Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 128,308
- 245,426
Hii ndio taarifa mpya kutoka Uhamiaji iliyotolewa leo na Msemaji wake Paul Mselle.
Paul Mselle amesema haya...
Pasi ya kusafiria ni 'document' ya kiusalama na ni haki ya kiusalama na ni mali ya Serikali, pale ambapo mtu ataitumia vibaya basi anaweza akanyang’anywa
Pasi ya kusafiria sio kitambulisho kusema mtu achukue abaki nayo ndani ni lazima kuwe na dhumuni la safari, kama hauna safari hatuwezi kukupa pasi ya kusafiria
Mtu atakayepoteza Pasi yake ya kusafiria (Passport), itamlazimu kutoa taarifa Polisi pamoja na kutangaza kwenye gazeti na kwamba ni lazima atoe kiasi cha shilingi Laki tano kwa kupoteza Passport hiyo, na ili aweze kupata nyingine.
Kumekuwa na changamoto ya kuchelewa kwa pasi ya kusafiria sababu unakuta mtu hajakamilisha vigezo vya kupata pasi ya kusafiria. Kuna wengine wanawasilisha vyeti vya kuzaliwa ambavyo haviko kwenye mfumo wa RITA na ukimuuliza alikipataje anasema alimtuma mtu kwa maana ya vishoka na hawa unakuta wengine ni raia wa Tanzania na wengine sio raia wa Tanzania
Wengine nao unakuta taarifa za cheti cha kuzaliwa zinatofautiana na taarifa za vitambulisho vya Taifa, unakuta kwenye Kitambulisho cha TAIFA(NIDA) kazaliwa Temeke kwenye cheti kazaliwa Morogoro.
Passport.png