Salamu kwenu wapenda mpira!
Leo nimeshangazwa na kitendo cha wanasimba kuharibu viti na kuvitupa baada ya kufungwa utadhani vile viti ni mali ya refa au Yanga. Kitendo kingine kilichonichekesha ni pale mchezaji wa Simba alipotakiwa acheze fair play, cha ajabu akaugongesha kwa makusudi ule mpira kwa mchezaji wa Yanga ili utoke halafu warushe wao na adhima yake ikatimia,akauchukua mpira haraka na kumrushia mwenzake na refa wa mwendokasi akaruhusu mchezo. Baada ya hapo nikagundua kucheza hapa hapa tz tu kuna athari kubwa kwa wachezaji, manake nikawafananisha wachezaji wa simba + refa na wale wachezaji na mwamuzi wa kitambo kile kwenye gazeti la Sani. Hasa hasa wale waloitwa Bush Stars!!