Uharibifu wa viti zaidi ya 200 uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba

Uharibifu wa viti zaidi ya 200 uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba

acheni ushamba fuatilieni ligi ya brasil, Argentina au Urusi mtaniambia watu wanachapana mpaka kuuana na wanaharibu uwanja sembuse bongo
Acha kutetea ujinga mkuu, kwa hiyo kama Brazil wanauana ndio na sie tuuane? Unatumia nini kufikiri wewe ndugu[emoji51]
 
simba wameshinda goli 1kwa mguu na yanga wameshinda goli1kwa mkono ILA sababu mpira ni wa miguu matokeo simba 1 yanga 0[emoji35] [emoji35] [emoji35]
 
Kosa akose Ngoswe adhabu ipewe kiti changu wapi na wapi?? Hicho kiti kilitoa kadi?? Uvunjifu wa viti ni kuonesha udhaifu wako. Mashabiki wa Simba hawataki kufungwa wanataka wao tu ndo washinde. Huo sio mpira labda muanzishe wa kikwenyu.
 
Ningekuwa mm natoa adhabu basi ningempa adhabu hiyo refa haiwezekani goli la ukweli la ajibu anasema sio goli,goli la tambwe la mkono wa wazi kabisa anasema goli unategema nn kitatokea kwa mechi kubwa kama hii



Kwa hivyo Kila klabu ikiona refa achezeshi vyema iwaamuru Mashabiki waanze kung'oa viti ili refa awe anachezesha vyema...?

Ni Marefa wangapi wamejirekebisha tangu muanze kung'oa viti......?
 
1475350190257.jpg


Aiseee mpira wa mkono au wa mguu
 
Vurugu Mchezoni zipo Dunia nzima tatizo lako si mfuatiliaji. Egypt watu walilete Usengerema Kama huu watu wakauana, Congo, Ghana kote the same story!


Kwa hivyo unatushauri tuendelee KUIGA hizo vurugu zao?
 
Hivi haya makundi ya wahuni ni nani anaye yaendekeza? Hebu jionee uharibifu wa Viti katika uwanja wa Taifa DSM wakati wa mchezo wa Yanga na Simba.

Huu uhuni na wahuni wahusika wanapaswa wachukuliwe hatua stahiki. Haiwezekani mali ya Taifa inaharibiwa kiasi hiki, Ikumbukwe kuwa hii tabia si Mara ya kwanza kujitokeza.

Hivyo Mamlaka zikishindwa kuchukua hatua stahiki wajue kuwa ipo siku hili litatojea tenaView attachment 410423View attachment 410424View attachment 410425View attachment 410426
Wanaume wa dar hao bora makao makuu yahamie dodoma
 
Nadhani bila mashabiki kuonyesha hasira hizo leo refa angetoa kadi nyekundu zaidi ya moja.Nakama waamuzi ndio hawa,iko siku hali itakuwa mbaya sana uwanjani!



Hapana haiwezi kuwa mbaya zaidi. Naona punde tu TFF itaanza kupiga Marufuku wavuta Bangi kuhudhuria Mtanange wowote ule wa Simba na Yanga...
 
mi nalia na refa!!!! hatakama simba watalipa fain refa hapaswi kuchwa hivi hivi!!!! hatakama si mshabiki wa mpira jamani yale maamuz hamna kabisaaaaa!!!
 
Nasikia leo mnafanya sherehe ya kutoa sare na WAKIMATAIFA WENYE SOKA LAO BONGO .........Hongereni, angalau soka lenu linaanza kuja kwa mbaaaaaaali.

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Simba na washabiki,viongozi watawajibika kwa ilo swala me sioni sababu ya kualibu Mari ya umu eti kisa refa haingii akilini
 
Tambwe mtu mbaya sana, kagoli kamoja tu viti kwachukwachu. Siye tulimiminwa 5 na hatukurusha hata chupa. Mjifunze ustaarabu wa matopeni, haya lipeni fine na mabomu juu...


Tambwe ana historia nzuri sana na hawa MATOPENI FC. Kila akikutana nao lazima awapigepo cha Ukwezi.....
 
Naunga mkono kung'olewa kwa viti. Huyu refarii alikuwa amefungiwa kuchezesha mechi yoyote kwa mwaka mmoja. Malinzi alipoingia madarakani akawasamehe waamuzi wote waliofungiwa, na huyu jamaa akaponea hapo. Badala ya kuonyesha watanzania kuwa ameshajirekebisha, anarudia makosa makubwa matatu; kukataa goli halali, kukubali goli lisilo halali na kutoa kadi nyekundu. Sasa huyo Malinzi aliyemfungulia kifungo ndio atengeneze viti, maana aliwaona waliomfungia jamaa kuwa ni wajinga!
 
Back
Top Bottom