ifuatwe na ipi isifuatwe. Huyu mama angekuwa na makaratasi yanayotakiwa angeendelea na safari. Kwanza unajuaje ni kweli anaenda Kenya. Unajuaje ni Mrundi. Kwa nini hakuwa na passport? Je huko Kenya angeingiaje bila passport? Si angeisha kurudishwa mpakani. Kama alipata uchungu na kwenda Nyasho Clinic, si ni afadhali kuliko kupatia uchungu ndani ya gari ambapo huduma ya ukunga hakuna?
Na kukimbia kwa wahusika unaitaje hiyo tabia!
 
Mimi napendekeza Uhamiaji na Polisi zifutwe, Jwtz ifanye majukumu yao!!! Gademiti,!!
 
Acha upuuzi wako, mambo mengine unatumia akili tuu sio kujifanya unafuata sheria za kufikirika na unauliza passport wakati wenye nazo hata one percent ya nchi nzima hawafiki
Mimi napendekeza Uhamiaji na Polisi zifutwe tuanze upya na chombo kingine !!
 
Tunalaumu kumtelekeza mtuhumiwa wenu!
Ubalozi wa Burundi ulipaswa kuja kumhudumia subject alien wao…

Tanzanian constitution does not guarantee civil protections for non citizen aliens…

Boarder patrol agents did everything by the book…
 
Kule Kigoma Kuna mzee mmoja alimwita Mmbwa wake imagiration sijui ndivyo inavyoandikwa, Basi kila akipita pale mpakani anamwita hivyo Basi wake jamaa wa uhamiaji wakampiga risasi yule mmbwa.
 
Ubalozi wa Burundi ulipaswa kuja kumhudumia subject alien wao…

Tanzanian constitution does not guarantee civil protections for non citizen aliens…

Boarder patrol agents did everything by the book…
Je muliwaasiliana na huo Ubalozi wa Burundi!?
 
Back
Top Bottom