zitto junior
JF-Expert Member
- Oct 7, 2013
- 20,537
- 31,729
Ndugu Wana jukwaa hasa wadau wa demokrasia kuna tatizo kubwa sana nimeliona kwenye uharaka wa kufanya maamuzi ndani ya CHADEMA. Hapa tuangalie baadhi ya mifano.
1. Kuondoka kwa Dr. slaa kuliichukua CHADEMA zaidi ya Mwaka mzima mpaka kuziba nafasi Ile. Ikimaanisha kama Dr Slaa angeamua kurudi kwa style ya Lipumba, CHADEMA ingepasuka kama CUF lakini hatukujifunza tu.
2. Kuwafukuza wabunge 19 wa viti maalum.
CHADEMA mapema sana mwaka jana waliafikiana kuwafukuza wabunge 19 baada ya kukiuka maazimio rasmi ya chama na pia kukaidi wito wa kamati kuu. Cha kushangaza tumekaa mwaka mzima ndio tunakuja kuwafukuza rasmi kupitia rufaa za Baraza kuu. Nachojiuliza mwaka mzima tunasubiri Nini? Sasa wameshajipanga tutaburuzana na kesi mpaka 2024 huko ndio waje kuondoka when it's too late na damage imefanyika.
3. BAWACHA Haina mwenyekiti!!
Baada ya Mdee kuondolewa kwenye chama nilitegemea haraka sana nafasi zote zizibwe, Nikashangaa Sharifa Suleiman ambaye ni makamu mwenyekiti ZNZ ni Kaimu-Mwenyekiti mpaka leo. Sasa tunakwama wapi kuziba hiyo nafasi? Hivi Mdee akisema Leo anarudi kwenye uenyekiti BAWACHA na akapewa back up na msajili (maana Bado kiti kipo wazi) unadhani damage itakua kubwa kiasi gani?
As much as tunakipenda hiki chama lakini kwenye maamuzi magumu tuwe na uharaka otherwise tutaendelea kulalamika tunahujumiwa kumbe tunaacha gaps wenyewe na maadui wanazitumia kutunyooshea.
Cc Tindo Erythrocyte Proved