Uharaka unahitajika kwenye maamuzi ya CHADEMA

Mzee ulitaka Chama kianhukie kwa Cecil Mwambe au Sumaye?
Chama kingekuwa wapi kwasasa! binafsi naheshimu mawazo yako lkn msijifananishe na ccm kujenga Chama Cha upinzani kwenye ncha za Africa na Tanzania yenye vijana wanaowaza kununulika Refer Katambi na Silinde sio jambo dogo! Lazima kujilidhisha nani unamuachia Chama ... hata hivyo Mbowe alishatangaza baada ya kipindi hiki kuisha hatagombea
 
Unatumia mifano batili kujiaminisha jambo, kweli ni haki yako!.
 
Heri umemwambia
 
Nilichogundua wanaoalamikia ujio wa Lowasa nakutaka Mbowe aondoke ni wadau wa Slaa kitu hataki kusema hata Slaa ni uzao wa ccm amekuja Chadema baada yakukatwa kwenye Ubunge huko ccm
Hebu tuwaze kwa pamoja uchaguzi wa mwenyekiti uliopita Sumaye ndio amekuwa mwenyekiti guess what happened! kujenga Chama kinatakiwa maarifa mengi mfano sasa hivi Mnyika ni uzao Cha Chadema hajaazimwa popote! uchaguzi wa 2020 kwa mara ya kwanza wametoa mgombea wao ambae sio wakuazima manake inavyokwenda mwisho Chama kitabaki kwa watu sahihii...hizi Lawama zingine ikiwa ni kweli ni watu wa mageuzi lazima muwaze mbali ya Sura za watu
Chadema inategemewa na wengi angalia sasa hivi Chama kilivyo kimya watu wanavyolalamika je wakikabidhiwa watu wanaowaza teuzi Chama kikiuzwa?
 

Mkuu hata CCM wanasema wanajua wamechokwa, ila hawaoni chama cha kukiachia nchi. Je unakubaliana na hayo maneno yao? Sasa hamashia hayo kwa Mbowe, ni kweli hakuna mwingine huko CDM anayeweza cheo hicho?

Na kama ni kweli CDM hakuna anayeweza kuwa mwenyekiti zaidi ya Mbowe kitu ambacho si kweli, basi hicho chama ni cha kukiangalia kwa umakini mkubwa.
 
Unatumia mifano batili kujiaminisha jambo, kweli nI haki yako!.

Kwako ni mifano batili, ila kwangu ni mifano halisi ya rejea. Na sina tatizo kwenye kutofautiana na ww kwenye hili maana ndio afya ya mjadala.
 
Hapana hoja yangu sikwamba hakuna mtu mwingine huko Chadema lkn hatuwezi kuwaiga ccm Mbowe huu ni msimu wake wa mwisho mwenyewe alishasema lkn ukweli unabaki tu kwamba kwa uchaguzi uliopita angekuwa Sumaye au Mwambe naamini muda huu tungekuwa tunajadili mengine
ombi langu tuwasaidie Viongozi wetu tuwashauri inapobidi lkn tusiwakatishe tamaa mpaka sasa Chadema imekuwa taasisi kubwa mtu anaechiwa dhamana lazima aeleweke!
mtu kama Mnyika alikuwa kwenye target yamanunuzi lkn aliweka msimamo na leo ni Katibu mkuu wa Chama sasa watu wa namna ile ukiwapa dhamana yakuongoza Chama unahakika kiko kwenye mikono salama
 
Soma tena hoja yote uelewe nilichoandika mimi situmii utumbo kufikiri
Hoja iko wapi!

Unawaponda watu kwakuwa kabla ya kuingia chadema walikuwa kwenye vyama vingine. Huyo lisu unayemsema kama wa kwenu unajua kabla ya kuingia chadema alitokea wapi?!
 
Hapana hoja yangu sikwamba hakuna mtu mwingine huko Chadema lkn hatuwezi kuwaiga ccm Mbowe huu ni msimu wake wa mwisho mwenyewe alishasema

Hii si mara ya kwanza kutamka hivyo. Muda ukifika kundi la chawa wake wataigiza kumshinikiza kugombea tena na kuigiza kumchukulia fomu. Kuna mtu atakuwa na ubavu wa kupinga?

Mimi hata hivyo nishaweka wazi mara nyingi humu kuwa kama mtu anachaguliwa kihalali bila mizengwe, na uwezo wa kuongoza anao, hili suala la kuwekeana ukomo siafikiani nalo.
 

Ukipitia post zangu kama una muda maana sio lazima, mimi sijawahi kuwa muumini wa kuwapa nafasi viongozi waliotoka CCM, ndio maana niliwahi kupendekeza itungwe sheria kuzuia mtu kugombea nafasi yoyote ndani ya CDM bila kuwa ameitumikia CDM she chini ya miaka mitano. Na kuwekwe kifungu kidogo kama ametoka chama kingine basi isiwe chini ya miaka 7, huku mwenendo wake ikichunguzwa.

Ukitazama vizuri zaidi % kubwa ya viongozi wa CDM waliorubuniwa kwenda kuunga juhudi ni waliokuja na mafuriko ya Lowassa. Hivyo hao akina Mwambe, Sumaye nk ni katika kundi la wahuni waliorukia mafanikio ya CDM. Chama kilipaswa kuwa makini na wale wahuni waliosubiri mafanikio.

Simkatishi kiongozi yoyote tamaa kwani natambua mchango wao muhimu kwenye chama, lakini kila jambo lina wakati wake.
 
Mambo haya na madhaifu mengine kadhaa ndio yanapelekea mimi kutaka Mbowe akae pembeni kama mwenyekiti ili aingie mtu mpya na mbinu mpya, kwani kwa sasa ni sahihi kabisa kwake kukaa pembeni
Wakati kama huu mnapofanya mazungumzo na Ccm, Mbowe ana umuhimu wake.
 
Wewe hujaona tofauti kati ya Magufuli na Salimia, hata kama lengo lao ni moja?
Mbowe aliweza kwa ushupavu mkubwa kumkabili Magufuli na kushinda. Huyu Maza Mizinguo yeye ana 'approach' tofauti ya kuendelea kufikia lengo lile lile la kuibakisha CCM madarakani, na kwa ubovu uleule ndani ya chama.
Na kama hujui, CCM ya Salimia haiko mbali sana na CHADEMA ya Mbowe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…